Kesi ya Mali ya Wakfu Masjid Mwinyi Miaka 32 Bado Hukumu Kupatikana

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Jaji Mkuu,
Majaji,
Mawakili na Mahakimu wote

Ukweli kuhusu umiliki wa viwanja 32/77 Somali Street na 17/56 Mtaa Mchikichi Kariakoo Dar es Salaam.

Mimi Abeid Maulid Abeid umri wangu hivi sasa ni miaka yangu 78.

Ni Imamu wa Masjid Mwinyi uliopo Mtaa wa Moshi, Ilala Boma toka mwaka 1990 lakini pia nilikuwa Imamu na Khaatibu wa Sala ya Ijumaa Msikiti Manyema, na pia Mdhamini.

Naomba maelezo haya yavifikie Vyombo vya Sheria, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mamlaka za Nchi.

Awali nilikuwa nikiishi mtaa wa Tabora, Ilala, jirani na Masjid Mwinyi, hivi sasa naishi Mbagala Charambe.

Wakati wa ujana wangu miaka ya 1960 mwanzoni hadi 1970 mwanzoni nilipata kuwa mchezaji wa timu ya Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars).

Nikiwa Mchezaji wa mchezo wa mpira, pia nilikuwa mfanyakazi serikalini, Wizara ya Kilimo na Mifugo nikiwa Afisa Mifugo.

Marehemu Hajjat Aziza Omar

Hajat Aziza Omar na ndugu yake Asha Omar ni ndugu waliokuwa wakiishi Mitaa ya Somali na Mchikichi Kariakoo Dar es Salaam.

Katika uhai wao walifanikiwa kumiliki nyumba.

Aziza Omar akimiliki nyumba Na. 32/77 Mtaa wa Somali na nyumba Na. 20 Mtaa wa Moshi Ilala Boma (hivi sasa Msikiti Miwnyi).

Lakini pia alikuwa akimiliki nyumba nyingine mtaa wa Congo ambayo kwa sasa inamilikiwa na Pius Kipengele.

Hii aliipata kwa manunuzi yenye shubha.

Aidha nduguye (dada yake) Asha Omar akimiliki nyumba Na. 17/56.

Mabibi hawa walikuwa na asili ya Singida, walikuwa waumini wa dini ya Kiislamu na hawakuwa na ndugu wengine wa nasaba kipindi hicho cha umri wao wakiwa Dar-es-Salaam.

Baada ya kufariki dunia Asha, mdogo wake Aziza Omar alirithi nyumba Na. 17/56 Mtaa wa Mchikichi.

Mwaka 1990 Aziza alifanikiwa kwenda Hija, ndio asili ya kuitwa Hajat, na aliporudi aliigeuza nyumba yake iliyopo mtaa wa Moshi Ilala Boma kuwa msikiti na katika kuufungua msikiti huo alimuomba aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati huo, Ali Hassan Mwinyi kuwa Mgeni Rasmi.

Na aliupa msikiti huo jina la la rais huyo.

Ndiyo asili ya kuitwa Msikiti au Masjid Mwinyi.

Aidha aliniteua mimi Abeid Maulid Abeid kuwa Imamu wa swala za kawaida, kwa kuwa hapakuwa pakiswaliwa swala ya Ijumaa.

Daniel Zakaria na Pius Kipengele

Daniel Zakaria alikuwa mpangaji wa Hajat Aziza Omar nyumba Na 32/77 mtaa wa Somali.

Pius Kipengele akiwa mfanyabishara maeneo ya Kariakoo alikuwa mpangaji pia wa Hajat Aziza Omar nyumba ya mtaa wa Moshi Ilala Boma kabla haijageuzwa kuwa msikiti.

Wakati huo akiwa na wapangaji wenziwe, miongoni mwao alikuwa Afisa Ardhi Manispaa Ilala Bwana Komba ambaye baada ya kustaafu alirejea kwao Songea (0756214978).

Daniel Zakaria, sasa marehemu, hakuwa na shughuli maalum.

Alikuwa akitumwa na Hajat Aziza kumtekelezea baadhi ya shughuli zake za nje, kama ulipaji umeme, maji na nyingine ndogo.

Daniel Zakaria si yeye tu aliyekuwa akitumwa shughuli hizo, bali alikuwepo Abdallah Rashid (marehemu sasa) ambaye ni mmoja wa watu aliowataja katika kiapo (wasia) chake.

Aidha Pius Kipengele kama mfanyabishara wakati huo hadi sasa alikuwa akimtumia kwa shughuli zake lakini pia akimfahamu kama mtu aliyekuwa akiishi nyumba ya Hajjat mtaa wa Somali.

Muungano wao na kile kilichokuja kufanyika baada ya kifo cha Hajjat Aziza, moja ya vimelea vyake ni hiki.

Kiapo na Kifo na cha Hajjat Aziza Omar

Kabla ya kufariki kwake, marhumat Aziza Omar aliandika Wasia (Kiapo) ambao upo ukiwa umesajiliwa Mahakama ya Mwanzo Mkwajuni (Kariakoo) mbele aliyekuwa Hakimu wa Mahakama hiyo, Mh. Jamila Ditopile.

Hila za Daniel(nyuma ya pazia akiwa Kipengele)

Kabla ya kufariki dunia, Hajat Aziza, aliishi maisha ya upweke mtaa wa Somali akihudumiwa kwa karibu na Abdallah Rashid.

Katika moja ya changamoto zilizomkuta bibi huyu ni pamoja kutendewa matendo ya udhalilishaji kutoka kwa Daniel Zakaria lakini kubwa zaidi kuibiwa hati za nyumba na nyaraka nyingine.

Mtuhumiwa wa wizi huu alikuwa Daniel Zakaria ambaye baada kutenda uhalifu huu alikimbilia kwao ambako alikaa hadi alipopata taarifa za kifo cha Hajat.

Kuripotiwa polisi Daniel Zakari

Kwa tukio la wizi, Hajat Aziza alitoa taarifa polisi kituo cha Msimbazi na kupata Report Book (RB) ambayo nakala yake ipo.

Daniel Zakaria hakuweza kupatikana hadi Hajat Aziza anafariki dunia mwezi June 1991.

Kwa dokezo tulizodokezwa, mipango ya wizi wa nyaraka za nyumba, na kurejea kimya kimya kwa Daniel Zakaria hadi kufungua Mirathi Mahakama ya Kisutu ilisukwa na Pius Kipengele.

,Mirathi ya Hajat Aziza

Wasia (kiapo) umetaja majina kadhaa likiwemo la Mwinshehe Mgumba na Abdallah Rashid kwamba, mara baada ya kifo chake ndiyo wawe wasimamizi wa Mirathi wakati huo huo aliwakana baadhi ya watu waliojinasibisha naye.

Wasia umeelekeza Nyumba zake mbili 32/77 Somali Street na 17/56 Mchikichi Street Kariakoo, zitumike kama rasimali (Wakfu) kuhudumia Msikiti Mwinyi.

Kwa ajili hiyo, mara baada ya kifo chake Mwinshehe Mgumba kwa niaba ya Masjid Mwnyi alifungua Mirathi Mahakama ya Kariakoo shauri Na 89/91 kwa niaba ya Masjid Mwinyi kuomba usimamizi kisheria.

Hii ikiwa ni mapema zaidi na hapakuwepo shauri lingine kama hilo.

Hata hivyo mirathi hii ilichelewa kutolewa hadi January 1992.

Hila za Daniel Zakaria na Pius Kipengele

Mara baada ya kusikia taarifa za kifo cha Hajjat Aziza, Daniel Zakari alijiitokeza Mahakama ya Kisutu kudai usimamizi wa mirathi akiwa na nyaraka zote za marehemu (alizoziiba).

