Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta



Je Askari waliotumikia nchi tena vitani kwa level ya komandooo wakiondolewa kazini kuna kosa kujitafutia kipato halali ? Mbona Lugumi naye alichukua wa aina hiyo walioko mitaani wakawa walinzi wake ? au wanataka wakawe walinzi wajummbani au walinde ATM ? au wanataka wakaajiriwe na waasi huko DRC na nchi zingine maana ajira ziko nje nje ….
Kama Rais Samia alivyosema ; Tutende haki ili Mungu asituadhibu….
Kama hii kesi haingeenda mahakamani tungejua vipi kuwa Komando huyu haonekani kama ilivyo kwa Komando Ramadhani Kadego ( na pengine wameuliwa
Serikali ya JPM imetuachia makovu sana na kimsingi tunahitaji mambo mengi zaidi kama haya yawe wazi ili tuweze kufanya marekebisho makubwa
Mfano leo hiii wanajeshi wanawafikiria vipi Polisi ?
 
wenye akili zao hawewezi kuamini maneno ya uongo ya Ligwenya/ Adamoo, huyo ni mtuhumiwa wa Ugaidi anaye daiwa kumtumikia mtuhumiwa Mbowe.
kama walidhani wanaweza kupoteza amani yetu ya Tz basi wajue amani ya Tz lazima ilindwe kwa gharama yoyote ile.
HAKIKA wewe ni mkuundugu yangu
 
Nyerere ndie alieweka misingi mibovu ya taifa ili!! Nyerere alishindwa kuweka misingi imara ya nchi,yeye na wenzake waliongoza nchi hii kwa misingi binafsi na ukatili wa hali ya juu sana.

Ndio maana kila mtawala anaefata anaongoza kwa utashi wake na sio kwa misingi ya katiba,maana system inayotumika ni ile ile ya Nyerere aliyorithi kutoka kwa wakoloni,mbinu wanazotumia ni zile zile walizo tumia wakoloni na Nyerere, kutesa,kuua, kubambika kesi, kuhujumu wapinzani wake mbinu ni zile zile tu.

Mwinyi kidogo alikuwa mcha Mungu ndio maana akutesa watu ila system ilimlazimu kupitisha wananchi jehanamu,waliofuata wote kuanzia kwa Mkapa,Kikwete,Magufuli wamedhulumu sana uhai wa watu wengi sana mpaka sasa, kwa utawala wa uyu mama dhuluma ya uhai na mateso inaendelea ni kawaida approach inayotumika ni ile ile ya Nyerere, kutesa na kuua hakuna utu.

Nyerere alivyoona hana nguvu tena ndio akajigeuza malaika na kuanza kuhubiri demokrasia ambayo yeye hakuitenda hata robo na wala hakuwahi kuiamini katika utawala wake,Mungu ampumzishe uko aliko kushindwa kwake kujenga misingi mizuri ya taifa ili ndio kunatughalimu mpaka leo.
 
Acheni uoga mmezidi kutishia uhai viongozi wa nchi. Huyu au yule akifanya hivi mnamtishia kifo. Saiv mmetulizwa kimyaaaaa sijaona tena vitisho kwa ndungai wala mama Samia. MLIZIDI MKOME
Utakuwa una mpasuko kwenye ubongo,au ubongo wako umejaa maji,yaani watu wasiokuwa na madaraka yeyote wamtishie Rais wa nchi hii kifo?! Are you serious? Rais ambae ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,atishiwe uhai wake na mkulima mmoja? Utakuwa umeandika kufurahisha genge tu nafikili
 
Povu lote pumba tupu.
 
Tunaomba kuonyeshwa japo mabaki ya MOSES LIJENJE sisi kama ndugu zake tukazike!!
 
Yaan unataka kesi ifutwe?Inaonekana ,unataka tusiyajue mengi.
Kesi ya Mbowe ni mpango wa Mungu ili kufunua yote yaliyofunikwa. Kwa mfano mpaka kesi iishe tutakuwa tumejua idadi kubwa ya vikundi vya wale wanaoitwa "WASIOJULIKANA!" ambao hata Polisi wanasema hawawajui. Tumeanza kujua nani wanakamata watu, kuwaficha, na kuwaua!
 
Nawaza kimya kimya makomando wa jeshi waliofukuzwa kazi wanapoajiliwa na kiongozi mkuu wa upinzani siri za serikali zinakuwa salama? hatuna haja ya kujiuliza akina kigogo wanapata wapi taarifa
 
nawaza kimya kimya makomando wa jeshi waliofukuzwa kazi wanapoajiliwa na kiongozi mkuu wa upinzani siri za serikali zinakuwa salama? hatuna haja ya kujiuliza akina kigogo wanapata wapi taarifa
Kwani kiongozi wa upinzani ni Raia wa nje ya nchi?? au mwanajeshi anatumikia v
ccm??

Utopolo fc
 
Kule uganda mtoto wa waziri wa ulinzi aliuliwa kwa risasi baada ya uchafuzi mwaka huu
 
nawaza kimya kimya makomando wa jeshi waliofukuzwa kazi wanapoajiliwa na kiongozi mkuu wa upinzani siri za serikali zinakuwa salama? hatuna haja ya kujiuliza akina kigogo wanapata wapi taarifa
Kwa taarifa yako DW iliwahi kutangaza kuna waliokuwa wanajeshi wa Tanzania wameajiriwa Congo na waasi na wezi wa madini,wewe unaongelea kiongozi wa upinzani ambaye anaweza kuwa rais ajaye.
Tatizo hawaandaliwi vizuri wafanye nini utumishi wao jeshini ukikoma,kwani wengi wao wanjua kupigana tuu.
 
Mpaka sasa tunasema Too late!
 
Mungu ni mwema sana damu za watu itakua nyingi zimemwagika tena watumishi waliolitumikia Taifa lazima karma iwaumbue kweli karma inafanya kazi watoa kesi ndio wanaomba kesi ifutwe tena haina maana wanaumbuka...
Ifutwe wakati kuna maelezo ya mto kutoweka?
 
🤔
 
Watengeneza kesi hawakutafakari kabla walikurupuka kutengeneza kesi tu huko moses lijenje akifa kwa mateso baada ya kuamua kuwa kimya kwa kuwambia kuwa hajui ugaidi wowote kwani yeye na Lt Urio walimpa mbowe Asikari wasitaafu kwa nia ya kuwapa ajila mpya tu wapate ridhiki, hawakujua chochote zaidi ya hayo, kitendo cha kutuma MP na Asikari kwenda kuwatesa kuwalazimisha waseme ugaidi hewa, ugaidi ambao hawana haupo kilikuwa kitendo cha kinyama ni kinyume cha haki za binadamu, ikumbukwe kuwa kesi ya mbowe ilisukwa na magufuli kwa lengo la kuidhoofisha chadema lakini washauri wa magufuli kipindi kile akina Sabaya ndiyo wakabuni mbinu za hovyo za kuwabambikia kesi za ugaidi huku mahita kingai wakipiga sana kuwafunga pingu mikono miguu saa 24 ni unyama ulioje, hawakutarajia siri kuvuja mahakamani ampapo sasa vichwa vinawauma kwa uonevu waliotenda dhidi ya mbowe na walinzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…