Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi yaahirishwa. Kuendelea Jumatatu ya tarehe 27/09/2021

Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi yaahirishwa. Kuendelea Jumatatu ya tarehe 27/09/2021

Kuna mamburumundu ya kijani hapa:

View attachment 1950823

eti kwa kuwa tu na mikuyenge yenye kudhani kila mwanamke inayomwona ni kahaba.

Wakamwulize Sirro na waliobakia, japo ringekuwa rire jiwe renyewe ndiyo ingependeza zaidi.
mbowe.jpg
 
Nimesikitika kuona comandoo anakamatwa kizembe na raia mkakamavu(polisi), nilitegemea wangekinukisha vya kutosha mpaka waje special task kutoka kikosi cha makomandoo
naunga mkono hoja,
amenisikitisha sana. sifa zote zile tunazosikia za makomando sikutegemea hili.
 
Jaji ameingia.. Watu wanasimama, Kesi inatajwa, watu wanaketi..

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: anatambulisha Mawakili wa Jamhuri..

Adv. Kibatala: anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi..
Peter Kibatala
Jonathan Mndeme
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
John Mallya
Sisty Aloyce
Alex Masaba
Idd Msawanga
Gaston Garubindi
Evaresta Kisanga
Hadija Aron
Faraj Mangula
Maria Mushi
George Masoud
Michael Lugina
Nashon Nkungu

Kibatala: ni hayo tu Mheshimiwa Jaji na wengine wakifika tutaijulisha mahakama..

Jaji: nimeona mawakili wa utetezi wapo upande huu, Je mpo sawa?

Wakili wa Serikali: Tupo sawa

Wakili Peter Kibatala: Tupo sawa

Jaji: Wakili Kidando

Wakili wa serikali: shauri limekuja kwa ajili ya kusikiliza na mpaka sasa tumeshaleta mashahidi 3 kati ya 7, na tunaomba hairisho mpaka Jumatatu.. tunaomba kupata muda wa kupitia ushahidi uliowasilishwa.

Wakili wa serikali: tunaomba kuondoa mashahidi wengine waliobakia kwa dhumuni la kesi ndogo tubakie na hao hao watatu Wakili wa Serikali anakaa chini..

Jaji: kuna lolote upande wa utetezi? Jaji anaendelea kuandika..

Kibatala: Hakuna mheshimiwa Jaji..

Jaji anaendelea kuandika..

Jaji: Shauri hili dogo kwa upande wa Jamhuri limefungwa, Nitamsikiliza wakili John Mallya...

Wakili Mallya: Mshtakiwa wa pili atajitetea mwenyewe na mashahidi wengine watatu pamoja na yeye watakuwa jumla wanne

Jaji: Kuna kingine.?

Mallya: Mheshimiwa ni hayo

Jaji: Mpo tayari kuanza utetezi hata sasa? au Mngehitaji muda wa kujiandaa?

Mallya: tupo tayari

Jaji anaandika. Mahakama kimya, Nje mvua inapiga kidogo

Jaji: Shahidi wa kwanza wa shauri dogo la utetezi aje kwenye kizimba..

Shahidi: anaenda kizimbani anasindikizwa na askari Magereza

Jaji: tutajie majina yako kwa ukamilifu wako unaitwa nani..

Shahidi: Adam Kasekwa

Jaji: Kuna Jina limekuwa likitumika la Adamoo unalitambua??

Shahidi: nalitambua

Jaji: Dini yako Mkristo?

Shahidi: ndiyo

Jaji: Apa

Shahidi: Naapa mbele ya mahakama hii, yote nitakayosema yatakuwa kweli tupu, Eeh! Mwenyezi Mungu nisaidie..

Jaji: unaweza kutoa ushahidi wako ukiwa umesimama au umekaa, Wakili John Mallya unaweza kuendelea..

Mallya: Shahidi umetoka kuapa, unaweza kututambulisha ulipokuja mahakamani umetokea wapi?

Shahidi: nimetokea gereza la Segerea..

Mallya: Siku za nyuma ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa askari wa JWTZ kikosi namba 72 Sangasanga Morogoro

Mallya: ni Kikosi cha namna gani?

Shahidi: zamani kikosi cha Makomandoo siku hizi kinaitwa SPECIAL FORCE

Mallya: umehudumu kwa miaka gani?

Shahidi: Miaka sita kuanzia 2012 mpaka 2018

Mallya: Kipi kilikufanya uache kazi?

Shahidi: sikuacha bali niliachishwa na wakuu wangu

Jaji: sijui mnasikia maana naona kelele za mvua zinaingilia, KILA MTU ANAYO HAKI YA KUSIKILIZA HII KESI

Jaji: Jamani Mnasikia

Wote: tunasikiaaaaaa

Jaji: Kama mkiona hamsikii tunaweza ku' break kidogo, Hasa mawakili na washitakiwa muwe free tafadhali..