Alifungua shauri hilo Na. 73/91 wakati tayari Masjid Mwinyi ikiwa imeshafungua Mirathi inayohusu Mali za Marehemu Hajat Aziza.

Tangazo la Mirathi alilitoa kwenye "Government Gazette" ambalo halisomwi mitaani.

Ndani ya siku chache zisizotimia 30 kwa mujibu wa sheria Mahakama ya Kisutu ikampa usimamizi.

Mara baada ya kupata usimamizi huo akawasilisha amri ya Mahakama Manispaa Ilala kwa ajili ya Umiliki.

Wakati anafanya haya, Masjid Mwinyi haikuwa na taarifa zozote.

Mwezi January 1992 Masjid Mwinyi kupitia mirathi aliyofungua Mwinshehe Mahakama ya Kariakoo ikapewa Usimamizi wa mirathi.

Ilipoanza kukusanya Mali za marehemu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nyaraka Manispaa Ilala, mirathi inayohusu Mali za Hajat Aziza iliyofunguliwa na Masjid Mwinyi ikagongana na mirathi iliyofunguliwa na Daniel Zakaria.

Kwa mgongano huu aliyekuwa Afisa Ardhi aliyeshughulikia suala hilo Bwana Komba pamoja na kuwajulisha Masjid Mwinyi juu ya utapeli wa Daniel Zakaria wakati huo akimshuhudia Kipengele akifika naye pale Manispaa, alimjulisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa Mama Kessy.

Wote wawili walijiuliza nini kifanyike?

Mkurugenzi Mama Kessy aliomba muongozo wa Mahakama Kisutu.

Aliyekuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Kisutu wakati huo Mama Natalia Kimaro akaelekeza usimamizi uwe wa aliyetangulia kuwa "granted" na ule wa mahakama ya juu ya nyingine ambayo kwa wakati Ile ilikuwa Kisutu.

Hata hivyo, kwa kuujua ukweli wa suala hilo na hila zilizokuwa zikiendelea baina ya Daniel Zakaria na Pius Kipengele, Mkurugenzi kwa ushauri wa Afisa Ardhi Mr. Komba, hakutekeleza maelekezo hayo hadi anahama Manispaa hiyo.

Kuhama kwa mkurugenzi huyo kulitoa fursa kwa Daniel Zakaria na mshirika wake, Kipengele kuendelea hatua za kufanikisha mchakato wa "usimamizi" kupitia Manispaa.

Daniel Zakari anakuwa Mmiliki toka Msimamizi, Pius Kipengele na Steven Mwamkoa wanakuwa wanunuzi.

Baada ya Daniel Zakari "kujimilikisha" kwa hila, ghushi na udanganyifu nyumba Na. 32/77, 17/56 na hata Msikiti Mwinyi (nyaraka zilizopo Manispaa ambazo zimekwisha muda zilisomeka nyumba ya Mtaa wa Moshi ambayo ni Masjid Mwinyi ni Mali ya Daniel Zakaria, na akiwa hai alishadai kuwa Msikiti huo ni mali yake), alimshirikisha pia Mchungaji Mtikila katika kudai huko ambako nusura kusababishe vurugu ya kidini kati ya Wakristo na Waislamu.

Yaliyojiri baada ya Daniel Zakaria kujimilikisha nyumba Na. 32/77 na 17/56

Pius Kipengele na mfanyabishara mwenziwe Steven wanakuwa wanunuzi.

Daniel Zakaria haraka haraka anawauzia mabwana hao.

Hii ikiwa ni mwaka 1993.

Pius "ananunua" nyumba Na. 32/77 anaigeuza nyumba hiyo pamoja na upangaji mwingine, kuwa Bar.

Steven Mwamkoa alinunua nyumba 17/56 iliyo mtaa wa Mchikichi jirani na Msikiti Mtoro.

Kufuatia hali hiyo na lawama kubwa kutoka kwa kuzingatia wasia wa marehemu na kwamba wasia ni jambo zito katika Uislamu na kwa shinikizo kutoka kwa waumini, pamoja na kujaribu kutafuta haki hiyo kwa njia za sheria, Mimi nikiwa Imamu na Khaatibu wa Swala ya Ijumaa, nilisimama katika Mimbar Msikiti wa Manyema siku ya Ijumaa nikaeleza mkasa huo kwa mamia ya waumini waaoswali hapo.

Hatua hiyo iliibua hasira na hamasa zilizowasukuma Waislamu kuvamia maeneo hayo.

Walianza nyumba ya Mchikichi wakaidhibiti kwa nguvu bila kufuata sheria kisha wakavamia nyumba ya Somali hali iliyozusha tafrani kubwa iliyovisukuma vyombo vya Ulinzi na Usalama kufuatilia kwa karibu.

Pius Kipengele na Steven Mwamkoa waenda kimya kimya kupata hati Wizara Ardhi

Wakati hayo yakijiri huku mtaani, Pius Kipengele na Steven Mwamkoa walipiga hatua kadhaa kimya kimya kujimilikisha kisheria Wizara ya Ardhi ambako walifanikiwa kupata hati.

Mafaili yaliyopo kwa Msajili naamini yanaonyesha umaalum wa usajili na umiliki wa nyumba hizi.

Naamini yanaweza kutoa picha fulani kwa jicho makini la kichunguzi.

Kwa hiyo, wakati waumini wakiendelea kuzishikilia nyumba hizo kwa uhalalisho wa wasia bila nyaraka nyingine za kisheria, tayari Pius na Steven ndio waliotambulika kama wamiliki halali wenye hati miliki.

Umiliki huo ukawapa nguvu kuvitaarifu Vyombo vya Usalama ambavyo vilichukua hatua dhidi ya waumini waliokuwa kwenye nyumba hizo.

Hatua hizo zilikuwa ni pamoja na kuwaweka mahabusu na kuwafungulia kesi ya ukaliaji nyumba za watu bila ruhusa yao (tracepass).

Hali hiyo iliendelea kuzusha tafrani kati ya waumini na serikali ikidaiwa serikali inawapendelea Wakristo waliopora mali za wakfu wa Waislamu.

Sanjari na hayo, Masjid Mwinyi haikukaa kimya ilijitajidi kufungua kesi kadhaa baadhi ikiwa dhidi ya Pius Kipengele na Steven Mwamkoa ambazo hata hivyo zilionekana kukosa mashiko kwa kuwa wao walionekana kama wanunuzi tu.

Ndipo mwaka 2000, tulipoifungua kesi na 196/2000 Mahakama Kuu dhidi ya Daniel Zakaria, ambayo ilikuwa mbele ya Jaji Madina Muro (marehemu).

Mawakili tuliowaweka ni pamoja na Zainab Muruke (sasa Jaji) na Issa Maige (naye pia sasa ni Jaji).

Hukumu ya kesi hiyo ilitengua usimamizi wa Daniel Zakaria aliyopewa na Mahakama ya Kisutu katika shauri Na. 73/91 na kuelekeza shauri hilo lisikilizwe upya kwa kuhusisha waomba mirathi wote ili maamuzi ya haki yapatikane.

Katika kipindi chote hicho Masjid Mwinyi ilikuwa ingali na usimamizi wa mirathi katika shauri Na. 89/91 ambalo kiuhakika halikuwa limetenguliwa kwa taratibu za kimahakama bali kukwamishwa na maelekezo ya Hakimu Mama Natalia Kimaro kwa Mkurugenzi wa Manispaa.

Hali iliendelea kuwa tete baina ya waumini na Daniel. Zakaria akishirkiana na "wanunuzi" wake Pius Kipengele na Steven Mwamkoa kiasi kwamba majina hayo yalikuwa yameendelea kuwa midomoni mwa waumini wa dini ya Kiislamu nchi nzima kuwa ni waporaji wa mali za wakfu.

