Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Binafsi nawapongeza maafisa wetu wa Jeshi la Polisi kwa nzuri wanayoifanya ya kutulinda raia wema wa nchi hii. Sisi tunalala na kukoroma, ninyi mnakesha mkisaka wahalifu ili sisi tuendelee kulala na kukoroma! Mungu awabariki sana!!!!!!Komando Mhina popote pale alipo na apokee salamu za kheri kutoka kwetu tunaoyaishi machungu yao.
Akiwa mtu huru, Commando Mhina alifika mahakamani kufanya sehemu yake ya kuuanika ukweli.
"Kwani nani anapenda kufika kwa ridhaa yake polisi au katika mahakama zinazosifika kwa dhuluma?"
"Kwa nini Commando Ling'wenya au awaye yote ahukumiwe kwa ushahidi wa uongo?"
Kama ilivyokuwa kwa ma Commando Ling'wenya, Adamoo, Malema, Urio, na Lijenje, Commando Mhina pia alikamatwa na kundi la akina Kingai, Jumanne, Mahita na Goodluck.
"Akihojiwa na wakili msomi Peter Kibatala 5/11/2021," Mahita Omar Mahita alikiri:
View attachment 2031579
Kwa maelezo ya Commando Mhina, kulikuwa na convoy kubwa kwenye kukamatwa kwake iliyokuwapo hapo bila kujihusisha moja kwa moja. Ikiwa tayari tayari kama angejaribu kujitetea.
Kwenye mazingira kama hayo haipo namna ambayo Commando Lijenje angeweza kutoweka RAU madukani.
View attachment 2031663
Commando Mhina alikamatwa akielekea Pub akapelekwa Central Polisi Tabora, moja kwa moja kwenye kinyumba nyuma ya jengo kuu (main block) kwenda kuteswa.
Baada ya kipigo kikali (cha masaa yasiyopungua 3) alipelekwa mahabusu Tabora Railways alikokaa kwa siku 2, kabla ya kuhamishiwa Nzega polisi mahabusu, alikokaa kwa siku 3.
Nzega, Mhina alikutana pia na Commando Malema aliyekuwa kaletwa hapo mahabusu polisi kwenye mazingira kama aliyofikishwa nayo hapo, yeye.
Makomando wawili hawa walisafirishwa kuja Dar chini ya ile ile himaya pendwa ya akina Kingai, Jumanne, Mahita, na Goodluck, ambako walifikishiwa 23/9/2020 moja kwa moja mahabusu Polisi Tazara.
Tokea 19/9/2020 Commando Mhina alipokamatwa na kufungwa pingu, hakuwahi kufunguliwa pingu hizo wala kupewa chakula hadi alipopelekwa mahakamani kisutu 25/9/2020.
Katika kipindi chote hicho hakuwahi kusajiliwa katika kitabu au register yoyote popote.
Wana nini cha kumwambia nani dhidi ya nani kina Kingai, Mahita, Jumanne au Goodluck naye akawaamini?
Bila shaka ni watu hawa hawa walio mkamata pia Mh. Mbowe usiku usiku Mwanza na kumsafirisha kuja naye Dar kibazazi wakimwahidi kuwa safari hii hachomoki.
Wapongezwe wote wanaokuwa na ujasiri wa kusimama imara kuufichua uongo dhidi ya ukweli.
Maisha na haki za watu haziwezi kuchezewa kwa kisingizio cha jina "serikali" kwa kiwango hiki. Kwani serikali hiyo itakuwa ina mwakilisha nani?
Nani kama Commando Mhina?
"Kudos Commando Mhina. Kwa hakika wewe ni shahidi wa haki na Rafiki mwema."
"Kwa hakika wapenda haki wote tutasimama nanyi kuona haipo haki yenu moja itakayopotea."
-----------
Sauti na Zipazwe Zaidi:
"Wako wapi makomando wetu. Wako wapi Urio, Malema na Lijenje ambao tunajua mara ya mwisho walikuwa mikononi mwa Kingai."
Kwani hata njia hiyo ya hirizi haiwezekani?Wale wana hirizi babu![]()
Movie Zinawatoa akili,. Jamaa hakua na kosa lolote alilotenda, yupo na ratiba zake za siku hana hofu wala wasiwasi wowote kwamba anawindwa anatoka zake kwenda kuangalia mpira ghafla anazungikwa na mapolisi wenye siraha na akaambiwa anahitajika kwa mkuu wa mkoa, we ulitaka afanyeje? Hata kama ni komandooMie mwenyewe nilishangaa sana comandoo unakamatwaje kizembe asee, tena kwenye pub za kuangalia mpira.... Wamedhalilisha sana fani ya ukomandoo..
Binafsi sielewi kwanini mbowe aliamua kuajiri hawa jamaa waluokua wamefukuzwa jeshini kwasababu mbalimbali....
Ukifuatilia hii kesi na comment za baadhi ya watu hapa JF, utajua Sisi watanzania ni katili kiasi gani.
Kesi inaonekana wazi kwamba imetengenezwa, lakini mashabiki wa ukatili wanaendelea kuwatete viongozi wao.
Viongozi hawa hawa ndio wanaotupilia mbali ufuatiliaji wa utekaji na mauaji yaliyofanyika kipindi cha nyuma.
Camera kwenye tukio la Lissu ziliondolewa, aliyeondoa hajakamatwa. Lissu alitandikwa risasi za kutosha polisi wanadai yeye Lissu na dereva wake hawatoi ushirikiano. Wangefariki ina maana isingechunguzwa kwa sababu hakuna ushirikiano?
Tukio la Akwelina, waliopiga risasi ni polisi. Lakini aliyekamatwa kwa kosa hili ni wengine tofauti kabisa.
Hii haileti picha katika uso Tanzania ilivyo na sofa kedekede,wanachama wa ccm muache kushabikia Mambo ya msingi Kama haya ya makomandoo,watu wanatoa hoja za msingi harafu mtu anaponda point.tunashindwa kuwaelewa na msifurahie hii kesi ya Mbowe na wenzake iposiku serikali ya ccm itapigwa chini kwa vigezo hivi vya haki ya mtu kukatisha maisha yake mjitafakari hapa mlipkfikia.
Hii kitu haitatokea Chini ccm kumbuka wanaufaika na huo uharamia inasemekana Sabaya analalama huko Jela kwamba kasaidia ccm kutangazwa mshindi HAI lkn wamtelekeza so ili haya yatokee tuongeze nguvu kudai Katiba tupate mfumo mpya wa utawalaNchi inanuka dhuluma:
1. Kesi hii kufutwa
2. Makomando wote kuachiwa
3. Kuwahikiki makomando wote waliotoweka
4. Kulishughulikia genge dhwalimu la kuna Kingai lililohusika na ukikwaji mkubwa huu wa haki
5. Kuwalipa fidia wahanga wote wa kadhia hii
6. Kufumuliwa kwa jeshi la polisi
7. Kuhakiki haki na ustawi wa makomando wote walioondoshwa jeshini
8. Nk.
Inaweza kusaidia kupoza chungu ya vidonda sugu vilivyomo mioyoni mwa watu.
Alaaniwe jiwe na washirika wake kokote kule waliko.
Hii kitu haitatokea Chini ccm kumbuka wanaufaika na huo uharamia inasemekana Sabaya analalama huko Jela kwamba kasaidia ccm kutangazwa mshindi HAI lkn wamtelekeza so ili haya yatokee tuongeze nguvu kudai Katiba tupate mfumo mpya wa utawala