Shahidi: Mwaka 2016 mpaka 2017 nilikuwa kwenye misheni KONGO na Kurejea salama nchini kwangu na kuendelea na kazi.. wakuu wangu wakagundua kuwa nina tatizo la BATTLE CONFUSION

Mallya: Unaweza kumueleza, Jaji Battle Confusion inakuwaje?

Shahidi: siwezi kujijua sana lakini ni hali ya Askari anaposikia milio ya mizinga na risasi kwa wingi anakuwa hafanyi vile anavyotakiwa na wakubwa wake

Mallya: Kwenye Afya ana athiri mfumo gani?

Shahidi: mfumo wa akili..

Mallya: sasa umeshafukuzwa kazi baada ya Battle Confusion, Je ulikuwa unafanya shughuli gani?

Shahidi: nilikuwa nafanya biashara ya kununua maharage huko Morogoro sehemu inaitwa Nongwe na kuuza soko la Lubeho, kote Morogoro

Mallya: unamfahamu mshtakiwa namba 4?

Shahidi: simfahamu sana ila nilitakiwa nikafanye naye kazi ya VIP PROTECTION

Mallya: kazi ya VIP PROTECTION ni kazi unayoweza kuifanya?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: OBJECTION

Mallya: naondoa swali

Mallya ulifanya nini?

Shahidi: nilikuwa kwenye hatua ya mazungumzo ya kazi

Mallya: yalikuwa yanahusisha nini?

Shahidi: kuhusiana na majukumu ya kazi na malipo yetu

Mallya: ilikuwa lini?

Shahidi: Mwishoni wa mwezi wa 7 mwaka 2020

Mallya: Makubaliano ya kufanya kazi na mshtakiwa wa 4 mlikuwa mnafanya wapi?

Shahidi: mara ya kwanza tulifanya Moshi

Mallya: nakupeleka tarehe 05 Mwezi 08 mwaka 2020 kilitokea nini?

Shahidi: siku hiyo nikiwa na mshtakiwa mwenzangu namba 03 Mohammed Ling'wenya sehemu inaitwa maduka, tukavamiwa na watu kama watano, walinivamia mimi kwanza wakaanza kunipiga, mshtakiwa mwenzangu akaja kuniokoa..

Shahidi: alipofika akawauliza "Mbona mnapiga huyu mtu?".. wakamuuliza wewe unamfahamu huyu, akajibu ndiyo namfahamu.. wakachukua madawa na silaha, nikawasikia wakisema ana madawa.. wakati Mimi wakiendelea kunishambulia.....

Shahidi: Mshitakiwa mwenzangu akawawahi akitoa vitu mfukoni, nikasikia kwa maneno akisema huyu mmeshamuwekea madawa? akiwa anamaanisha mimi... mmemuweka madawa na silaha? Mimi natoa vitu vyangu kabisa msije mkaniweka na mimi, Wakati huo mimi wakiendelea kunishambulia..

Mallya: unaweza Kuwakumbuka watu hao ukiwa hapa Mahakamani.?

Shahidi: Mahakamani nimeshawaona watu 2

Jaji: Subiri kidogo, anaendelea kuandika..

Mallya: ni nani umewaona hapa mahakamani?

Shahidi: Ramadhani Kingai na Mahita ambao nimekuja kuwafahamu majina yao hapa mahakamani

Mallya: hawa watu wawili ambao umewataja walikuwa na majukumu gani?

Shahidi: nilikuwa nawatambua kwa sura na matendo yote ya kunipiga na kuniwekea Madawa na silaha..

Jaji: Ukisema kuwekewa madawa na silaha nini kilichotokea?

Shahidi: Wakati wananipiga na wamenibana, akaingiza mkono wake kwenye suruali akasema ana madawa na mwingine akaingiza kitu nyuma ya mkanda akatoa kitu akasema ana silaha

Mallya: hili eneo ambalo tukio limetokea lilikuwa ni eneo la wazi?

Shahidi: pana maduka ya kubadilisha pesa. M-pesa na tiGoPesa na Grocery pembeni

Mallya: Wewe ulikuwa sehemu gani?

Shahidi: nilikuwa katikati upande kulia maduka na upande wa kushoto Grocery..

Mallya: Ulikuwa umekwenda kufanya nini?

Shahidi: kuagiza chakula, Nilikuwa naandaliwa nyama ya kuchoma lakini hata kulipa bado

Mallya: nini kilifuata,?

Shahidi: baada ya mwenzangu kusema natoa vitu vyangu msije kuniwekea kama mlivyo muwekea huyu, wakatukamata na wakatufunga pingu na kutuingiza kwenye gari yao..

Mallya: baada ya kuingizwa kwenye gari waliwapeleka wapi?

Shahidi: Muda wote tulikuwa tunapigwa, hatukujua tunaelekea wapi, baadae wakatufikisha kituo cha polisi

Mallya: kituo gani?

