Kesi ya Mbowe na wanasheria wa Tigo na Airtel ikumbushe wenye mamlaka kutunza siri za wateja ni muhimu kujenga sekta imara ya benki na mawasiliano

Kesi ya Mbowe na wanasheria wa Tigo na Airtel ikumbushe wenye mamlaka kutunza siri za wateja ni muhimu kujenga sekta imara ya benki na mawasiliano

Police ni chambo cha usalama na kudai taarifa za mtuhumiwa yeyote au mtu anayepelelezwa ni sawa kabisa ...achani ushabiki wa kisiasa..maana ya usalama nini sasa..kwa hiyo wasipewe huo uwezo ili nchi itekwe mara moja..achani ushabiki na ujinga..kwa hiyo police wakatufute order mahakani ili process ya kubaini wahalifu mara moja liwe complicated..acheni ushabiki
Huna akili hata moja mkuu....sorry to say that
 
Kwan kweny mwenendo wa hii kesi wewe umesikia kwamba shahidi alipata hyo order ya mahakama kutoa hizo taarifa ? Kama angefuata taratibu za kisheria zinavyotaka wala hakuna shida mkuu tusifanye kazi kwa mashinikizo bali kwa sheria na miongozi yetu

kwa sababu mtuhumiwa ni mbowe au sababu ni kweli mteja ana haki ya kufichiwa taarifa zake na mtandao??
 
Hata kama mtuhumiwa angekuwa Sabaya.
Ni kweli hata kama ni raia au mtu yoyote hata kama siyo mbowe ila ukweli ni kwamba taratibu hazikufuatwa hapo hata tigo waruke vip ila wamezingua, privacy ya mtu awe mbowe mimi au wewe ni kubwa sana hivyo sheria na taratibu lazima tujue zinatakaje siyo kufanya kazi kwa maelekezo na mazoea
 
Naona kila mtu anazungumzia usiri kuhusu kutoa taarifa za wateja. Hili jambo sijaelewa, mfano ikitokea kuna jambo lolote baya linafanywa na mteja, kisheria imekaaje? Tigo inapaswa kumlinda mteja mmoja hata kama jambo lolote hatarishi linalenga wateja wengi?...

Mmmh
kuna ishu moja ili trend sana dunian hapo kati ya kigaidi, kuna gaidi mmoja wa mashariki ya kati huko alikamatwa na jeshi la marekani asa ushahidi ulikuwa kwenye iphone so ilibid iphone ifunguliwe ili ushaidi uonekane,. asa gaidi mwenyewe aligoma kufungua sim yake kwaiy jeshi la marekani liliomba kampuni ya apple wafungue passcode lkn mpka mwish apple waligoma kufungua kwa kuwa wenyewe wanatunza siri za wateja.. nafikir hapo utakuwa umelewa
 
Shahidi wa leo, kwenye kesi dhidi ya Mh. Mbowe na wenzake, bwana Fredy ametudhihirishia wateja wa mitandao ya simu kuwa polisi wanaweza kwenda kwenye hii mitandao na kuwaambia wenye mitandao wawape taarifa zako zote, kama mawasiliano, ulipo, miamala yako, wao hata hawaulizi ni kwaajili ya nini, wanawapa.

Watanzania hatupo salama kiusalama wala kifaragha, kila unapotumia mtandao wa simu. Polisi mwenye nia mbaya nawe, anaweza kwenda kwenye mitandao, na kuomba location yako, atapewa; akitaka kujua una mahusiano na mtu gani, atapewa; akitaka kujua simu yako ilituma hela kwa nani na ina balance kiasi gani, anapewa; atapewa chochote anachotaka alimradi tu ni polisi.

Hii ni wakeup call, kuwa usitumie mitandao ya simu kama siyo lazima sana. Labda utumie zaidi data ili mawasiliano yawe kwa whatsap, skype au telegram, huduma ambazo savers hazipo nchini, lakini siyo sms wala calls, au kutuma hela.

hicho ni kitu cha kawaida sana , hakuna mtandao ambao haukusanyi taarifa zako lasivo internet isingekua na hela
 
Huna akili hata moja mkuu....sorry to say that

polisi wana haki zote kupata taarifa zako wakati wowote wanapozitaka bila maswali yoyote, na bila hata ya kuzifuata wana uwezo ya kujua chochote kinachohusiana na simu yako mpaka location wanajua, na ukipoteza simu ukitaka kuipata haraka we nenda polisi mitandao ya simu haiwezi kukurudishia simu kwa sababu hawajui iko wap
 
Wakuu, habari ndiyo hiyo, tumefumbuliwa macho na mwanasheria wa kampuni husika, Hakuna usiri wowote wa mteja unaolindwa.

Wala Hakuna taratibu zozote za kuwashirikisha wateja au mahakama pale taarifa zinapohitajika kitu kilicho kinyume na sheria.

Kuweni makini Sana wateja wa Tigo

usiri gan wakati ni haki yao kupata taarifa zako mda wowote
 
Si rahis kiivyo mnavyofikiria kupata taarifa za mteja wa tigo ni mziki mnene hata polis wanajua hili uwepes wanaopta ni kutoka mindao mingine hata waliomba taarifa kwa kampun hizo hupata kwa haraka niwahi shudia hiyo
 
Lazima kuwepo na utaratibu maalum wa kutoa hizo taarifa ambao unamlinda mteja dhidi ya matumizi mabaya ya taarifa zake. Nchi zote zinzothamini taarifa za wateja jaji wa mahakama lazima aidhinishe kwa warrant kuachiliwa kwa taarifa za mteja, sio polisi au mamlaka ya mawasiliano inaamua tu na kupewa taarifa za wateja.
Hata hiyo kufanya Kila kitu mmoja imeshangaza sana bila hata jopo la management kuhakiki nini mfanyakazi mmoja anafanya yaani nimeajua ndo maana ukitumia mtu hela unashangaa msg za kijinga na utapeli zinaanza kutumwa kwenye simu maana yake Kuna watu wanaamka Asubuhi kuingia kazini kuchungulia line za watu.
 
