Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Baada ya kesi ya Mbowe na wenzake kuondolewa / kufutwa na DPP mahakamani ni wakati muhafaka tukiangazia yaliyojiri kipindi chote cha kesi hii bila kuweka ushabiki na uzandiki.
Mosi,Kabla kesi haijaanza kusikilizwa IGP alitoa kauli nzito kwamba wanaushahidi mzito.Binafsi niliwaza na kuwazua iwapo kweli ushahidi mzito upo.
Baada ya Jamhuri kupeleka mahakamani mashahidi 13 badala ya mashahidi 24 nikajikuta nikiwaza na kutafakari iwapo kweli IGP Sirro ana akili nzuri !.
Tanzania ina idadi ya watu wanaokadiriwa kufika 60 million inaweza kama vipi taifa likawa na IGP wa kiwango duni kiasi hiki ?.Kauli ya mtu mzito wa kiwango cha IGP ilipaswa kuonekana wazi wakati mashahidi wa Jamhuri wakitoa ushahidi wao mahakamani.
Katika nchi za watu wanaojitambua IGP alipaswa kujiuzulu ili kumpa nafasi na wepesi mteuzi.IGP Sirro anastahili kubeba lawama na fedhea kwa jinsi mwenendo wa kesi ulivyokwenda ilionekana dhahiri ushahidi mwingi ilikuwa wa kupika au ukipenda kutunga.
Pili Majaji waliosimamia kesi hii walikubali pasipo shaka kupindisha sheria ilikumlinda mteuzi dhidi ya fedhea hasa kupitia matamshi yake na Kikeke.Kiwango cha weledi kimeshuka sana mahakama zetu si kimbilio la haki hata kidogo.Majaji mara kadhaa tena pasipo aibu wametoa maamuzi ya hovyo na wamekuwa sehemu ya uovu katika nchi yetu.
Mwisho Tanganyika inahitaji katiba mpya kuliko wakati mwingine wowote tangu kuasisiwa kwa taifa letu.