Utekelezwaji wa Maelekezo ya Jaji Muro hukumu kesi Na. 196/2000

Kilipita kipindi kirefu bila maelekezo ya hukumu ya Jaji Madina Muro kutekelezwa.

Hiyo ilisababishwa na kile ninachoweza kutuhumu kama "mizengwe" kadhaa ikiwa ni pamoja na faili husika na 73/91 kutoonekana katika hifadhi ya mafaili ya Mahakama ya Kisutu, hali iliyoendelea kusababisha mvutano wa waumini na akina Pius Kipengele wakati huo huo vurugu katika nyumba za Mirathi ya Hajat Aziza na misikitini.

Jitihada za Wakili Msomi Profesa Abdallah Safari

Alikuwa ni Wakili Profesa Safari aliyefanikisha kupatikana kwa Faili Na. 73/91 Mahakama ya Kisutu kwa kumtumia aliyekuwa muhudumu wa mafaili wa mahakama hiyo (sasa marehemu).

Ambaye alifanya kazi ya zoada kulitafuta hadi kulibaini likiwa limefichikana "store" ya mafaili.

Kupatikana kwa faili hilo ndipo shauri husika likaanza kusikilizwa mwaka 2010.

Kusikilizwa kwa shauri hili kulianza na kutafuta uhusika (locus stand) wa Abdallah Rashid aliyesimama kama msimamizi akiwakilisha Masjid Mwinyi, katika kesi iliyofunguliwa na Daniel Zakari aliyedai na kufanikisha usimamizi wa mali za Hajat Aziza.

Wakati huo Daniel Zakari alikuwa hai alihudhuria Mahakamani akiwakilishwa pia na wakili ambaye ilikuja kufahamika kuwa alikuwa akilipwa na Pius Kipengele.

Shauri hili awali lilisikilizwa na Hakimu Mama Revocatus alipohama likaendelea kusikilizwa na Hakimu Mama Nkya, alipoteuliwa kuwa Msajili Mahakama Kuu, usikilizwaji ukarndelezwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Mheshimiwa Katemana.

Baada ya "Locus stand" kupatikana kwa Abdallah Rashid.

Ikafuata hatua ya "extension of time" kabla ya kusikilizwa shauri la msingi ambalo ni Mirathi.

Wakati shauri likiwa katika hatua hii, Daniel Zakari alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Na taarifa zake hazikupatikana mara moja, cha ajabu wakili wake aliendelea kuhudhuria mahakamani bila kukosa ikiashiria mteja halisi hakuwa Daniel Zakaria, bali wale wanunuzi, Pius Kipengele na Steven Mwamkoa, na hasa Pius Kipengele.

Hata hivyo katika moja ya vikao vya Mahakama, Hakimu Katemana alimuuliza wakili juu ya aliko mteja wake swali lililoonesha kumpa taharuki wakili na kukiri kuwa alikuwa hajui.

Hakimu Katemana alipomuuliza tena nani alikuwa akimlipa kuwakilisha kesi hiyo kama hajui aliko mteja wake, wakili alionyesha kutatizika zaidi.

Kwa ajili hiyo Hakimu Katemana alimuamuru Wakili amjulishe mteja wake ahudhurie kikao kilichofuatia.

Hata hivyo, katika kikao kilichofuatia wakili huyo alilazimika kuieleza mahakama kuwa mteja wake alikuwa amefariki dunia masiku kadhaa.

Ilikuja kufahamika Bwana Daniel Zakaria alifariki dunia Hospitali ya Muhimbili na alizikwa na Manispaa kwa kuwa ilidaiwa hakujitokeza ndugu yoyote kuchukua mwili wake.

Kesi kufa (aberterd)

Baada ya taarifa ya kifo cha Daniel Zakaria, Hakimu Katemana alitoa muda kwa wahusika ambao ni ndugu wa marehemu kujitokeza kuendelea na kesi.

Hata hivyo muda ulipita hakujitokeza ndugu yeyote, shauri hilo likawa "aberted" na Hakimu Katemana kuamuru yeyote aliye na "interest" na Mali za Hajat Aziza afungue Mirathi.

Masjid Mwinyi tulifungua shauri la Mirathi Na. 40 Mahakama ya Kariakoo na kufanikiwa kumuweka Bwana Seif Kiambwe, mmoja wa wadhamini, kuwa msimamizi kwa kuwa Abdallah Rashid naye alikuwa mgonjwa na muda mfupi baadae alifariki dunia.

Tangazo la Mirathi tulilitoa katika gazeti Uhuru.

Na hakujitokeza mtu kupinga.

Mahakama ya Kariakoo ikatoa Usimamizi kwa Seif Kiambwe akiwakilisha Masjid Mwinyi.

Kujitokeza kwa mara nyingine Pius Kipengele na Steven Mwamkoa

Mara baada ya kupata usimamizi, Mahakama ya Kariakoo iliandika barua Manispaa Ilala na Wizara ya Ardhi kutambulisha usimamizi wa Masjid Mwinyi kwa mali za wakfu za Hajat Aziza Omar na kuzielekeza mamlaka hizo ziweke sawa nyaraka na kumbukumbu kwa mujibu wa sheria za umiliki, wakati huo huo kuwaamuru wanaodai umiliki kuondoka, ndipo walipojitokeza Pius Kipengele la Steven Mwamkoa wakati huo akiwa ameshauza nyumba Na. 17/56 Mtanzania mwenye asili ya Kihindi (Kiasia), Moez Jaffer Morbiwala.

Kwa hiyo Pius Kipengele, Steven Mwamkoa na Morbiwalla nyuma yake, walifungua kesi ya kupinga amri hiyo ya Mahakama ya Mwanzo katika Mahakama ya Wilaya mbele ya Mahakimu Mama Kaluyenda na Mama Minde.

Katika Hali iliyotatanisha na iliyoonesha kukanganya, wakati Hakimu akisoma hukumu, Wakili Musa Godwin wakati hukumu ikosomwa aliinuka kutaka kupinga hali iliyomshangaza wakili wetu Mheshimiwa Abdulafattah akiwakilisha Chamber ya Wakili Maige wakati huo.

Wakili Minde alimtuliza Wakili huyo, na kuendelea kusoma hukumu hiyo ambayo mwisho ilitoa ushindi kwa wateja wakili wa walalamikaji Bwana Steven Meamkoa akishirikiana na Moez Morbiwallah.

Hali iliyosababishwa, wakili wa Masjid Mwinyi Mh. Maige kukata rufaa Mahakama Kuu.

Wakati Masjid Mwinyi inaendelea na taratibu na taratibu za sheria, Steven Mwamkoa na Moez Morbiwala kwa kumtumia mmoja wa maafisa ardhi Ofisi ya Msajili Hati walifanikisha kufanya "transfer'' ya umiliki kutoka kwa Steven Mwamkoa kwenda Moez Morbaiwalla.

Hii ilikuwa kwenye nyumba Na. 17/56.

Ulaghai huu wa kisheria ulifanyika wakati faili zote mbili za nyumba 32/77 na 17/56 zikiwa na "Caveat."

Utovu huu wa kisheria ulifanyika wakati Msajili Mama Subira Sinda akiwa likizo.

Aidha Nyumba na 32/77 hati iliendelea kusomeka jina la Pius Kipengele kabla ya jitihada za kiutawala kutekeleza amri ya Mahakama ya Mwanzo kuhamisha umiliki kwenda Masjid Mwinyi, hazijakamilika.

