Kesi ya Masogange yakwama kusikilizwa tena

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Julai 13, imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili Agnes Gerald maarufu Masogange kutokana na kuwa mgonjwa.

Masogange anayetetewa na Wakili Ruben Simwanze amemuomba Hakimu Mkazi Mkuu Wilbrod Mashauri kuihairisha kesi hiyo kutokana na mteja wake kuumwa. Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serekali Costantine Kakula aliiambia Mahakama kuwa kesi imekuja kwa ajili ya kuanza kutolewa ushahidi na mashahidi wawili tayari wamefika.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mashauri alikubali ombi la upande wa utetezi na kusema; "mtuhumiwa anapoumwa huwezi kumlazimisha kusikiliza ushaidi.’ Awali, Masogange alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka 2017, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika maeneo yasiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam alitumia dawa hizo za kulevya
Tayari upelelezi umekamilika na kesi imehairishwa hadi Julai 20 itakapoanza kutolewa ushahidi.


Mwananchi

=====

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
Ataugua mpaka 2020

Sent from my Infinix NOTE 3 using JamiiForums mobile app
 
Kesi nyepesi hii ,kutumia madawa tena eneo lisilojulikana
 
Mbona manji alisomewa shtaka akiwa hospital?bure kabisa mahakama zetu.



Swissme
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…