Shahidi: nilikuaa sikijui, lakini baada ya kuongea mahakamani nimegundua ni Central Moshi

Mallya: Baada ya kupelekwa Central Moshi kitu gani kilifuata?

Shahidi: walinitoa pale ndani kituoni kuna chumba cha pembeni palikuwa na jopo la watu wengi wakanivua nguo zote, nikawa ninaning'inizwa kwenye kichuma fulani mithili ya MSHIKAKI au POPO

Mallya: wakakuning'iza kama Popo, kitu gani kilifuata?

Shahidi: wakianza kunipiga na kunitesa na muda wote wananiuliza swali "HUKU MOSHI UMEFUATA NINI" nikijibu kuwa huku Moshi nimekuja kufanya VIP PROTECTION kwa Mheshimiwa MBOWE,Hilo jibu hawalitaki wala haliingii akilini

Shahidi: nikiwa siwezi kusimama wakanitoa pingu wakanivalisha suruali na shati, wakaanza kunikokota

Jaji: umezungumzia kuvaa!

Shahidi: Ndiyo walinivalisha suruali. wakawa wananikokota kunipeleka mahabusu, baada ya kufika mahabusu wakanifunga pingu za mikono wakaniacha ndani

Mallya: jambo gani lilifuata?

Shahidi: ndani ya mahabusu kuna chumba kidogo cha mlango wa nondo wakawatoa watu mule wakanifungia mimi..

Mallya: ulijua hatima ya yule mtuhumiwa mwingine?

Shahidi: sikujua hatima yake

Mallya: nini kilifuata?

Shahidi: niliendelea kukaa ndani

Mallya: kuna ushahidi umetolewa kuwa mlizunguka maeneo mbalimbali Moshi na Hai

Shahidi: hapana sikutolewa kwenda popote

Shahidi: Ndani ya chumba kuna Askari alikuja kumwaga maji

Mallya: nini kiliendelea

Shahidi: kesho yake nilikuja kugundua ni kesho tayari baada ya kuona Jua

Shahidi: wakanitoa wakinilazimisha nitembee lakini nikawa nikawa siwezi.

Simu inaita kwa VIBRATION (mithili ya Philips)

Jaji: naomba kila Mtu aweke simu yake katika mazingira ambayo hayaathiri kazi yangu au ya shahidi, Msilazimishe niongee Jambo ambalo sitaki kuongea..

Jaji: Endelea baada ya kutolewa

Shahidi: wakaja watu wakanikokota na kunipandisha kwenye gari

Mallya: unaweza kukumbuka hao waliokuwa wanakukokota ni akina nani?

Shahidi: namtambua mmoja anaitwa Goodluck

Mallya: baada ya kukukokota na kukufunga Jacket usoni walikupeleka wapi?

Shahidi: sikujua naenda wapi, nilitambua tu nipo kwenye gari na ikaanza kutembea

Mallya: kitu gani kiliendelea?

Shahidi: nikiwa ndani ya gari kabla haijatoka kwa muda wa nusu saa, mateso yaliendelea kwa kunichoma choma na bisibisi

Shahidi: wakawa wananiambia "Leo ndiyo mwisho wa maisha yako, na kwamba hapa tulipo unamjua nani, nikajibu simjui Mtu, wakasema basi na wewe hakuna anayejua upo na nani".

Mallya: Endelea

Shahidi: nilikuwa nimelazwa kwenye floor ya gari, siyo kwenye siti..

Shahidi: baada ya safari ya muda mrefu sana, tukafika sehemu wakanishusha kwa kunikokota vievile na tulipofika kwenye kachumba wakanitoa Jacket wakaniuliza "Unajua upo wapi hapa?" nikawaambia "hapana sifahamu" wakafunga mlango nikiwa ndani nikiwa na pingu lakini Jacket wamenitoa

Mallya: unamkumbuka aliyekuwa anakuuliza hayo?

Shahidi: namkumbuka ni Goodluck

Mallya: Jambo gani lingine lilitokea kwenye kile chumba?

Shahidi: nikiwa na pingu nikajikokota kusogea mlangoni bahati nzuri nikaona watu wengine wamefungiwa kwenye chumba kingine kidogo mule

Shahidi: nikawauliza ni wapi hapa? Wakanijibu hapa ni TAZARA

Mallya: hao watu waliokwambia hapa upo TAZARA ulipata kuwafahamu au ulikuwa unawafahamu?

Shahidi: hapana nilikuwa siwafahamu

Mallya: nini kilifuata?

Shahidi: nilikaa pale tarehe 7, 8 na 9 na ilipofika tarehe 9 usiku wakaja kunichukua usiku.

Mallya: umesema umekamatwa Moshi tarehe 05 je kati ya tarehe 5 Mpaka tarehe 7 kuna nini kilitokea?

