Kesi ya Mbowe: Madai Mahakamani yathibitishwe Kisayansi

Kama yapo ambayo kina Kibatala wanatakiwa kumwambia jaji naamini mengi wameshafanya hivyo, labda machache wakumbushwe

Ila nikwambie kitu, hata ushahidi wa daktari kisheria bado haumlazimishi jaji kutoa maamuzi ambayo mimi nawe tunaweza kuyatarajia, kwasababu hizo ni fani mbili tofauti, pamoja na yote kufanyika, jaji bado anaweza kuchanganya na facts nyingine kwenye kesi akaamua shauri tofauti.
 

Ninakubaliana na wewe. Lakini tufanye yetu yote.

Mwache Jaji aamue anavyotaka.

Tutakuwa tumenawa mikono.
 
Nikazie, kesi hii inaweza kuishia hapa kwa wao kuamua kutoyafanikisha kupatikana kwa:

1. CCTV camera records za RAU - Moshi - Arusha - Dar - Mbweni kuwahusianisha kina Kingai.
2. Mobile phones records RAU - Moshi - Arusha - Dar - Mbweni kuwahusianisha kina Kingai.
3. Ripoti ya daktari kuhusiana na kuteswa kwa Ling'wenya.
4. Kuletwa kwa wanaoitwa wasiri wa Kingai.

Bottom line tunasubiri wao kuyawasilisha hayo na yote tunayoyahitaji kutoka kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…