Komando Mhina popote pale alipo na apokee salamu za kheri kutoka kwetu tunaoyaishi machungu yao.
Akiwa mtu huru, Commando Mhina alifika mahakamani kufanya sehemu yake ya kuuanika ukweli.
"Kwani nani anapenda kufika kwa ridhaa yake polisi au katika mahakama zinazosifika kwa dhuluma?"
"Kwa nini Commando Ling'wenya au awaye yote ahukumiwe kwa ushahidi wa uongo?"
Kama ilivyokuwa kwa ma Commando Ling'wenya, Adamoo, Malema, Urio, na Lijenje, Commando Mhina pia alikamatwa na kundi la akina Kingai, Jumanne, Mahita na Goodluck.
"Akihojiwa na wakili msomi Peter Kibatala 5/11/2021," Mahita Omar Mahita alikiri:
Kwa maelezo ya Commando Mhina, kulikuwa na convoy kubwa kwenye kukamatwa kwake iliyokuwapo hapo bila kujihusisha moja kwa moja. Ikiwa tayari tayari kama angejaribu kujitetea.
Kwenye mazingira kama hayo haipo namna ambayo Commando Lijenje angeweza kutoweka RAU madukani.
Commando Mhina alikamatwa akielekea Pub akapelekwa Central Polisi Tabora, moja kwa moja kwenye kinyumba nyuma ya jengo kuu (main block) kwenda kuteswa.
Baada ya kipigo kikali (cha masaa yasiyopungua 3) alipelekwa mahabusu Tabora Railways alikokaa kwa siku 2, kabla ya kuhamishiwa Nzega polisi mahabusu, alikokaa kwa siku 3.
Nzega, Mhina alikutana pia na Commando Malema aliyekuwa kaletwa hapo mahabusu polisi kwenye mazingira kama aliyofikishwa nayo hapo, yeye.
Makomando wawili hawa walisafirishwa kuja Dar chini ya ile ile himaya pendwa ya akina Kingai, Jumanne, Mahita, na Goodluck, ambako walifikishiwa 23/9/2020 moja kwa moja mahabusu Polisi Tazara.
Tokea 19/9/2020 Commando Mhina alipokamatwa na kufungwa pingu, hakuwahi kufunguliwa pingu hizo wala kupewa chakula hadi alipopelekwa mahakamani kisutu 25/9/2020.
Katika kipindi chote hicho hakuwahi kusajiliwa katika kitabu au register yoyote popote.
Wana nini cha kumwambia nani dhidi ya nani kina Kingai, Mahita, Jumanne au Goodluck naye akawaamini?
Bila shaka ni watu hawa hawa walio mkamata pia Mh. Mbowe usiku usiku Mwanza na kumsafirisha kuja naye Dar kibazazi wakimwahidi kuwa safari hii hachomoki.
Wapongezwe wote wanaokuwa na ujasiri wa kusimama imara kuufichua uongo dhidi ya ukweli.
Maisha na haki za watu haziwezi kuchezewa kwa kisingizio cha jina "serikali" kwa kiwango hiki. Kwani serikali hiyo itakuwa ina mwakilisha nani?
Nani kama Commando Mhina?
"Kudos Commando Mhina. Kwa hakika wewe ni shahidi wa haki na Rafiki mwema."
"Kwa hakika wapenda haki wote tutasimama nanyi kuona haipo haki yenu moja itakayopotea."
-----------
Sauti na Zipazwe Zaidi:
"Wako wapi makomando wetu. Wako wapi Urio, Malema na Lijenje ambao tunajua mara ya mwisho walikuwa mikononi mwa Kingai."