Shahidi: tarehe 05 - 7 nilikamatwa Moshi na kuteswa kisha nikasafirishwa kuja TAZARA

Shahidi: tarehe 09 wakanitoa usiku, siku hiyo angalau nilikuwa na uwezo wa kutembea, Lakini wakaniambia huku tunakoenda yanaenda kukuta yaleyale ya Moshi, sasa UJIANDAE

Mallya: Tarehe 09 nini KILIFUATIA?

Shahidi: Wakinitoa wakanipandisha kwemye gari, safari ikaanza..

Shahidi: haikuchukua muda kama Moshi. Siku hiyo sikuwekwa chini kama walivyonisafirisha kutoka Moshi. wakaniingiza kwenye chumba wakanifungua

Jaji: Subiri kidogo..

Jaji: unasema mlipofika wakakushusha?

Shahidi: walifikisha mpaka kwenye chumba, Kilipofunguliwa wakanitoa Jacket usoni, wakaniamuru niingie ndani

Jaji: Ndiyo

Mallya: rudi nyuma kidogo shahidi baada ya kuambiwa kuwa upo TAZARA, Ulifanya jambo lolote kuthibitisha upo TAZARA?

Shahidi: ilipofika jioni nilikuwa nasikia mlio wa honi ya TRENI,nikagundua nipo MAENEO yanayofanana na TAZARA

Mallya: sasa tayari upo sehemu nyingine umefumguliwa koti machoni

Shahidi: niligundua umeshaingia usiku, kesho yake usiku tena akaja Kingai na Goodluck wakanitoa ndani

Mallya: Taratibu Shahidi Jaji aandike

Shahidi: wakanipeleka Kwenye chumba kilichokuwa kina meza, Goodluck akawa mlangoni na Kingai akakaa mbele yangu tukawa tunatazamana

Jaji: NDIYO

Mallyaunazozungumzia ni zipi

Shahidi: pingu za chuma

Shahidi: Kingai akaniambia "mateso yanapopungua ujue kuna kuna mambo mazuri yamekaribia" m tunataka uwe mstaarabu, hapa kuna nyaraka tunakuja mnazo tunataka usaini..

Mallya: Mkono wa kushoto na pingu, wa kulia na kalamu, nini kilifuata!

Shahidi: akawa ananionyesha sehemu za kuandika kama "NATHIBITISHA" au KUSAINI

Mallya: Ulipata Kujua Kimeandikwa kitu gani ktk kile kingai anachokuoatia Kuthibitisha au Kusaini

Shahidi: Hapana

Mallya: Moshi umetuambia walikupiga, wakakulaza kwenye Floor sehemu yenye Joto kwenye gari, Je unauthibisho wowote unaoweza kuonyesha mahakamani?

Shahidi: naweza Kuthibitisha kwa kuonyesha sehemu nilizoumizwa, Makovu yanayoeleka kupona na mguu nimeumia leo siwezi kutembea vizuri

Jaji: kabla hajatuonyesha atueleze yapo sehemu gani, isije ikawa sehemu ambayo yanaweza kutweza utu wake

Mallya: Shahidi tueleze maeneo ya mwili ambayo umeumia

Shahidi: Mguu wangu wa kushoto na mkono wamgu wa kushoto

Jaji: sina tatizo na maeneo hayo, Wakili unaweza kuendelea

Mallya: unaweza kusimama kuonyesha mahakama?

Jaji: unaweza kusimama na mimi nitasogea kuweza kuona..

Jaji: hiyo ni mguuni (anaonyeshwa)

Jaji: sawasawa anarudi kukaa sehemu yake

Shahidi: anarudi sehemu yake pia Mahakama ipo kimyaaa!

Mallya: kuna wakati ulitaka kumueleza Jaji kuna vingine ulitaka kumueleza nini hivyo?

Shahidi: Takribani Mwaka 1 na mwezi sasa tangu niteswe na kuumizwa, sikuwahi kupelekwa hospitali kwa matibabu na mpaka sasa nahisi maumivu makali

Mallya: Je ulipata kutambua kuwa upo kituo gani cha polisi?

Shahidi: nilikuja kujua nipo kituo cha polisi MBWENI

Mallya: Ulijuaje kuwa upo Mbweni?

Shahidi: kuna askari polisi alikuwa zamu, alisema hamtakiwi kujua mpo wapi, lakini mpo kituo cha Polisi Mbweni

Mallya: Utofauti wa majina yako Mbweni ulijuaje?

Shahidi: siku ya kwanza nafika Mbweni nilifika pale Mlangoni nikakabidhiwa kikaratasi kuwa kuanzia siku hiyo naitwa VICENT JUMA na wakikikuuliza umekamatiwa wapi sema TABORA na useme kesi ya UNYANG'ANYI, ukiseme Majina yako tutajua

Mallya: baada ya kujua upo Mbweni nini kiliendelea?

