Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu jamaa anatetwa na mwanasiasa mwanasheria Bob Makani. Hivi bado yuko kwenye siasa za upinzani au ameshahamia CCM kundi la mafisadi? Upinzani wa siasa za nchi hii unaniacha na wasiwasi mkubwa saa zote, ni njaa ama nini? Hata kama ni njaa, mpinzani wa ufisadi na wizi huwezi kujitokeza front line kumtetea mtuhumiwa wa ajenda hiyo - ndiyo ana haki ya utetezi lakini wapo wasiofungamana na upande wowote.
Mkuu,
Uwakili unakula kiapo kama udaktari tu, huwezi kukataa kumhudumia mteja kwasababu tu morally hukubaliani na alichofanya. Huwezi kumlaumu Makani, Marando au Lissu kwa kuangalia watu wanaowatetea mahakamani.
Watakuwa wanakiuka maadili ya kazi zao kama watakaa kuhudumia wateja kwasababu ni mafisadi au majambazi au wauaji.
Mkuu,
Uwakili unakula kiapo kama udaktari tu, huwezi kukataa kumhudumia mteja kwasababu tu morally hukubaliani na alichofanya.
Ni Kweli, lakini tuaachiwa own judgement juu ya mteja gani tumwatend. Kwa mwanaharakati, mtetea haki za binadamu hawezi kuchukua kesi ya kumtetea mvunja haki hizo, hataeleweka mkuu.
Huwezi kumlaumu Makani, Marando au Lissu kwa kuangalia watu wanaowatetea mahakamani.
Sitawaelewa siku nikisikia wanawatetea mahakamani mafisadi kama wa EPA, Rostam et al. Kwanza naturally mteja atamwendea mwanasheria atayekuwa tayari kubeba matakwa yake - haitatokea mwenye kesi obvious ya ujambazi kutetewa na advocate obvious mlokole kwa mfano.
Watakuwa wanakiuka maadili ya kazi zao kama watakaa kuhudumia wateja kwasababu ni mafisadi au majambazi au wauaji.
You do not enjoy diplomatic immunity in your own country. Wangekuwa wameshtakiwa Italia ingekuwa ina make sense.
Afu alikuwa ni Professor wa Sheria UDSM.
=====================================Ebwana ee, jamaa sasa anakumbatia unyasi!Inaelekea mlango wa lupango uko wazi na una mkaribisha!!!
Diplomatic Immunity? Ukiiba fedha za Tanzania ukiwa nje ya Tanzania unaweza kuwa na diplomatic immunity huko nje, lakini ukisharudi Bongo hakuna immunity.
Nielewavyo diplomat hana immunity nyumbani kwake. Labda Marando adai ruhusu ya DPP ilitakiwa (kama haikutolewa).
Noana wakubwa wamejikita kwenye technicality zaidi siku hizi. Liyumba alisababisha upotevu wa fedha, sio kwamba alizipoteza yeye.
Yetu macho. Sidhani kama kuna kigogo hata mmoja atapatikana na hatia. Yanayoendelea ni danganya toto tu.