Kwa sasa nyumba hii iko chini ya umiliki wa Masjid Mwinyi kabla ya Kipengele kufungua shauri Mahakama Kuu mbele ya Jaji Luvanda na Jaji Mgonya ambao wameamuru jina la Masjid Mwinyi lifutwe na kurejeshwa tena Kwa kuwa "taratibu za kisheria" zilikosewa.

Hukumu imeasababisha Masjid Mwinyi kwa kuzingatia rwajibu (role)ya Mahakama ya Rufaa katika utoaji haki, kuomba Mahakama ya hiyo chini ya Jaji Mkuu kufanya mapitio ya kesi nzima iliyohusisha kesi kadhaa ndani yake, ili haki ifike kunakostahiki.

Jitihada za Masjid Mwinyi kwa ushauri wa vyombo vya Ulinzi na Usalama

Wakati hali ikiendelea kutoeleweka, waumini misikitini wakiendelea kwa dua na kujihamasisha kufanya maandamano kwenda Ardhi kulalamika kwa nini wizara hiyo chini ya Waziri Profesa Mama Tibaijuka wakati ule imefanikisha mali za wakfu kuporwa na watu, tena wasio waumini wa dini hiyo, maafisa wa polisi hasa aliyekuwa OCD Msimbazi na maafisa wa Idara ya Usalama walishauri Masjid Mwinyi iendelee kufuata taratibu za kiutawala na kisheria kupata haki hizo ili kusaidia kutunza amani ikiwa ni pamoja na kuwatuliza waumini.

Masjid Mwinyi ilitekeleza kwa busara maelekezo hayo kwa kushirikiana na moja ya magazeri ya Kiislamu (Alhuda) kusaidia jukumu hilo la kutunza amani kuwazuia waumini kutumia nguvu zao kuhami mali hizo.

Masjid Mwinyi kwa kushirikiana na gazeti hilo walifanikiwa kuwatuliza Waislamu huku ikiendelea kusimamia suala hilo kwa njia za amani kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Hata hivyo hatua hii imekuwa na changamoto kubwa ya chuki, kuchafuliwa na lawama kubwa miongoni mwa Waislamu dhidi yangu na Masjid Mwinyi na kwa chombo husika cha habari kwa madai kuwa hatua zetu zinasaidia waporaji kupora Mali za Waislamu na kwamba tumehongwa na matapeli.

Na hasa wanapoona nyumba ya ghorofa sita ikiwa imejengwa na Moez Morbiwalla kiwanja cha wakfu na. 17/56 akiendelea na biashara zake bila hofu.

Nimeandika waraka huu mrefu kueleza ukweli juu ya Mali za Wakfu na suala la usimamizi wa Mirathi ya Hajjat Aziza Omar.

Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa nimekuwa mkweli na nimesimamia suala hili wakati wote yeye akinishuhudia na nafsi yangu ikishuhudia hivyo.

Najielekeza kwa MOLA wangu kuwa nimetimiza Amana.

Allah nishuhudie.

Nimebeba jukumu hili nikiwa na umri wa miaka 46 mwaka 1991 sasa nina miaka 78 ambalo limeendelea kutatiza na kuwa kizungumkuti katika mahakama zetu kwa takribani miaka 32 sasa.

Hivi sasa shauri hili liko Mahakama ya Rufani.

Ni Maombi yangu kuwa suala hili litapatiwa ufumbuzi wenye haki Kwa mujibu wa sheria.

Naamini ni wajibu wa Mahakama ya Rufaa kuichimba na kuitafuta haki kwa jicho kali zaidi ili iweze kufika kule inakotakiwa kwa sababu wajanja na watu wasio waaadilifu wamekuwa wakitumia taratibu na kanuni za kimahakama kupoka haki za watu katika jamii hali iliyosababisha dhuluma, chuki na wakati mwingine vurugu katika jamii.

Namuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu, hekima na busara na uadifilifu Rais Wetu Mpendwa Mama Samia na Serikali, Majaji, Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu, Mawakili wote na Mahakimu wote Mahakama zote nchini

Sheikh Abeid Maulid Abeid

Masjid Mwinyi
0713 326 695
 
Mzee baba unazungumzia uvccm viongozi wote wawe Waislamu... Huo sio mfumo Makka?
 
Wahamiaji kutoka mikoani, kesi hii ina mafunzo mengi kuhusu umilikaji mali huku ndugu zako wa karibu wanaishi kijijini na wala mjini hawapajui.
 
Tangazo la Mirathi alilitoa kwenye "Government Gazette" ambalo halisomwi mitaani.
Hapo ndiyo chanzo cha haya yote Sasa hivi.
Nani alipewa cheti cha kifo?
Kutokusoma Government Gazette ndiyo kumemponza Trustee wa Masjid Mwinyi.
Ila hizo Mali zitarudi tu, Ili mradi hizi habari na nyaraka zipite kwa vizazi vijavyo.
 
Daaah huu mkasa umenihudhunisha sana, naomba kujua hatma ya waumini ambao walifunguliwa kesi ya kukalia Mali isiyo yao kinguvu!?
 
Mwishowe wote tutakufa na kuacha hizo mali za urithi.
Kesi miaka 32 sasa mmeshindwa kujenga msikiti kwingine clean muachane na huo mkorogo wa urithi.
Badala yake mnaingiza Udini
 
Babukijana,
Waislam wanajenga misikiti mipya nchi nzima kila siku.
Suala lililopo hapa ni wizi na dhulma.

Waislam wameamrishwa na Mola wao kutokudhulumu na pia kutokubali kudhulumiwa.

Hili ndilo lililopo.
Kama kuna udini katika kesi hii basi haukutoka kwa Waislam.
 
Ujanja ujanja tu, kwanini hao wapigania wakfu wasitoe viwanja vyao. Leo hii viwanja vingapi wamejimilikisha wao, hizo ndo sababu matapeli wa dini nyingine kuingilia kati na wao kupora hvyo viwanja. Hapo kinachopiganiwa sio uislam ni mali ambazo hazieleweki kinaga ubaga, Wallah naapa hata hao sijui wanaotaka kuzitetea nyumba hizo wanalengo Moja kama LA huyo bwana Daniel,
 
Daaah huu mkasa umenihudhunisha sana, naomba kujua hatma ya waumini ambao walifunguliwa kesi ya kukalia Mali isiyo yao kinguvu!?
hii ilishapitaga nakumbuka ilikuwa mwishoni mwa miaka 90s kama sikosei sin hakika
ila nakumbuka kipindi masjid mtambani inajengwa miaka 90 mwishoni
nondo zote zilikuwa zinasukwa pale KKOO MANYEMA ilikuwa umaliziaji tu
ilikuwa hatari IJUMAA mpk tukawa tunakatazwa na WAZAZI kwenda kuswali pale MTAMBANI mana muda wote kinanuka MABOMU na FFU
Edhi hizo ITIKADI ITIKADI kweli sio masihara
sio sasa BAKWATA pale imejaa MAMLUKI
hakuna zile ITIKADI
na walivyoubadirisha UONGOZI masjid IDRISA Itikadi ikapotea kabisa
sasa hivi hiyo MISIKITI haina ile itikadi tena iliyokuwa na MIONGOZO THABITI ya KIDINI
 
Ujanja ujanja tu, kwanini hao wapigania wakfu wasitoe viwanja vyao. Leo hii viwanja vingapi wamejimilikisha wao, hizo ndo sababu matapeli wa dini nyingine kuingilia kati na wao kupora hvyo viwanja. Hapo kinachopiganiwa sio uislam ni mali ambazo hazieleweki kinaga ubaga, Wallah naapa hata hao sijui wanaotaka kuzitetea nyumba hizo wanalengo Moja kama LA huyo bwana Daniel,
Zamani wenye Nyumba nyingi kuanzia Kariakoo,Ilala hadi Magomeni na kinondoni wengi walikua Wanawake na hawakua na Mume wala Watoto, ndiyo maana unaona Mali zao kila Mtu anagombania baada ya wao kufa na kutokua na mrithi!!
 
umaskini tu na kupenda dezo navyoona hao msikiti hawakupewa haki kwenye wosia si ajabu walishinikiza ajuza kuandika....huyo aliyekuja kudai alistahili kwa kuwa alikuwa karibu na marehemu....sasa ile njaa na upenda devo ndio vinafanya waendelee kudai vya wafu...
 