Shahidi: niliendelea kukaa Mbweni muda wote mpaka siku nafikishwa mahakamani na muda wote sikufunguliwa pingu

Mallya: unakumbuka ilikuwa siku gani? Mahakama gani?

Shahidi: ilikuwa Tarehe 19 Mwezi 08 Mwaka 2020

Shahidi: Nilipofika mahakamani ndipo nilikutana na mshtakiwa mwenzangu ambaye tulikamatwa pamoja Moshi na mshtakiwa namba 1..

Jaji: Kama naelewa tangu mtoke Moshi hamkuwahi kuonana

Shahidi: ndiyo hatukuwahi kuonana kwa macho

Mallya: Je mliwahi kuwasiliana?

Shahidi: tukiwa TAZARA tuliwasiliana kwa sauti akitokea chumba kingine lakini hatuonani

Mallya: tarehe 05 RAU Madukani, Moshi ukisema wamekuwekea vitu, Je wewe Binafsi ulikuwa na nini mfukoni?

Shahidi: nilikuwa na pesa Laki 2 na 60 taslimu, simu ya Itel na line ya Halotel

Mallya: hivyo vitu vipo wapi?

Shahidi: tangu wavichukue sijavipata

Mallya: nani alichukua.+?

Shahidi: alichukua mfukoni Goodluck akampatia Kingai

Jaji: Shahidi bado unayo maji mkononi, Kama utahitaji break utasema maana kuulizwa maswali kunatumia sana akili na kuchosha mwili

Shahidi: Asante Mheshimiwa Jaji

Mallya: ukiondoa Kingai na Goodluck kuna mtu mwingine unamkumbuka alikuja Mbweni?

Shahidi: nilimuona Mahita

Mallya: alikuja kufanyeje?

Shahidi: nilimuona wakati wanakuja kuniona, Lakini hakuhusika kuingia katika kile chumba

Jaji: chumba kipi?

Shahidi: chumba kile ambacho kilikuwa na Meza mbili na Kingai

Jaji: nimekuelewa

Mallya: Umesikia wakitoa ushahidi hapa,kwamba walikuwa wanawapa matunzo mazuri na walikuwa wanatunza utu wenu

Shahidi: si kweli

Mallya: walisema waliharibikiwa gari Himo je unasemaje kuhusu hilo?

Shahidi: kwangu ni ngumu kuhusu kuelezea kwa sababu tulikuwa tunasimama sehemu nyingi lakini nilikuwa nimefungwa usoni nisione kitu

Mallya: je unakumbuka tangu tarehe 05 mpaka Kingai anakuletea maelezo yako usaini zilikuwa zimepita siku ngapi

Shahidi: Siku 06

Mallya: Kwa sasa sina la zaidi Mheshimiwa Jaji

Jaji: Wakili Malya unafikiri Shahidi wako anaweza Kuendelea.?

Mallya: it depends

Jaji: nimekupa wewe kuamua nilikuwa naweza kuendelea bila kukuuliza

Mallya: Anaweza kuendelea Mheshimiwa Anaingia wakili Nashon Nkungu

Nashoni: Je ni kweli baada ya kupata Battle Confusion hukupatiwa matibabu?

Shahidi: hapana nilipatiwa kwa maana nilipelekwa hospitali ya Lugalo

Nashoni: kwenye maelezo watu hawa walikwambia sisi hautufahamu na wewe hutufahamu ni sahihi?

Shahidi: ni sahihi.

Nashoni: Ulipata hisia gani kuwa na watu hao?

Shahidi: wasiwasi nikaona roho yangu ipo mkononi

Wakili wa Serikali: MHESHIMIWA JAJI HISIA NI KITU GANI

Jaji: hilo linamuhusu mwenyewe, kuhusu hisia zake, haliwezi kuathiri Jambo lolote

Jaji: rudia hisia ulisikiaje hisia zako

Shahidi: niliogopa kwamba naweza kuteswa sana

Nashon: umeeleza kuwa ulikuwa unachomwa BISIBISI, Je ni maeneo gani sasa?

Shahidi: Maeneo ya MBAVU na MATAKONI

Nashon: Ukisafirishwa kutoka ulipokamatwa Moshi kuja Dar es salaam, TAZARA..

Shahidi: baada ya siku MOJA

Nashon: Uliambiwa kuwa mnaanza safari ya kuja Dar es salaam au popote.?

Shahidi: Hapana sikuambiwa

Nashon: unaweza kujua kwanini hamkuanza safari ya kuja Dar es salaam baada tu ya kukamatwa?

Shahidi: Hapana

Nashon: Unakumbuka kuwa mlifika Arusha baada ya kukamatwa?

Shahidi: Sikumbuki na wala halikwepo jambo hilo

Nashon: unasema ulikuwa na Pesa,260,000/= unakumbuka kuandikiwa risiti ya pesa hizo?

