Kesi ya Lulu: Polisi asema alikuta chupa ya Jack Daniel na Panga kwenye tendegu la kitanda

Kesi ya Lulu: Polisi asema alikuta chupa ya Jack Daniel na Panga kwenye tendegu la kitanda

lulu+pic.jpg

Daktari amesema alipompima Kanumba kiwango cha sukari kilikuwa cha kawaida lakini alipompima shinikizo la damu hakupata kabisa mapigo ya moyo.

Daktari Paplas Kagaiya aliyekuwa akimtibu msanii maarufu wa fani ya uigizaji filamu nchini, Steven Kanumba ametoa ushahidi Mahakama Kuu akieleza hali aliyoikuta alipokwenda nyumbani kwa msanii huyo.

Mbali na Dk Kagaiya, askari Polisi aliyemtia mbaroni msanii wa kike Elizabeth Michael, maarufu Lulu, pia ametoa ushahidi mahakamani hapo leo Ijumaa Oktoba 20,2017.

Lulu ambaye yuko nje kwa dhamana anadaiwa kumuua Kanumba bila kukusudia kosa analodaiwa kulitenda Aprili 7,2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Kanumba.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi kutoa ushahidi, Dk Kagaiya amesema alipofika nyumbani kwa Kanumba alikuta akiwa ameanguka na alimpima kiwango cha sukari na shinikizo la damu.

Amesema kiwango cha sukari kilikuwa cha kawaida lakini alipompima shinikizo la damu hakupata kabisa mapigo ya moyo, hivyo alishauri Kanumba apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dk Kagaiya amesema daktari katika kitengo cha dharura Muhimbili alipompima Kanumba aliwaeleza alikuwa tayari ameshafariki dunia.

Baada ya kupewa maelezo hayo, amesema walikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Selander Bridge.

Shahidi huyo alipoulizwa na wakili wa Lulu, Peter Kibatala kama kuna vitu vyovyote alivyoviona eneo la tukio chumbani kwa Kanumba, ikiwemo chupa ya pombe alisema hakutambua chochote.

Katika hatua nyingine, askari Ester Zefania kutoka Kituo cha Polisi Msimbazi akitoa ushahidi amesema alikwenda kumkamata Lulu alfajiri, eneo la Bamaga kwa msaada wa Dk Kagaiya, ambaye walikuwa wakiwasiliana kwa simu.

Akijibu swali la wakili Kibatala kama alimpeleka Lulu hospitalini kwa matibabu, shahidi huyo amesema ni kweli alimpeleka hospitali.

Hata hivyo, Zefania amesema Lulu hakumueleza kuwa alipigwa na Kanumba na wala hakuona majeraha. Alijibu hayo baada ya kuulizwa swali na wakili Kibatala.

Zefania amesema aliagizwa na mkuu wake wa kazi ampeleke Lulu hospitalini lakini hakujua alikuwa ana matatizo gani.

Pia Afisa wa Polisi ametoa ushahidi wake kwa Mahakama wa hali ya Mazingira waliyoikuta chumbani kwa marehemu Kanumba, ambapo ASP Ester zefania ameileza Mahakama kuwa alipoingia chumbani kwa Kanumba alikuta kitanda kimevurugika kama kimetumika, stuli iliyokuwa na chupa ya Sprite, glass yenye kinywaji.Pia chupa ya Whisky aina ya Jack Daniel na kwenye tendegu la kitandana kulikuwa na Panga.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Sam Rumanyika itaendelea Jumatatu Oktoba 23,2017 kwa upande wa mashtaka kukamilisha ushahidi wake.
mkuu ,kitanda kimevurugika kama kimetumika??fafanua zaidi MKUU.
 
Good question...hii Lulu aitumie kwenye utetezi

labda aliti.wa....sio rahisi kumuua mtu.....uliyetoka

kuti.ana nae
Sasa hakuna mahali rahisi sana kwa mwanaume kukamatiwa chini na mwanamke aidha kuuwawa au vyovyote viwavyo zaidi ya kitandani. Mwanamke amekuwa silaha bora ya wakati wote kwa wanaume amini usiamini!!
 
anataka kutuonesha anajiamini sana...
mi nadhani angeinama tu awe anasali sala ya baba yetu uliye mbinguni...
hizi sio zama za jk

kila la kheri kwake
Huezijua labda ashajua nini kitaendelea! Kwani lulu ni Msukumaa?? Maana hii nchi yetu bhana wanaojiamini kwasasa daaah[emoji36] Ngoja waje[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Huezijua labda ashajua nini kitaendelea! Kwani lulu ni Msukumaa?? Maana hii nchi yetu bhana wanaojiamini kwasasa daaah[emoji36] Ngoja waje[emoji125] [emoji125] [emoji125]
mhaya wa kagera. mixer mchaga.

labda kashatoa uchi wake ndo ajue nini kinafuatia.
binti hajielewii..huyu kibatala mwenyewe alijitolea tu bure baada ya kuona hana msaada...
 
mhaya wa kagera. mixer mchaga.

labda kashatoa uchi wake ndo ajue nini kinafuatia.
binti hajielewii..huyu kibatala mwenyewe alijitolea tu bure baada ya kuona hana msaada...
Hapo sasa ndio wengi wanafumbwa macho. We unadhani nani keshapewa uchi Hakimu au wakili Kibatala? Halafu Kwani kosa la kuua mtu bila kutegemea sio kosa hii inakaaje?? Hapa wanasheria naombeni majibu japo sisi sio mahakimu!!
 
kesi haiendeshwi na wakili mmoja..wapo zaidi y mmoja tena wanawake kwa wanaume.
kuua bila kukusudia ni kosa..na lina kifungo.
 
Hivi unakumbuka ile kesi ya Dittopile ambayo nayo ilikuwa figizufigizu?
ditopile aliua..kwa kukusudia
alikua anajitetea hivo tu ili adhabu ipungue..chezea kifungo cha maisha!
alikua barabaran foleni ndefu sasa dereva wa daladala aliovateki na kujikuta anapiga pasi(kulikwaruza) gari la ditopile..mzee nae alikua na jazba..si unajua uheshimiwa...nahos dereva alimjibu vibaya..dito akachomoa bastola fasta puuuh!kamshuti dereva wa daladala kichwani.
na konda alikuwepo kashuhudia..
dito katelekeza gari na bastola kakimbia..ila walimwona.
alihukumiwa kifungo cha maisha akajinyonga jela.
 
Back
Top Bottom