Hiyo stori akili yangu inakataa hoja ya huyo mama kutoka singida awe na nyumba kazaa kariakoo. Na bado ndugu zake wasijitokeze kuishi nae.

Watu wasingida wanapenda sana kuishi pamoja hasa ndugu yao akiwa na nyumba mjini.

Pili naona kuna ujanja ujanja.. huo wasia wa nyumba zake zote zipewe msikiti akili yangu inakataa.

Naona hapo marehemu kafa .. kila upande umejipa umuhimu wa kumiliki mali zake kiujanja ujanja. Wosia feki imetengenezwa na upande mwingine na wengine nao hati feki wametengeza,, Upande ulioona umezidiwa ujanja ndio unaplay victim role.

Pia swala la kuibiwa hati zote. Yaani mtu uibiwe hati za nyumba yako upuuzie tu wala usiende ardhi wakupe copy zake.

Maana rekodi za hati zipo wizara ya ardhi
 
hii ilishapitaga nakumbuka ilikuwa mwishoni mwa miaka 90s kama sikosei sin hakika
ila nakumbuka kipindi masjid mtambani inajengwa miaka 90 mwishoni
nondo zote zilikuwa zinasukwa pale KKOO MANYEMA ilikuwa umaliziaji tu
ilikuwa hatari IJUMAA mpk tukawa tunakatazwa na WAZAZI kwenda kuswali pale MTAMBANI mana muda wote kinanuka MABOMU na FFU
Edhi hizo ITIKADI ITIKADI kweli sio masihara
sio sasa BAKWATA pale imejaa MAMLUKI
hakuna zile ITIKADI
na walivyoubadirisha UONGOZI masjid IDRISA Itikadi ikapotea kabisa
sasa hivi hiyo MISIKITI haina ile itikadi tena iliyokuwa na MIONGOZO THABITI ya KIDINI

Internet na utandawazi ndio sababu.. dini zote haziaminiki siku hizi kama zamani
 
hii ilishapitaga nakumbuka ilikuwa mwishoni mwa miaka 90s kama sikosei sin hakika
ila nakumbuka kipindi masjid mtambani inajengwa miaka 90 mwishoni
nondo zote zilikuwa zinasukwa pale KKOO MANYEMA ilikuwa umaliziaji tu
ilikuwa hatari IJUMAA mpk tukawa tunakatazwa na WAZAZI kwenda kuswali pale MTAMBANI mana muda wote kinanuka MABOMU na FFU
Edhi hizo ITIKADI ITIKADI kweli sio masihara
sio sasa BAKWATA pale imejaa MAMLUKI
hakuna zile ITIKADI
na walivyoubadirisha UONGOZI masjid IDRISA Itikadi ikapotea kabisa
sasa hivi hiyo MISIKITI haina ile itikadi tena iliyokuwa na MIONGOZO THABITI ya KIDINI
Hv hlo ghorofa la Muhindi ni lipi🤔🤔
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Jaji Mkuu,
Majaji,
Mawakili na Mahakimu wote

Ukweli kuhusu umiliki wa viwanja 32/77 Somali Street na 17/56 Mtaa Mchikichi Kariakoo Dar es Salaam.

Mimi Abeid Maulid Abeid umri wangu hivi sasa ni miaka yangu 78.

Ni Imamu wa Masjid Mwinyi uliopo Mtaa wa Moshi, Ilala Boma toka mwaka 1990 lakini pia nilikuwa Imamu na Khaatibu wa Sala ya Ijumaa Msikiti Manyema, na pia Mdhamini.

Naomba maelezo haya yavifikie Vyombo vya Sheria, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mamlaka za Nchi.

Awali nilikuwa nikiishi mtaa wa Tabora, Ilala, jirani na Masjid Mwinyi, hivi sasa naishi Mbagala Charambe.

Wakati wa ujana wangu miaka ya 1960 mwanzoni hadi 1970 mwanzoni nilipata kuwa mchezaji wa timu ya Yanga na Timu ya Taifa (Taifa Stars).

Nikiwa Mchezaji wa mchezo wa mpira, pia nilikuwa mfanyakazi serikalini, Wizara ya Kilimo na Mifugo nikiwa Afisa Mifugo.

Marehemu Hajjat Aziza Omar

Hajat Aziza Omar na ndugu yake Asha Omar ni ndugu waliokuwa wakiishi Mitaa ya Somali na Mchikichi Kariakoo Dar es Salaam.

Katika uhai wao walifanikiwa kumiliki nyumba.

Aziza Omar akimiliki nyumba Na. 32/77 Mtaa wa Somali na nyumba Na. 20 Mtaa wa Moshi Ilala Boma (hivi sasa Msikiti Miwnyi).

Lakini pia alikuwa akimiliki nyumba nyingine mtaa wa Congo ambayo kwa sasa inamilikiwa na Pius Kipengele.

Hii aliipata kwa manunuzi yenye shubha.

Aidha nduguye (dada yake) Asha Omar akimiliki nyumba Na. 17/56.

Mabibi hawa walikuwa na asili ya Singida, walikuwa waumini wa dini ya Kiislamu na hawakuwa na ndugu wengine wa nasaba kipindi hicho cha umri wao wakiwa Dar-es-Salaam.

Baada ya kufariki dunia Asha, mdogo wake Aziza Omar alirithi nyumba Na. 17/56 Mtaa wa Mchikichi.

Mwaka 1990 Aziza alifanikiwa kwenda Hija, ndio asili ya kuitwa Hajat, na aliporudi aliigeuza nyumba yake iliyopo mtaa wa Moshi Ilala Boma kuwa msikiti na katika kuufungua msikiti huo alimuomba aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati huo, Ali Hassan Mwinyi kuwa Mgeni Rasmi.

Na aliupa msikiti huo jina la la rais huyo.

Ndiyo asili ya kuitwa Msikiti au Masjid Mwinyi.

Aidha aliniteua mimi Abeid Maulid Abeid kuwa Imamu wa swala za kawaida, kwa kuwa hapakuwa pakiswaliwa swala ya Ijumaa.

Daniel Zakaria na Pius Kipengele

Daniel Zakaria alikuwa mpangaji wa Hajat Aziza Omar nyumba Na 32/77 mtaa wa Somali.

Pius Kipengele akiwa mfanyabishara maeneo ya Kariakoo alikuwa mpangaji pia wa Hajat Aziza Omar nyumba ya mtaa wa Moshi Ilala Boma kabla haijageuzwa kuwa msikiti.

Wakati huo akiwa na wapangaji wenziwe, miongoni mwao alikuwa Afisa Ardhi Manispaa Ilala Bwana Komba ambaye baada ya kustaafu alirejea kwao Songea (0756214978).

Daniel Zakaria, sasa marehemu, hakuwa na shughuli maalum.

Alikuwa akitumwa na Hajat Aziza kumtekelezea baadhi ya shughuli zake za nje, kama ulipaji umeme, maji na nyingine ndogo.