Shahidi: Hapana

Nashon: Mheshimiwa Jaji yangu ni hayo tu

Jaji: Wakili Fred na Matata mtauliza maswali wote 2 au 1 kwa niaba ya mshtakiwa wa 3?

Wakili Fred Kihwelo: Kwa niaba ya mshtakiwa wa tatu hatutokuwa na maswali yoyote

Jaji: Kibatala kwa niaba ya mshtakiwa wa nne

Wakili Kibatala: nataka utuambie kwa vitendo Ulikabwaje pale RAU MADUKANI..

Shahidi: nilikuwa naongea na simu nikiwa nimevaa Jacket naongea na simu, akatokea mtu kwa nyuma akashika mkono wenye simu na Jacket wakati najitetea akatokea kwa mbele mwingine, Mwingine akatokea akanishika mkanda hapa kiunoni..

Kibatala: unaweza kutonyesha?

Shahidi: bahati nzuri suruali niliyovaa siku ile nakamatwa ndiyo niliyovaa leo, haina hata RUSKI

Kibatala: naweza KUONA?

Shahidi: Ndiyo unaweza kusogea

Kibatala: sawa lakini pia mahakama inataka kuona

Kibatala: Wakati wanakukamata hapo ikawaje

Shahidi: akatokea mtu mbele akanipiga ngumi

Kibatala: unamkumbuka?

Shahidi: ndiyo alikuwa dereva wa gari tuliyopanda

Kibatala: Kingai alikwepo eneo la tukio.+?

Shahidi: ndiyo

Kibatala: alikuwa anafanya nini?

Shahidi: yeye ndiyo ALICHUKUA PESA ZANGU BAADA YA kusachiwa

Kibatala: Afande anayeitwa Mahita alikwepo wakati unakamwata.l?

Shahidi: alikwepo na yeye ndiye alikuwa wa kwanza kunikaba wakati naongea na simu

Kibatala: uliwezaje kuona tukio hilo la kukabwa?

Shahidi: niliona kwa sababu ilikuwa mchana na nilikuwa na akili timamu

Kibatala: Wakati wanafika kukukamata waliijitambulisha kwa mujibu wa PGO na sheria.l?

Shahidi: Hapana hawakufanya hilo..

Kibatala: na ni kweli kwamba wakati wanakukamata hawakuwa wameshika Ki' Notebook?

Wakili wa Serikali: MHESHIMIWA OBJECTION anachokifanya Wakili Msomi siyo kinacholekezwa kwa mujibu wa TRIAL WITHIN a TRIAL pamoja kwamba haijasema UKOMO wa maswali.. Matters ambazo ni Mpya zitaipotezea Muda Mahakama

JAJI: Wakili Kibatala..

Kibatala: Kwa heshima na taadhima wakili Msomi mwenzangu HANA HOJA, Shahidi analindwa na Jaji kama ningemuuliza SWALI ambalo lingemdhalilisha ningezuiwa, sijui anamaanisha nini?

Jaji: tuendeleee Shahidi ni wa Utetezi siyo wa mashtaka ,Labda iwe kwa maswali yanayo dhalilisha

Jaji: Tuendeleeeeeeeee

Kibatala: uliwahi kuona mtu ameshika NOTEBOOK wakati wa zoezi kukukaba na kukukamata linaendelea?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: wakati unakamatwa ni eneo la wazi bila shaka watu wengi walishuhudia wakati wa Kukamatwa kwako

Shahidi: ndiyo walikuwa wengi

Kibatala: je uliona wakati wowote Kingai anaita watu washuhudie kukamatwa kwako?

Shahidi: Hapana

Kibatala: uliona hapa mahakamani kitabu chochote ambacho mahakamani kimeletwa kinaeleza ni aina gani ya silaha ulikamatwa nayo Moshi?

Shahidi: hapana

JAJI: wakili naomba tu' break ni takribani masaa mawili sasa, na tutaendelea saa 7 kamili mchana.. natoa Break ya nusu saa kisha tutarejea kuendelea...

Jaji ananyanyuka anatoka

Tunasimama..

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------


Jaji ameingia.. Kesi inatajwa..

Mafaili yanapelekwa kwa jaji

Jaji: Wakili wa Serikali kuna mabadiliko yoyote?

Wakili wa Serikali: Hapana

Jaji: Kuna mabadiliko yoyote upande wa utetezi?

Kibatala: Hapana Mheshimiwa

Jaji: Nakuita sasa shahidi na kukumbusha upo chini ya kiapo

Kibatala: kwa Kumbukumbu zako kuna shahidi yoyote aliwahi kuwasilisha hapa mahakamani kwamba bastola imeingia kama sehemu ya ushahidi?

Shahidi: Hapana sijaona..

Kibatala: umesikia mashahidi wa serikali wamesema walipokuchukua Moshi kwamba waliwachukua kwenda kumtafuta Moses Lijenje kwa sababu ya upelelezi?