Hii sheria ina udhaifu mkubwa sana, haipaswi kuwa ni police officer au law enforcement officer bali inapaswa kuwa ni mahakama.
View attachment 1996101View attachment 1996102
Wakili Fred kaulizwa kama alitajiwa tuhuma za huyo mteja akasema hapana. Akaulizwa alivojibu alitaja tuhuma akasema hapana!
Muhimu alichosema ni kuwa kwao Tigo compliance (utii) ni muhimu kuliko Siri za mteja wao. Japokuwa alikuwa na uwezo wa kuhoji na kumtaka polisi mtaka taarifa kutumia vifungu vingine vya sheria hiyo hiyo..View attachment 1996103
 
Kesi ya Mbowe inayoendelea iliamshe bunge kama mhimili na chombo cha kutunga sheria, kuweka sheria madhubuti za upatikanji taarifa za wateja katika simu, mabenki, hospitali na huduma nyingine. Hii itasaidia sana pia kuvutuia uwekezaji kutoka nje.
Bunge la nani? Ndugai? CCM? mashetani watupu
 
Aisee. Kumbe tuna double staneard na Mihemko. Msumeno ukate kote kote. Privacy za mtu zinweza kuhitajika na vyombo vya usalama vya nchi
 
Kama ilifanyika hivyo bila idhini ya mahakama ni kosa. Bahati mbaya sana hakuna watu wengi makini waliofuatilia au wanaofuatilia kesi za Sabaya kwa sababu ya udhalimu wake mwingi aliotuhumiwa nao kuwafanyia binadamu wenzake hata kabla ya kufikishwa mahakamani.
Sheria haiko hivyo haina macho eti kwa sabaya kwa kuwa ni jambazi sawa kwa mbowe kwa kuwa ni kipenzi chako ndio ukurupuke kutetea
 
Kwa mwenendo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA freeman Mbowe na ushahidi na mashahidi wanaojitokeza kuna vilio vitakuja baadae.

Shahidi namba 05 wa leo ama kwa kujua ama kutokujua au kwa kushinikizwa unaona kabisa ameitumbukiza shimoni TIGO na MIC.

Huyu Shahidi wa TIgo anaonesha kabisa kuwa hajui ama alifanya kwa kufuata maelekezo. Kuna sehemu anasema wao mtu yeyote akipata barua toka Polisi kuhusu kuchunguzwa kwa mtu hawaangalii chochote.

Hapa anabanwa na sheria ya faragha. Mbowe anapiga hela hapa. Hata kama Mbowe atafungwa kwa case atakayofungua dhidi ya TIGO ana uhakika wa familia yake kuishi kwa raha.

TIGO wamejiingiza katika mgogoro mkubwa na watumiaji wengine. Wasijione wapo bora waulize gazeti kongwe duniani lilivyofutika katika uso wa dunia.

Mwanasheria wa TIGO kama mlinda siri wa Wateja.

Hii kesi inaleta mengi.
Umepaniki. Relax.
 
Lazima kuwepo na utaratibu maalum wa kutoa hizo taarifa ambao unamlinda mteja dhidi ya matumizi mabaya ya taarifa zake. Nchi zote zinzothamini taarifa za wateja jaji wa mahakama lazima aidhinishe kwa warrant kuachiliwa kwa taarifa za mteja, sio polisi au mamlaka ya mawasiliano inaamua tu na kupewa taarifa za wateja.
Samahani mkuu niulize.
Hivi vyombo vya usalama vya nchi, TRA na Taasisi zingine kutaka kujua kuwa kuna uwezekano wa hujuma kuwepo na kutaka taarifa kwa ajili uchunguzi ni MATUMIZI MABAYA? Au kukosa weledi wa watendaji wa Taasisi ndio VIBAYA?

Pia maoni yangu tunahamisha goli, sasa tunajadili privacy ya Mbowe jambo ambalo ni Sawa lkn tunaacha kuziba kuwa kufanya miamala sio Kosa ana Haki ya kumtumia au kupokea pesa halali.
As if tuna cover kuwa kuna uhalifu kwa kutumia miamala.
 
Inapohitajika kufanya hivyo na hivyo vyombo ni muhimu sana kukawa na pande ya katikati ambayo itahakikisha haki na mahitaji ya wote yanazingatiwa na huo upande duniani kote katika nchi zilizoendelea na kustaarabika huwa ni Mahakama. Mahakama inapaswa kusimama katikati ya mteja, chombo cha dola na kampuni kuhakisha utaratibu na haki za mteja zinazingatiwa.
Samahani mkuu niulize.
Hivi vyombo vya usalama vya nchi, TRA na Taasisi zingine kutaka kujua kuwa kuna uwezekano wa hujuma kuwepo na kutaka taarifa kwa ajili uchunguzi ni MATUMIZI MABAYA? Au kukosa weledi wa watendaji wa Taasisi ndio VIBAYA?

Pia maoni yangu tunahamisha goli, sasa tunajadili privacy ya Mbowe jambo ambalo ni Sawa lkn tunaacha kuziba kuwa kufanya miamala sio Kosa ana Haki ya kumtumia au kupokea pesa halali.
As if tuna cover kuwa kuna uhalifu kwa kutumia miamala.
 
Back
Top Bottom