Daniel Zakaria si yeye tu aliyekuwa akitumwa shughuli hizo, bali alikuwepo Abdallah Rashid (marehemu sasa) ambaye ni mmoja wa watu aliowataja katika kiapo (wasia) chake.

Aidha Pius Kipengele kama mfanyabishara wakati huo hadi sasa alikuwa akimtumia kwa shughuli zake lakini pia akimfahamu kama mtu aliyekuwa akiishi nyumba ya Hajjat mtaa wa Somali.

Muungano wao na kile kilichokuja kufanyika baada ya kifo cha Hajjat Aziza, moja ya vimelea vyake ni hiki.

Kiapo na Kifo na cha Hajjat Aziza Omar

Kabla ya kufariki kwake, marhumat Aziza Omar aliandika Wasia (Kiapo) ambao upo ukiwa umesajiliwa Mahakama ya Mwanzo Mkwajuni (Kariakoo) mbele aliyekuwa Hakimu wa Mahakama hiyo, Mh. Jamila Ditopile.

Hila za Daniel(nyuma ya pazia akiwa Kipengele)

Kabla ya kufariki dunia, Hajat Aziza, aliishi maisha ya upweke mtaa wa Somali akihudumiwa kwa karibu na Abdallah Rashid.

Katika moja ya changamoto zilizomkuta bibi huyu ni pamoja kutendewa matendo ya udhalilishaji kutoka kwa Daniel Zakaria lakini kubwa zaidi kuibiwa hati za nyumba na nyaraka nyingine.

Mtuhumiwa wa wizi huu alikuwa Daniel Zakaria ambaye baada kutenda uhalifu huu alikimbilia kwao ambako alikaa hadi alipopata taarifa za kifo cha Hajat.

Kuripotiwa polisi Daniel Zakari

Kwa tukio la wizi, Hajat Aziza alitoa taarifa polisi kituo cha Msimbazi na kupata Report Book (RB) ambayo nakala yake ipo.

Daniel Zakaria hakuweza kupatikana hadi Hajat Aziza anafariki dunia mwezi June 1991.

Kwa dokezo tulizodokezwa, mipango ya wizi wa nyaraka za nyumba, na kurejea kimya kimya kwa Daniel Zakaria hadi kufungua Mirathi Mahakama ya Kisutu ilisukwa na Pius Kipengele.

,Mirathi ya Hajat Aziza

Wasia (kiapo) umetaja majina kadhaa likiwemo la Mwinshehe Mgumba na Abdallah Rashid kwamba, mara baada ya kifo chake ndiyo wawe wasimamizi wa Mirathi wakati huo huo aliwakana baadhi ya watu waliojinasibisha naye.

Wasia umeelekeza Nyumba zake mbili 32/77 Somali Street na 17/56 Mchikichi Street Kariakoo, zitumike kama rasimali (Wakfu) kuhudumia Msikiti Mwinyi.

Kwa ajili hiyo, mara baada ya kifo chake Mwinshehe Mgumba kwa niaba ya Masjid Mwnyi alifungua Mirathi Mahakama ya Kariakoo shauri Na 89/91 kwa niaba ya Masjid Mwinyi kuomba usimamizi kisheria.

Hii ikiwa ni mapema zaidi na hapakuwepo shauri lingine kama hilo.

Hata hivyo mirathi hii ilichelewa kutolewa hadi January 1992.

Hila za Daniel Zakaria na Pius Kipengele

Mara baada ya kusikia taarifa za kifo cha Hajjat Aziza, Daniel Zakari alijiitokeza Mahakama ya Kisutu kudai usimamizi wa mirathi akiwa na nyaraka zote za marehemu (alizoziiba).

Alifungua shauri hilo Na. 73/91 wakati tayari Masjid Mwinyi ikiwa imeshafungua Mirathi inayohusu Mali za Marehemu Hajat Aziza.

Tangazo la Mirathi alilitoa kwenye "Government Gazette" ambalo halisomwi mitaani.

Ndani ya siku chache zisizotimia 30 kwa mujibu wa sheria Mahakama ya Kisutu ikampa usimamizi.

Mara baada ya kupata usimamizi huo akawasilisha amri ya Mahakama Manispaa Ilala kwa ajili ya Umiliki.

Wakati anafanya haya, Masjid Mwinyi haikuwa na taarifa zozote.

Mwezi January 1992 Masjid Mwinyi kupitia mirathi aliyofungua Mwinshehe Mahakama ya Kariakoo ikapewa Usimamizi wa mirathi.

Ilipoanza kukusanya Mali za marehemu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nyaraka Manispaa Ilala, mirathi inayohusu Mali za Hajat Aziza iliyofunguliwa na Masjid Mwinyi ikagongana na mirathi iliyofunguliwa na Daniel Zakaria.

Kwa mgongano huu aliyekuwa Afisa Ardhi aliyeshughulikia suala hilo Bwana Komba pamoja na kuwajulisha Masjid Mwinyi juu ya utapeli wa Daniel Zakaria wakati huo akimshuhudia Kipengele akifika naye pale Manispaa, alimjulisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa Mama Kessy.

Wote wawili walijiuliza nini kifanyike?

Mkurugenzi Mama Kessy aliomba muongozo wa Mahakama Kisutu.

Aliyekuwa Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Kisutu wakati huo Mama Natalia Kimaro akaelekeza usimamizi uwe wa aliyetangulia kuwa "granted" na ule wa mahakama ya juu ya nyingine ambayo kwa wakati Ile ilikuwa Kisutu.

Hata hivyo, kwa kuujua ukweli wa suala hilo na hila zilizokuwa zikiendelea baina ya Daniel Zakaria na Pius Kipengele, Mkurugenzi kwa ushauri wa Afisa Ardhi Mr. Komba, hakutekeleza maelekezo hayo hadi anahama Manispaa hiyo.

Kuhama kwa mkurugenzi huyo kulitoa fursa kwa Daniel Zakaria na mshirika wake, Kipengele kuendelea hatua za kufanikisha mchakato wa "usimamizi" kupitia Manispaa.

Daniel Zakari anakuwa Mmiliki toka Msimamizi, Pius Kipengele na Steven Mwamkoa wanakuwa wanunuzi.

Baada ya Daniel Zakari "kujimilikisha" kwa hila, ghushi na udanganyifu nyumba Na. 32/77, 17/56 na hata Msikiti Mwinyi (nyaraka zilizopo Manispaa ambazo zimekwisha muda zilisomeka nyumba ya Mtaa wa Moshi ambayo ni Masjid Mwinyi ni Mali ya Daniel Zakaria, na akiwa hai alishadai kuwa Msikiti huo ni mali yake), alimshirikisha pia Mchungaji Mtikila katika kudai huko ambako nusura kusababishe vurugu ya kidini kati ya Wakristo na Waislamu.

Yaliyojiri baada ya Daniel Zakaria kujimilikisha nyumba Na. 32/77 na 17/56

Pius Kipengele na mfanyabishara mwenziwe Steven wanakuwa wanunuzi.

Daniel Zakaria haraka haraka anawauzia mabwana hao.

Hii ikiwa ni mwaka 1993.

Pius "ananunua" nyumba Na. 32/77 anaigeuza nyumba hiyo pamoja na upangaji mwingine, kuwa Bar.

Steven Mwamkoa alinunua nyumba 17/56 iliyo mtaa wa Mchikichi jirani na Msikiti Mtoro.

Kufuatia hali hiyo na lawama kubwa kutoka kwa kuzingatia wasia wa marehemu na kwamba wasia ni jambo zito katika Uislamu na kwa shinikizo kutoka kwa waumini, pamoja na kujaribu kutafuta haki hiyo kwa njia za sheria, Mimi nikiwa Imamu na Khaatibu wa Swala ya Ijumaa, nilisimama katika Mimbar Msikiti wa Manyema siku ya Ijumaa nikaeleza mkasa huo kwa mamia ya waumini waaoswali hapo.