Shahidi: Hapana sijaona

Kibatala: kuna nyaraka yoyote imetolewa ushahidi wa upande wa mashitaka kwamba kuna nyaraka inaonyesha gari iliharibika na kutengenezwa

Shahidi: Hapana

Kibatala: ushawahi kuona shahidi kutoka Moshi Central Polisi Station Moshi kuwa uliingia na kutoka mara kadhaa ukiwa kituoni

Shahidi: Hapana sijamuona

Kibatala: Umemuona Shahidi ambaye ni dereva ambaye gari lake liliharibika Himo na ndiye aliyewaendesha kutoka sehemu mbalimbali

Shahidi: Hapana

Kibatala: Umemuona RPC ambaye baada ya gari kuharibika ndiye alitoa gari yake kuwaleta DSM kuthibitisha hilo

Kibatala: Ulimsikia Jumanne ndiyo alikupekua Moshi, uliwahi kumuona Jumanne mahakamani kama shahidi muhimu?

Shahidi: Hapana

Kibatala: ulimsikia shahidi kutoka central Police Station DSM kuwa alikabidhiwa watuhumiwa ikiwemo wewe kutoka kwa Jumanne, je Jumanne umemuona Mahakamani

Shahidi: hapana sijamuona

Kibatala: Ushawahi kumuona mahakamani dereva wa RPC ambaye aliwachukua na gari yake kutoka Himo — Dar.?

SShahidiahidi: Sijamuona

Kibatala: hapa Mahakamani ulishawahi kuona kithibitisho chochote kinacho onyesha gari ya RPC imeruhusiwa kutoka Moshi - DSM?

Shahidi: Hapana sijaona

Kibatala: kwanza kwa uelewa wako wewe ulitekwa au ulikamatwa?

Shahidi: nilitekwa

Kibatala: Je Ulishawahi kusikia hapa Mahakamani Kingai au wenzie wanazungumzia kuhusu pesa zako?

Shahidi: Hapana

Kibatala: umesikia Mashahidi wa serikali wanasema waliwakamata mkiwa mnakula?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Utakubaliana na mimi kama mlienda kula bila shaka ulikuwa na pesa, Je umesikia hapa mahakamani wamezungumzia kuhusu Pesa ulizokuwa unataka kununulia chakula?

Shahidi: Hapana

Shahidi: Hapana

Kibatala: wakati unatoka RAU Madukani kwenda Central Police station Moshi ulifungwa kitambaa usoni?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwa hiyo ulifungwa kitambaa machoni wakati wa kutoka Moshi kwenda Dar es salaam na wakati kutoka TAZARA kwenda Mbweni?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ulisema ulipokuwa kituoni TAZARA ulipafahamu kwa kusikia honi ya treni?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: nini kingine kilikufanya utambue kuwa upo TAZARA

Shahidi: kwa sababu niliuliza MAHABAUSU wenzangu

Kibatala: unawakumbuka hao Mahabusu?

Shahidi: ndiyo nakumbuka mmoja alikuwa anavaa kanzu mrefu kama msomali, na mwingine alikuwa mwanajeshi kutoka kambi ya TWALIPO na wote walikuwa na MASHTAKA ya UGAIDI pia

Kibatala: Je kwa kesi hii hii.+?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Umesikia shahidi wa serikali amesema rumande aliwaletea uji ilikuwa shimoni, Je rumande ya TAZARA ipo shimoni

Shahidi: Hapana haipo Shimoni

Kibatala: je mlipokuwa TAZARA walikuja maafisa wawili wa JWTZ je unawafahamu

Shahidi: Siwafahamu kwa majina ila nawakumbuka kwa sura kwa sababu nilifanya nao kazi kikosi cha 92KJ

Kibatala: je unafahamu walikuwa wanahusika na nini pamoja na kina Kingai

Shahidi: sifahamu

Kibatala: wakati unakwenda Mbweni ulijua kuwa unaenda kwenye MATESO?

Shahidi: Ndiyo ni sahihi.

Kibatala: ni kweli au si kweli kwa askari aliyekwambia hapa upo Mbweni ingawa hukutakiwa kujua upo wapi, alionyesha utu na kwamba unaonewa?

Shahidi: Ni sahihi Kabisa

Kibatala: Ni sahihi wakati unahojiwa, Afande kingai anakulazimisha usaini maelezo na kupelekea kesi ndogo katika kesi kubwa, Kule Mbweni, muelezee Mheshimiwa Jaji, Goodluck alipokuwa mlangoni alikuwa ameshika bastola?

Shahidi: Sahihi kabisa

Wakili wa Serikali: OBJECTION. Sheria ya ushahidi kifungu 146(1) na (2) kwamba Cross Examination inafanywa na upande wa pili, kwa madhumuni kama haya tunakubaliana, ila madhumuni yake ni kwamba anayefanya mahojiano (Cross examination) awe kwa ushahidi ambao umesemwa,Lakini Cross examination inatumika kuingiza ushahidi mpya.. tena kwa Leading questions ambapo shahidi kazi yake hapa anasema hapa ni kweli, sijui hapa Mheshimiwa tunaipeleka mahakama wapi, imekuwa ni Practice sana.

