Kesi ya Lwakatare kuchukua muda zaidi

Kesi ya Lwakatare kuchukua muda zaidi

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
Kesi tajwa huenda ikachukua muda zaidi, ikiwa haki itatendeka, kwa maana ya hadi wahusika wote washukiwa katika kesi hii watakapo hojiwa...
Kwa jinsi hali ilivyo sasa wanaopaswa kuunganishwa na kesi hii kwa maana ya kuhojiwa kwa kina ni
1.Mwigulu Nchemba,
2.Polisi waliopewa mkanda 'na Mwigulu miezi mitatu iliyopita'
3.'Wasamaria wema kutoka CDM waliomkabidhi mkanda Mwigulu'
Ikiwa haki haitatendeka, basi 1-3 itawekwa kando na vyombo vya dola pamoja na TISS yao,
na kwa vyovyote mwisho wa siku kesi itakuwa sio kesi, ila hujuma na ukandamizaji wa vyombo vya dola kwa CDM.
 
Mkuu ulicho kiongea ni kweli kabisa ; Lakini ni vyema magamba wakasoma alama za nyakati na wakalielewa hili mapema " siku zote ukweli una tabia ya kuchelewa, na kamwe huwezi kuuzuia kufika uliko kusudia"
 
Mwigulu si amtaje mtu tu bali atoe ushahidi usioacha shaka kuwa huyo anayemtaja kumpa ni kweli alimpa. Najua anasema hivyo kuwa kapewa ili kuleta mgawanyiko na kutoaminiana kati ya wanaCDM. Anaweza kumtaja Naibu katibu mkuu mwenzake yaani ZZK, Nassari, Leticia Nyerere au hata Dr. Slaa ili tu alete mkanganyiko na kuzorotesha M4C na mikakati ya kukijenga CDM.
 
wewe unapendekeza awe amepewa na nani huo mkanda.
 
Mkuu ulicho kiongea ni kweli kabisa ; Lakini ni vyema magamba wakasoma alama za nyakati na wakalielewa hili mapema " siku zote ukweli una tabia ya kuchelewa, na kamwe huwezi kuuzuia kufika uliko kusudia"

mimi imani yangu bado haijabadilika ktk hili mbichi na mbivu zitafahamika tu hata iweje labda watu waihonge mahakama.
 
Unajua kila jambo lina mwishowe, acha ichelewa lakini haki ya mtu haipotei.Kwa ukweli mtu wa kwanza katika kesi hii ni mwigulu ambaye ndo anayejua huo mkanda alipewa na nani,ila kama alompa hakupa mbele ya shahidi yeyote ujue kazi anayo.
 
Mwigulu anajutia hili Gemu alilocheza,kinachomuumiza ni hatua yake ya kumtumia Ludo 50elfu kupitia line yake..hapo nna mashaka na akili yake.Namfananisha mwigulu na jambazi aliyekwenda kuiba afu akadondosha kitambulisho kwa makusudi.
 
Now ccm has a price to pay for having Mwigulu in it.... mdomo wa Mwigulu utakitafuna chama chao, just wait and see na jinsi jeshi letu la polisi linavyocheza sarakasi zake kwenye suala hili..
 
Now ccm has a price to pay for having Mwigulu in it.... mdomo wa Mwigulu utakitafuna chama chao, just wait and see na jinsi jeshi letu la polisi linavyocheza sarakasi zake kwenye suala hili..

Kikwete huwapa vyeo washikaji wake kishikaji, alichoongea Mkapa kule Bukoba safari hii kama akiwa mmoja wa waandamizi wakuundani ya CCM inatoa picha kamili ya kile ambacho wengi walioko CCM wanajutia sasa Kikwete alipokifikicha chama cha CCM.

Kwa maneno mengine Mkapa yuko Tayari kutumbukiza kura kwenye sanduku itakayokuwa kinyume cha matarajio ya CCM kama isingekuwa kura ya siri. Tamko la kule Kagera ni kuchangamkia upinzani.
 
Mwigulu anajidai ni mtoto wa mjini kumbe hakuna anachojua.polisi nao kwa ujinga wanahangaikia kumbeba mwigulu vinginevyo wangesha itupilia mbali huo usanii.
 
In short ni kuwa hakuna lolote katika hayo mashtaka...hii habari itaenda mwisho wa siku utasikia mahakama imeshindwa kuwatia hatiani washtakiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha.
Kumbukeni hii ndiyo kesi ya kwanza inayohusisha ushahidi wa picha za video...
 
Naskia shehe yahya amefariki, kumbe aliyerithi mikoba yake yuko hapa jf
 
Mi nlitegemea kuona watanzania wote kwa pamoja tungeweka pembeni itikadi za vyama na kukemea vitendo hivi vya kigaidi badala yake wabongo tunautetea
 
Mi nlitegemea kuona watanzania wote kwa pamoja tungeweka pembeni itikadi za vyama na kukemea vitendo hivi vya kigaidi badala yake wabongo tunautetea
kwenye hili la lwakatare tunalia na ukandamizaji wa haki za binadamu kwa kutumia polisi ugaidi tumeusemea sana kwenye ishu ya mwakyembe, mwandosya, mwaikusa, ulimboka na mwangosi lakini kwa kuwa wahusika ni wa kubwa serikalini basi wameziba masikio
 
Back
Top Bottom