Kuna wakili yule wa serikali anaonekana ni jeuri na mtu wa majungu sana, kuna maswali alikuwa akimuuliza Adamo akitaka kujua yale ambayo yanafanyika kule DRC, kuna wakati anachonokoa kutaka kufahamu ni kwa jinsi gani Makomando wanavyofanya kazi.
DPP aingilie kati kuepuka haya kutokea maana tunapoelekea huko siri nyingi zitawekwa wazi, pia itatengeneza uhasama kati ya majeshi haya wawili jeshi la polisi na jeshi la wanannchi.
Swali langu? Hadi huyo luteni Urio kuteswa huko ni kwamba Jenerali Mabeyo hana taarifa na kinachoendelea kwa vijana wake, inasikitisha sana.