Hatua hiyo iliibua hasira na hamasa zilizowasukuma Waislamu kuvamia maeneo hayo.

Walianza nyumba ya Mchikichi wakaidhibiti kwa nguvu bila kufuata sheria kisha wakavamia nyumba ya Somali hali iliyozusha tafrani kubwa iliyovisukuma vyombo vya Ulinzi na Usalama kufuatilia kwa karibu.

Pius Kipengele na Steven Mwamkoa waenda kimya kimya kupata hati Wizara Ardhi

Wakati hayo yakijiri huku mtaani, Pius Kipengele na Steven Mwamkoa walipiga hatua kadhaa kimya kimya kujimilikisha kisheria Wizara ya Ardhi ambako walifanikiwa kupata hati.

Mafaili yaliyopo kwa Msajili naamini yanaonyesha umaalum wa usajili na umiliki wa nyumba hizi.

Naamini yanaweza kutoa picha fulani kwa jicho makini la kichunguzi.

Kwa hiyo, wakati waumini wakiendelea kuzishikilia nyumba hizo kwa uhalalisho wa wasia bila nyaraka nyingine za kisheria, tayari Pius na Steven ndio waliotambulika kama wamiliki halali wenye hati miliki.

Umiliki huo ukawapa nguvu kuvitaarifu Vyombo vya Usalama ambavyo vilichukua hatua dhidi ya waumini waliokuwa kwenye nyumba hizo.

Hatua hizo zilikuwa ni pamoja na kuwaweka mahabusu na kuwafungulia kesi ya ukaliaji nyumba za watu bila ruhusa yao (tracepass).

Hali hiyo iliendelea kuzusha tafrani kati ya waumini na serikali ikidaiwa serikali inawapendelea Wakristo waliopora mali za wakfu wa Waislamu.

Sanjari na hayo, Masjid Mwinyi haikukaa kimya ilijitajidi kufungua kesi kadhaa baadhi ikiwa dhidi ya Pius Kipengele na Steven Mwamkoa ambazo hata hivyo zilionekana kukosa mashiko kwa kuwa wao walionekana kama wanunuzi tu.

Ndipo mwaka 2000, tulipoifungua kesi na 196/2000 Mahakama Kuu dhidi ya Daniel Zakaria, ambayo ilikuwa mbele ya Jaji Madina Muro (marehemu).

Mawakili tuliowaweka ni pamoja na Zainab Muruke (sasa Jaji) na Issa Maige (naye pia sasa ni Jaji).

Hukumu ya kesi hiyo ilitengua usimamizi wa Daniel Zakaria aliyopewa na Mahakama ya Kisutu katika shauri Na. 73/91 na kuelekeza shauri hilo lisikilizwe upya kwa kuhusisha waomba mirathi wote ili maamuzi ya haki yapatikane.

Katika kipindi chote hicho Masjid Mwinyi ilikuwa ingali na usimamizi wa mirathi katika shauri Na. 89/91 ambalo kiuhakika halikuwa limetenguliwa kwa taratibu za kimahakama bali kukwamishwa na maelekezo ya Hakimu Mama Natalia Kimaro kwa Mkurugenzi wa Manispaa.

Hali iliendelea kuwa tete baina ya waumini na Daniel. Zakaria akishirkiana na "wanunuzi" wake Pius Kipengele na Steven Mwamkoa kiasi kwamba majina hayo yalikuwa yameendelea kuwa midomoni mwa waumini wa dini ya Kiislamu nchi nzima kuwa ni waporaji wa mali za wakfu.

Utekelezwaji wa Maelekezo ya Jaji Muro hukumu kesi Na. 196/2000

Kilipita kipindi kirefu bila maelekezo ya hukumu ya Jaji Madina Muro kutekelezwa.

Hiyo ilisababishwa na kile ninachoweza kutuhumu kama "mizengwe" kadhaa ikiwa ni pamoja na faili husika na 73/91 kutoonekana katika hifadhi ya mafaili ya Mahakama ya Kisutu, hali iliyoendelea kusababisha mvutano wa waumini na akina Pius Kipengele wakati huo huo vurugu katika nyumba za Mirathi ya Hajat Aziza na misikitini.

Jitihada za Wakili Msomi Profesa Abdallah Safari

Alikuwa ni Wakili Profesa Safari aliyefanikisha kupatikana kwa Faili Na. 73/91 Mahakama ya Kisutu kwa kumtumia aliyekuwa muhudumu wa mafaili wa mahakama hiyo (sasa marehemu).

Ambaye alifanya kazi ya zoada kulitafuta hadi kulibaini likiwa limefichikana "store" ya mafaili.

Kupatikana kwa faili hilo ndipo shauri husika likaanza kusikilizwa mwaka 2010.

Kusikilizwa kwa shauri hili kulianza na kutafuta uhusika (locus stand) wa Abdallah Rashid aliyesimama kama msimamizi akiwakilisha Masjid Mwinyi, katika kesi iliyofunguliwa na Daniel Zakari aliyedai na kufanikisha usimamizi wa mali za Hajat Aziza.

Wakati huo Daniel Zakari alikuwa hai alihudhuria Mahakamani akiwakilishwa pia na wakili ambaye ilikuja kufahamika kuwa alikuwa akilipwa na Pius Kipengele.

Shauri hili awali lilisikilizwa na Hakimu Mama Revocatus alipohama likaendelea kusikilizwa na Hakimu Mama Nkya, alipoteuliwa kuwa Msajili Mahakama Kuu, usikilizwaji ukarndelezwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Mheshimiwa Katemana.

Baada ya "Locus stand" kupatikana kwa Abdallah Rashid.

Ikafuata hatua ya "extension of time" kabla ya kusikilizwa shauri la msingi ambalo ni Mirathi.

Wakati shauri likiwa katika hatua hii, Daniel Zakari alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Na taarifa zake hazikupatikana mara moja, cha ajabu wakili wake aliendelea kuhudhuria mahakamani bila kukosa ikiashiria mteja halisi hakuwa Daniel Zakaria, bali wale wanunuzi, Pius Kipengele na Steven Mwamkoa, na hasa Pius Kipengele.

Hata hivyo katika moja ya vikao vya Mahakama, Hakimu Katemana alimuuliza wakili juu ya aliko mteja wake swali lililoonesha kumpa taharuki wakili na kukiri kuwa alikuwa hajui.

Hakimu Katemana alipomuuliza tena nani alikuwa akimlipa kuwakilisha kesi hiyo kama hajui aliko mteja wake, wakili alionyesha kutatizika zaidi.

Kwa ajili hiyo Hakimu Katemana alimuamuru Wakili amjulishe mteja wake ahudhurie kikao kilichofuatia.

Hata hivyo, katika kikao kilichofuatia wakili huyo alilazimika kuieleza mahakama kuwa mteja wake alikuwa amefariki dunia masiku kadhaa.

Ilikuja kufahamika Bwana Daniel Zakaria alifariki dunia Hospitali ya Muhimbili na alizikwa na Manispaa kwa kuwa ilidaiwa hakujitokeza ndugu yoyote kuchukua mwili wake.

Kesi kufa (aberterd)

Baada ya taarifa ya kifo cha Daniel Zakaria, Hakimu Katemana alitoa muda kwa wahusika ambao ni ndugu wa marehemu kujitokeza kuendelea na kesi.

Hata hivyo muda ulipita hakujitokeza ndugu yeyote, shauri hilo likawa "aberted" na Hakimu Katemana kuamuru yeyote aliye na "interest" na Mali za Hajat Aziza afungue Mirathi.

