Leo kumekuwapo shahidi mahakamani kuonyesha Ling'wenya hakuwahi kufikishwa Tazara Polisi.
Shahidi huyu ana anayodai kuwa ni detention register kama ushahidi. Baadhi ya kurasa zake zimenyofolewa na nyingine zimeongezwa.
Si mageni kusikia polisi wamebambikizia watu kesi, wamewaweka watu rumande kwa majina bandia au hata bila kuwaandikisha kabisa.
Yamewakuta kina Mdude, kina Ulimboka na wengi wengine. Yumkini kina Ben, Lijenje au hata Azory ni hali hizo hizo. Ni hakika kwa maneno ya Sirro kuwa:
"Polisi hawa siyo malaika."
Haki za watu haziwezi kuendelea kuchezewa hivi.
Kwa maana halisi ya haki, kwa nini ushahidi wa kisayansi uliopo usitumike kutenganisha mbivu na mbichi hizi?
Ushahidi wa ma CCTV lukuki yaliyoko sehemu mbalimbali na pia kutokea kwenye makampuni ya simu za mkononi mbona upo?
Kwa vile ushahidi huu ni bora zaidi, hazipo sababu ya kutokuuhitaji ili kutumika mahakamani?
Nyendo kamili za Kingai, Mahita, Jumanne, Goodluck na timu nzima tokea RAU hadi Mbweni ni muhimu kuhakikiwa zaidi ya maneno yao.
Mahakamani kusifanywe kuwa kichaka cha kupitishia uongo dhidi ya watu wengine.
Maneno ya mtu dhidi ya mwingine, kwa "litmus paper" ipi kuthibitisha mwongo ni yupi?