Shahidi wa leo, kwenye kesi dhidi ya Mh. Mbowe na wenzake, bwana Fredy ametudhihirishia wateja wa mitandao ya simu kuwa polisi wanaweza kwenda kwenye hii mitandao na kuwaambia wenye mitandao wawape taarifa zako zote, kama mawasiliano, ulipo, miamala yako, wao hata hawaulizi ni kwaajili ya nini, wanawapa.
Watanzania hatupo salama kiusalama wala kifaragha, kila unapotumia mtandao wa simu. Polisi mwenye nia mbaya nawe, anaweza kwenda kwenye mitandao, na kuomba location yako, atapewa; akitaka kujua una mahusiano na mtu gani, atapewa; akitaka kujua simu yako ilituma hela kwa nani na ina balance kiasi gani, anapewa; atapewa chochote anachotaka alimradi tu ni polisi.
Hii ni wakeup call, kuwa usitumie mitandao ya simu kama siyo lazima sana. Labda utumie zaidi data ili mawasiliano yawe kwa whatsap, skype au telegram, huduma ambazo savers hazipo nchini, lakini siyo sms wala calls, au kutuma hela.