Masjid Mwinyi tulifungua shauri la Mirathi Na. 40 Mahakama ya Kariakoo na kufanikiwa kumuweka Bwana Seif Kiambwe, mmoja wa wadhamini, kuwa msimamizi kwa kuwa Abdallah Rashid naye alikuwa mgonjwa na muda mfupi baadae alifariki dunia.

Tangazo la Mirathi tulilitoa katika gazeti Uhuru.

Na hakujitokeza mtu kupinga.

Mahakama ya Kariakoo ikatoa Usimamizi kwa Seif Kiambwe akiwakilisha Masjid Mwinyi.

Kujitokeza kwa mara nyingine Pius Kipengele na Steven Mwamkoa

Mara baada ya kupata usimamizi, Mahakama ya Kariakoo iliandika barua Manispaa Ilala na Wizara ya Ardhi kutambulisha usimamizi wa Masjid Mwinyi kwa mali za wakfu za Hajat Aziza Omar na kuzielekeza mamlaka hizo ziweke sawa nyaraka na kumbukumbu kwa mujibu wa sheria za umiliki, wakati huo huo kuwaamuru wanaodai umiliki kuondoka, ndipo walipojitokeza Pius Kipengele la Steven Mwamkoa wakati huo akiwa ameshauza nyumba Na. 17/56 Mtanzania mwenye asili ya Kihindi (Kiasia), Moez Jaffer Morbiwala.

Kwa hiyo Pius Kipengele, Steven Mwamkoa na Morbiwalla nyuma yake, walifungua kesi ya kupinga amri hiyo ya Mahakama ya Mwanzo katika Mahakama ya Wilaya mbele ya Mahakimu Mama Kaluyenda na Mama Minde.

Katika Hali iliyotatanisha na iliyoonesha kukanganya, wakati Hakimu akisoma hukumu, Wakili Musa Godwin wakati hukumu ikosomwa aliinuka kutaka kupinga hali iliyomshangaza wakili wetu Mheshimiwa Abdulafattah akiwakilisha Chamber ya Wakili Maige wakati huo.

Wakili Minde alimtuliza Wakili huyo, na kuendelea kusoma hukumu hiyo ambayo mwisho ilitoa ushindi kwa wateja wakili wa walalamikaji Bwana Steven Meamkoa akishirikiana na Moez Morbiwallah.

Hali iliyosababishwa, wakili wa Masjid Mwinyi Mh. Maige kukata rufaa Mahakama Kuu.

Wakati Masjid Mwinyi inaendelea na taratibu na taratibu za sheria, Steven Mwamkoa na Moez Morbiwala kwa kumtumia mmoja wa maafisa ardhi Ofisi ya Msajili Hati walifanikisha kufanya "transfer'' ya umiliki kutoka kwa Steven Mwamkoa kwenda Moez Morbaiwalla.

Hii ilikuwa kwenye nyumba Na. 17/56.

Ulaghai huu wa kisheria ulifanyika wakati faili zote mbili za nyumba 32/77 na 17/56 zikiwa na "Caveat."

Utovu huu wa kisheria ulifanyika wakati Msajili Mama Subira Sinda akiwa likizo.

Aidha Nyumba na 32/77 hati iliendelea kusomeka jina la Pius Kipengele kabla ya jitihada za kiutawala kutekeleza amri ya Mahakama ya Mwanzo kuhamisha umiliki kwenda Masjid Mwinyi, hazijakamilika.

Kwa sasa nyumba hii iko chini ya umiliki wa Masjid Mwinyi kabla ya Kipengele kufungua shauri Mahakama Kuu mbele ya Jaji Luvanda na Jaji Mgonya ambao wameamuru jina la Masjid Mwinyi lifutwe na kurejeshwa tena Kwa kuwa "taratibu za kisheria" zilikosewa.

Hukumu imeasababisha Masjid Mwinyi kwa kuzingatia rwajibu (role)ya Mahakama ya Rufaa katika utoaji haki, kuomba Mahakama ya hiyo chini ya Jaji Mkuu kufanya mapitio ya kesi nzima iliyohusisha kesi kadhaa ndani yake, ili haki ifike kunakostahiki.

Jitihada za Masjid Mwinyi kwa ushauri wa vyombo vya Ulinzi na Usalama

Wakati hali ikiendelea kutoeleweka, waumini misikitini wakiendelea kwa dua na kujihamasisha kufanya maandamano kwenda Ardhi kulalamika kwa nini wizara hiyo chini ya Waziri Profesa Mama Tibaijuka wakati ule imefanikisha mali za wakfu kuporwa na watu, tena wasio waumini wa dini hiyo, maafisa wa polisi hasa aliyekuwa OCD Msimbazi na maafisa wa Idara ya Usalama walishauri Masjid Mwinyi iendelee kufuata taratibu za kiutawala na kisheria kupata haki hizo ili kusaidia kutunza amani ikiwa ni pamoja na kuwatuliza waumini.

Masjid Mwinyi ilitekeleza kwa busara maelekezo hayo kwa kushirikiana na moja ya magazeri ya Kiislamu (Alhuda) kusaidia jukumu hilo la kutunza amani kuwazuia waumini kutumia nguvu zao kuhami mali hizo.

Masjid Mwinyi kwa kushirikiana na gazeti hilo walifanikiwa kuwatuliza Waislamu huku ikiendelea kusimamia suala hilo kwa njia za amani kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Hata hivyo hatua hii imekuwa na changamoto kubwa ya chuki, kuchafuliwa na lawama kubwa miongoni mwa Waislamu dhidi yangu na Masjid Mwinyi na kwa chombo husika cha habari kwa madai kuwa hatua zetu zinasaidia waporaji kupora Mali za Waislamu na kwamba tumehongwa na matapeli.

Na hasa wanapoona nyumba ya ghorofa sita ikiwa imejengwa na Moez Morbiwalla kiwanja cha wakfu na. 17/56 akiendelea na biashara zake bila hofu.

Nimeandika waraka huu mrefu kueleza ukweli juu ya Mali za Wakfu na suala la usimamizi wa Mirathi ya Hajjat Aziza Omar.

Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa nimekuwa mkweli na nimesimamia suala hili wakati wote yeye akinishuhudia na nafsi yangu ikishuhudia hivyo.

Najielekeza kwa MOLA wangu kuwa nimetimiza Amana.

Allah nishuhudie.

Nimebeba jukumu hili nikiwa na umri wa miaka 46 mwaka 1991 sasa nina miaka 78 ambalo limeendelea kutatiza na kuwa kizungumkuti katika mahakama zetu kwa takribani miaka 32 sasa.

Hivi sasa shauri hili liko Mahakama ya Rufani.

Ni Maombi yangu kuwa suala hili litapatiwa ufumbuzi wenye haki Kwa mujibu wa sheria.

Naamini ni wajibu wa Mahakama ya Rufaa kuichimba na kuitafuta haki kwa jicho kali zaidi ili iweze kufika kule inakotakiwa kwa sababu wajanja na watu wasio waaadilifu wamekuwa wakitumia taratibu na kanuni za kimahakama kupoka haki za watu katika jamii hali iliyosababisha dhuluma, chuki na wakati mwingine vurugu katika jamii.

Namuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu, hekima na busara na uadifilifu Rais Wetu Mpendwa Mama Samia na Serikali, Majaji, Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu, Mawakili wote na Mahakimu wote Mahakama zote nchini

Sheikh Abeid Maulid Abeid

Masjid Mwinyi
0713 326 695
Inahuzunisha sana,ALLAH atawalipa Insha Allah
 
Hii ni story ya upande mmoja,tengepata na story ya upande wa pili ingependeza sana.
 
Back
Top Bottom