Kesi ya Mbowe: Kupoa mno Kwetu ndilo Tatizo Kuu

Kesi ya Mbowe: Kupoa mno Kwetu ndilo Tatizo Kuu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kama ilivyo tarajiwa hukumu ya leo haikuwa na jipya kama zitakavyokuwa za siku zijazo.

Refa kajikita kutafuta chochote dhidi ya upande wa utetezi ili kutupilia mbali lolote wanalo wasilisha.

Ama kweli ni refa mchezaji aliyedhamiria kweli kweli.

Hoja ngapi za mashtaka zilikuwa na utata mwingi lakini zote kazifumbia macho?



Wako wapi wanaume chapa ya moto (fire brand)? Kwani hawapo? Hii ndiyo type ya mheshimiwa Mbowe ambaye bila wao kumepoa.

Kwa hakika ndiyo sababu wanamshikilia na wataendelea kuwa naye kwa muda mrefu sana:

Mbowe: Kwanini atashikiliwa kwa Muda Mrefu

Bila amsha amsha za haja wanatuchukulia poa tu.

Itambulike haipo tija tunayotegemea kupatikana kutokea mahakamani bila ya kuwepo kwa uwazi wa hisia zetu kwao.

Tulipo hawaoni athari wala hatari yoyote ya kujifanyia lolote na kwa vyovyote.

Lembrus Mchome alituwakilisha vyema, ila haitoshi.

Ilikuwa ni muhimu sana kwa Makumi kwa elfu yetu hisia zetu wakazielewa bayana.

Ni hayo tu ndugu Makamanda.
 
Chadema kusubiri huruma ya watesi huku watesi.

Hii ni sawa na kifaranga cha kuku awe anajichekesha na kujisogeza mbele ya mwewe. Akitarajia kwa kufanya hivyo atahurumiwa na mwewe.
 
Chadema kusubiri huruma ya watesi huku watesi.

Hii ni sawa na kifaranga cha kuku awe anajichekesha na kujisogeza mbele ya mwewe. Akitarajia kwa kufanya hivyo atahurumiwa na mwewe.

Uongozi ni pamoja na kuchukua risks. Tulipo ni muhimu kuchukua risks na kwa hakika wala si risks. Tayari wapo kwenye spotlight.

Wenye kigugumizi na amsha amsha za kueleweka huu uwe muda wao wa kukaa pembeni.

Hii nchi itakombolewa na wenye moyo.

Kesi za Winnie Mandela zilikuwa haziendeshwi kwenye ubaridi huu. Pamoja na kesi ya wazi ya kuuwawa Stompie Seipei mikononi mwake Winnie aliachiwa huru.

Nyakua nyakua iliyokuwa ikiendelea nje ya viunga vya mahakama, ilikuwa tosha kabisa kupeleka ujumbe mahsusi kwa Jaji na hata mashahidi kwamba umma ulikuwa ukitaka nini.
 
Back
Top Bottom