Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 534
Naanza kupata picha juu ya kesi ya Lwakatare. Hii si kesi ya kweli kwani kama kweli serikali yetu ingeamua kupambana na magaidi ingeanzia mbali:
1. Waliomtesa Dr. Ulimboka ni akina nani? Je, Ramadhani Ighondu ni nani? amejificha wapi hata asiweze kukamatwa na kuhojiwa tu kisha aachiliwe maana yeye ni mtukufu sana hawezi lala sero? Mnakumbuka hata Ulimboka mwenyewe amemtaja mtu huyu?
2. Waliomtesa Kibanda ni akina nani na wako wapi? Hatujasikia hata mmoja kakamatwa hata kuulizwa tu ndg unaishi wapi.
3. Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu. Hisia zangu na za watanzania wengi ni kuwa kesi hii ni ya kisiasa! Ndiyo, kwani Ulimboka na Kibanda ambao wametendwa si watu? Mbona mmeshabikia la Lwakatare kwa haraka namna hii? Hamuoni kuwa nia si Lwakatare bali ni Chadema? Hamuoni kuwa kinachopangwa ni ushabiki wa kisiasa ili kuthibitisha kauli za Mzee wa Gombe na wenzake kuwa CDM itakufa kabla ya 2015? Hata kama Lwakatare atafungwa, tutajua amefungwa kisiasa kwa jinsi mlivyolivalia njuga jambo hili na kuacha haki na maisha ya wenzetu walioonewa wakiteseka bila ya msaada wowote.
Kumbukeni jamani udhalimu una mwisho na mwisho wa mdhalimu ni mbaya. Alikuwepo Amin wa Uganda, yuko wapi? Gaddafi yuko wapi? Yule wa Misri naye yuko wapi? CCM mnang'ang'ania madaraka ili kulinda mlivyotuibia ili muweze kuendelea kutuibia. Sasa hata sisi wakulima wa vijijini tumewashtukia!
Za mwizi arobaini, na ya kwenu imekaribia! Mtakuja kusema tulisema!