VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kesho tarehe 5/8/2021, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, itatajwa kesi ya jinai inayomjumuisha Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe. Mbowe pamoja na wenzake watatu wanashtakiwa kwa makosa mbalimbali ya kijinai.
Kwake binafsi, Mbowe anashtakiwa kwa mashtaka ya kula njama na kufadhili vitendo vya kigaidi. Washtakiwa wenzake walianza kupandishwa kizimbani huku Mbowe akiunganishwa baadaye.
Maandalizi ya tukio la kesho yameshafanyika na kukamilika. Magereza alipo, wamejipanga na kupangika kuhakikisha kuwa Mbowe na wenzake wanafikishwa na kurejeshwa salama salmini gerezani.
Polisi wamejipanga, kuanzia nchi kavu hadi anga, kuimarisha ulinzi bila ulanzi kuhakikisha usalama usio na lawama mahakamani hapo. Polisi wamejiandaa 'kuwahi' mapema sehemu ya tukio ili 'kukagua' na 'kudhibiti' wanaoingia mahakamani hapo.
Mawakili wa pande zote mbili wamejipanga bila mapanga kutetea pande zao za mashtaka na utetezi kusiko na utelezi. Mawakili wa Serikali wamejiandaa kuthibitisha makosa ya Mbowe na wenzake watatu huku wa CHADEMA wakijiandaa kumtetea kisheria Mbowe na kumnasua kwenye kesi hiyo.
Vyombo vya habari vya ndani na nje vitafurika hadi kufunika Kisutu. Nasi wananchi wa Dar es Salaam tutajongea kushuhudia 'kipute' hiki kitakachoanza kesho.
Amini nawaambia, Kisutu kwa kila siku Mbowe atakayoletwa na hata akianza kupelekwa Mahakama Kuu, hapatatosha. Mahakamani, pumba na mchele vitatenganishwa. Tukutane Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kesho.
Pumzika kwa amani mtani na mdogo wangu Elias Kwandikwa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam