Kesi ya Mali ya Wakfu Masjid Mwinyi Miaka 32 Bado Hukumu Kupatikana

Kesi ya Mali ya Wakfu Masjid Mwinyi Miaka 32 Bado Hukumu Kupatikana

Hii ni story ya upande mmoja,tengepata na story ya upande wa pili ingependeza sana.
Kumaliza huu ugomvi ni kazi sana. Wahusika muhimu walishafariki na waliobaki wote ni kama victims. Sasa kama huyo mhindi aliyejenga ghorofa ana kosa? Akiondolewa sasa hivi itakuwa siyo kumtendea haki hasa kama alifuata taratibu zote kwenye kununua hiyo sehemu. Kosa kubwa lililofanyika ni kutomaliza hili suala mapema, wakati mhusika mkuu anayetuhumiwa kutapeli akiwa hai. Hata huyo Pius sioni kosa lake na hata kama alikuwa anasaidia kumlipa wakili kwa sababu ana interest kwenye hili suala.
 
Zamani wenye Nyumba nyingi kuanzia Kariakoo,Ilala hadi Magomeni na kinondoni wengi walikua Wanawake na hawakua na Mume wala Watoto, ndiyo maana unaona Mali zao kila Mtu anagombania baada ya wao kufa na kutokua na mrithi!!
Hiii ilitokana na nn?
 
Wakfu huwa hautolewi baada ya mtu kufariki.

wakfu mtu anapaswa autoe akiwa hai.. mali zake zihamie kabisa kwa msikiti akiwa bado yupo hai.

mtu akifariki wakfu haukubaliki hapo ni mirathi tu ndiyo inayokubalika
 
Wakfu huwa hautolewi baada ya mtu kufariki.

wakfu mtu anapaswa autoe akiwa hai.. mali zake zihamie kabisa kwa msikiti akiwa bado yupo hai.

mtu akifariki wakfu haukubaliki hapo ni mirathi tu ndiyo inayokubalika
Hii kesi iliiisha?
 
Huyu Mzee wa Tandamti udini umemjaa hadi anashindwa ku reasons mambo.
Yani kwenye kesi kaleta malalamiko ya upande mmoja kwamba wailsmau wamedhulumiwa..
Hajabalansi stori yake
 
Umebalansi vp stori ikiwa hujasikiliza upande wa pili?!
Sidhani na wewe kama umepata habari za upande wa upili, kama upande wa pili akileta habari zao ndiyo tunaweza kupima na hukumu ikatolewa lakini mimi si hakimu, na kilicholetwa ni lalamiko la watu ambao kesi yao takriban miaka 32 hakuna suluhisho. Wewe ndiye ambaye unatakiwa uthibitishe huo udini kwenye bandiko hili.
 
hii ilishapitaga nakumbuka ilikuwa mwishoni mwa miaka 90s kama sikosei sin hakika
ila nakumbuka kipindi masjid mtambani inajengwa miaka 90 mwishoni
nondo zote zilikuwa zinasukwa pale KKOO MANYEMA ilikuwa umaliziaji tu
ilikuwa hatari IJUMAA mpk tukawa tunakatazwa na WAZAZI kwenda kuswali pale MTAMBANI mana muda wote kinanuka MABOMU na FFU
Edhi hizo ITIKADI ITIKADI kweli sio masihara
sio sasa BAKWATA pale imejaa MAMLUKI
hakuna zile ITIKADI
na walivyoubadirisha UONGOZI masjid IDRISA Itikadi ikapotea kabisa
sasa hivi hiyo MISIKITI haina ile itikadi tena iliyokuwa na MIONGOZO THABITI ya KIDINI
Hizo itikadi kali Zitatusaidia nini Waafrika kama wanapenda itikadi kali waende Afghanistan huko
 
Hiyo stori akili yangu inakataa hoja ya huyo mama kutoka singida awe na nyumba kazaa kariakoo. Na bado ndugu zake wasijitokeze kuishi nae.

Watu wasingida wanapenda sana kuishi pamoja hasa ndugu yao akiwa na nyumba mjini.


Pili naona kuna ujanja ujanja.. huo wasia wa nyumba zake zote zipewe msikiti akili yangu inakataa.

Naona hapo marehemu kafa .. kila upande umejipa umuhimu wa kumiliki mali zake kiujanja ujanja. Wosia feki imetengenezwa na upande mwingine na wengine nao hati feki wametengeza,, Upande ulioona umezidiwa ujanja ndio unaplay victim role.

Pia swala la kuibiwa hati zote. Yaani mtu uibiwe hati za nyumba yako upuuzie tu wala usiende ardhi wakupe copy zake.

Maana rekodi za hati zipo wizara ya ardhi

Matapeli wako kila sehemu..Singida, Urambo katavi etc
 
Back
Top Bottom