Kesi ya Mbowe: Madai Mahakamani yathibitishwe Kisayansi

Mwisho huo hapaswi kuachiwa Mungu peke yake madhali kesha tuonyesha ilipo nia ovu ilipo.
Mfano nimeshangaa eti hicho kitabu kuna missing pages sasa unajiuliza register muhimu kama hiyo haina serial number? Hakuna utaratibu wa kimahakama wa kukataa document ambayo imekuwa tempered au kufanyiwa forgery? How come document ya serikali, tena ya polisi inatiliwa mashaka na bado inaendelea kuwa kielelezo mahakamani?? Imagine eti vituo vikubwa vya polisi kama hivyo vya Dar mhalifu anaingia pale haingizwi kwenye mifumo ya kisasa ya computer ya kumchukua picha mhalifu, finger prints etc.... Sishangai ile issue ya Lugumi ya kuweka computer system kwenye hivyo vituo ilipigwa chini..
 
Kwanini mawakili wa utetezi wasiwasilishe maombi rasmi kuhusu haya 3 tumwone Jaji ataamua vipi?

Mention register (za kustukiza) za Moshi na Mbweni zilikuwa muhimu kwa kesi hii pia.
Jaji anaweza kuwaambia hafundishwi kazi, ndio maana kwenye lile pingamizi la mwanzo kabisa licha ya jaji kumsogelea mtuhumiwa na kuyaona yale majeraha lakini hakuhangaika kuyaweka kwenye rekodi zake, typical politics.
 
Jaji anaweza kuwaambia hafundishwi kazi, ndio maana kwenye lile pingamizi la mwanzo kabisa licha ya jaji kumsogelea mtuhumiwa na kuyaona yale majeraha lakini hakuhangaika kuyaweka kwenye rekodi zake, typical politics.

Kwanini tuwe manabii kumsemea jaji? Kwanini asiseme mwenyewe tukamsikia?

Akitamka tutapima na kuchukua hatua?
 
Naona kama mahakama inazunguka mno na vielelezo ambavyo ni wazi inatakiwa ivikatae. Judge kuna maeneo ana nafasi ya kukataa kielelezo lakini unaona bado anakipokea tu. Naona sheria wakati mwingine inazunguka barabara ndefu bila sababu. Judge anayumba sana.
 
Huwezi ukadhulumu haki ya mtu Kisha ukaendelea kubaki salama,
Labda kama Mungu hayupo.
Lakini yeye mwenyewe katamka"mimi Niko ambae Niko"

Pamoja na yote hayo hatupaswi kumwachia Mungu peke yake. Ndiyo maana akatujalia alivyotujalia.
 
Kwanini Mawakili wa utetezi wasishinikize ushahidi huu kuletwa mahakamani?

Kwanini Mawakili wa utetezi wasishinikize kuwepo ushahidi wa daktari kuhusiana na hali za washitakiwa?

Kama mawili haya hayakubaliki kuna haja gani ya kuendelea na kesi hii?

Utetezi uko katika kuleta shaka kwa sababu sheria zetu zinataka ushahidi usiokuwa na shaka! Na panapokosekana ushahidi wa kisayansi, basi uliopo ndio wenye mashaka na kama upande wa mashtaka hauyaondoi - basi washitakiwa hawewezi kuadhibiwa.

Shida ni hii - je washitaki na mahakama wanatenda haki?? Kama hawatendi haki hakuna kitu wakili wa utetezi anaweza kubadilisha hilo.

Unaposikia Polisi anasema “sio muhimu kuandika diari au kusaini dention register” inaleta picha kuwa kuna uwekano kuwa mtuhumiwa anaweza pia asiandikwe majina kwa sababu amri za wakubwa ni muhimu kukiko taratibu ama sheria. Ukizingatia sio polisi wote walishughulika na hawa watuhumiwa walijia kinachofanyika - holes zilo za kutosha.
 
brazaj, I am lagging behind! Hivi shahidi wa leo alikuwa anatoa ushahidi ku establish nini? Na what is the significance of that which he was struggling to establish?
 

Mkuu umeeleza vizuri sana. Lakini ni wazi kuwa si mahakama wala upande mashtaka wanaoonekana kutenda haki. Rejea:

1. Ushahidi wote wenye mashaka unaoletwa na upande wa mashtaka.
2. Hukumu za majaji Luvanda, Siyani na hata Tiganga katika hatua mbalimbali.

Kwenye hali hii utetezi hauna uwezo wa kufanya lolote kupata ushahidi ulio bora zaidi kwa mustakabala wa haki badala ya kujikita kwenye ku "poke holes" tu kwenye ushahidi wao tu?

Kumbuka Siyani alidai mbona utetezi hawakutaka DR ya Moshi iletwe mahakamani au hata kupinga ile ya Central isipokelewe?
 
brazaj, I am lagging behind! Hivi shahidi wa leo alikuwa anatoa ushahidi ku establish nini? Na what is the significance of that which he was struggling to establish?

Mkuu aya mbili za mwanzo kwenye uzi huu zime summarize yote ya shahidi huyu. Yote yamo:

"Alitokea wapi, walikuwa na nia gani na wapi wameendelea kuyakoroga."
 
Kumbe tupo wengi, mimi naona ujinga mtupu sifuatilii tena hiyo kesi.
 
Hayo kamweleze Jaji, hapa unapoteza muda tu
 
Kumbe tupo wengi, mimi naona ujinga mtupu sifuatilii tena hiyo kesi.

Hauko peke yako. Wengi hatufuatilii tena. Ila hilo limekuwa ndiyo lengo lao kuu tusifuatilie. Kama vipi Ikiwezekana na mahakamani tusifike kabisa.

Nia yao ni kuwatenga washitakiwa na sisi.

Kwa kuacha kufuatilia, hadi hapa - watakuwa wanahesabu mafanikio makubwa.
 
Leo kumekuwapo shahidi mahakamani kuonyesha Ling'wenya hakuwahi kufikishwa Tazara Polisi.

Shahidi huyu ana anayodai kuwa ni detention register kama ushahidi. Baadhi ya kurasa zake zimenyofolewa na nyingine zimeongezwa.
Had it not been for Liganga to adjudicate this case, this alone will qualify to disqualify this blood bastard lies teller!
 
Had it not been for Liganga to adjudicate this case, this alone will qualify to disqualify this blood bastard lies teller!

The today's witness was gathered informally to testify. This was done just a few days ago.

He confessed, not to had been aware that he was to appear in court.



"They brought him (only) to show the accused were never at Tazara."

Equally then, why shouldn't we show the Kingai were never anyhow close to "Central" on the said days?
 

Mwenyewe niliacha fatilia ni vile maamuzi yalishafanyika wanajaribu tengeneza mazingira ionekane ni halali kwa maamuzi yao
 
Kama tunakubaliana utetezi upo kwa ajili ya kuleta shaka basi pia tukubaliane kwamba utetezi wameshaona hawawezi kushinda hii kesi mahakama kuu kwa mazingira yaliyopo na yanayoendelea kutokea kila siku.

Hii shaka unayoisemea hapa manufaa yake yatakuja kuonekana mahakama ya rufaa kama upande wa utetezi wakikata rufaa kupinga hukumu watakayopewa watuhumiwa na mahakama kuu, something which is so plain for eveeyone to see.

Anachotaka brazaj ni kuondoa hizo shaka ili ikiwezekana kesi iishie mahakama kuu hapo hapo, na hiki kwa mtazamo wangu natilia shaka kama kitawezekana kutokana na tabia za majaji walizoonesha kwenye hii kesi mpaka sasa.

Kuanzia yule wa kwanza kuwafundisha jamhuri nini cha kufanya, wapili kuikataa pingamizi licha ya PGO kukiukwa, na huyu wa tatu kuendelea na tabia hizo hizo kwenye mengi ya mapingamizi yanayowekwa na utetezi.
 

Ni muhimu jitihada zote kabisa bila kuacha moja zikafanyika kwenye hatua hii ya shauri la Ling'wenya.

Kwenye shauri la Adamoo tuliamini hakukuwa na haja ya kufanya yote kwani kama ni kuonyesha tu mashaka kwenye ushahidi wa mashtaka kwa hakika hakikuachwa kitu.

Itapendeza kuacha kuufunga ushahidi upande wa utetezi kwenye shauri hili kabla ya kuyasikia maamuzi ya mahakama kuhusu ushahidi wa:

1. CCTV camera records za RAU - Moshi - Arusha - Dar - Mbweni kuwahusianisha kina Kingai.
2. Mobile phones records RAU - Moshi - Arusha - Dar - Mbweni kuwahusianisha kina Kingai.
3. Ripoti ya daktari kuhusiana na kuteswa kwa Ling'wenya.
4. Kuletwa kwa wanaoitwa wasiri wa Kingai.

Tupate huduma hata za wapelelezi binafsi kukusanya ushahidi wowote zaidi unaoweza kusaidia.

Thamani ya haki na uhuru wa mtu ilinganishwe na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…