Jaji: kufupisha muda, unaelewa nini kuhusiana na ADVERSE PARTY?

Wakili wa Serikali: najua mahakama ndiyo ina haki ya ku' Control Cross examination ila tuliruhusu hili sisi tutakosa nafasi ya Kuhoji, Tulitegemea wenzetu wangeuliza kwa kielelezo ambacho wamekigusa wao

Jaji: Kuna kingine?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni kweli Cross examination haina mipaka, Lakini sheria imeaininisha masuala yapi yataulizwa kwenye Cross examination.. Sheria ya ushahidi kifungu namba 151 (6) a,b,c

Jaji: kwa tafsiri yako je?

Wakili wa Serikali: Maana yake ni kwamba anaweza shahidi akaulizwa maswali, lakini maswali hayo lazima yajikite katika mambo yafuatayo kutikisa ushahidi yaelekezwe katika kuvumbua ni nani na nafasi yake katika maisha ni Ipi, yaende katika kutikisa uadilifu wake na uadilifu wake kwa tabia zake kwa mujibu wa kifungu cha 155 Ya Sheria ya ushahidi Maswali ya ulimuona Goodluck alishika bastola hatufanyi kujua yeye ni nani... tukiruhusu tutakuwa tunakiuka sheria, Mahakama ielekeze katika kuhoji shahidi

Jaji: umesoma 155 na ngapi?

Wakili wa Serikali: 155 yenyewe tu ila ina a,b na c

Wakili wa Serikali: kabla, hujaamua tunaomba turejee kifungu cha sheria ya Ushahidi 146 mahakama inayoamua kipi kiiingie katika Ushahidi, anachokiuliza Kibatala hakitakiwi kuingia kwenye ushahidi

Wakili wa Serikali: Swali alililouliza Kibatala "upo Mbweni lakini hutakiwi kujua kama hapa upo wapi" na kauliza swali linalofuata kuwa "Je alikuonea huruma" Je swala hilo linaweza kuthibitishwa? Kifungu kidogo cha( 3) Mahakama ndipo ushahidi huo unaweza kupokelewa

Jaji: NDIYO

Wakili wa Serikali: inaenda kwa maswali aliyokuwa anam' lead shahidi kuwa Je ushahidi uliletwa au haukuletwa,Je ukiwa haukuletwa wataweza kuleta?

Jaji: Kibatala, unaweza kujibu?

Kibatala: Wenzangu Wamechanganya Dhumuni la Ushahidi. wamechanganya Kujua nafasi yao katika kesi hii

Kibatala: Wamechanganya kujua mimi na Mallya ni akina nani.. Sisi sote ni adverse Party tupo upande mmoja na ndiyo maana tulitengana.. Kwa hiyo sisi interest zetu ni adverse party Niende kwa Kifungu cha 155 Shahidi anapohojiwa maswali ya dodoso anaweza, ukiongezea maswali yoyote

Kibatala: Kifungu 152 maswali ya kumuongoza shahidi yanaruhusiwa wakati wa kufanya Dodoso, hakuna mipaka. kwa sababu wa leading huenda kuna mitego, unapouliza maswali ya dodoso unaruhusiwa kuuliza maswali yanayomtega, kwa hiyo kifungu 155 wenzetu wamekisoma visivyo

Kibatala: Hapa tuna discuss mchakato wa kielelezo siyo kielelezo, shahidi yupo Free na hawa siyo Mawakili wa mshtakiwa kwamba mshtakiwa amelalamika nimemtesa na maswali, na mwisho Mallya mwenyewe mteja wake hajalalamila kuwa namtesa shahidi wake..

Kibatala: halafu kuhusu Goodluck aliongea Mallya wakati wa kuhoji ushahidi wake hawakuhoji, sasa ikipita imeshapita.. Kuhusu Relevance nimemuuliza kitu kilichoingia kwenye ushahidi wa kwanza Kuhusu kumuita huyo Goodluck mimi naweza kumuita kwa kupitia mshtakiwa wa nne

Kibatala: walitakiwa kumzuia Mallya kuhusu kumuongelea Goodluck, ilishapita imepita. Ujumla Mh Jaji yalipo ni maoni binafsi ya mawakili wenzetu siyo maoni ya sheria, Hatuwezi kufunika haki kwa sababu upande fulani unakereketwa, katazo au ruhusa lazima lipimwe katika vigezo hivyo

Jaji: Kama nilivyosema wiki iliyopita, Jambo hili linahusu ushahidi gani upokelewe au ushahidi gani usipokelewe, kwa hiyo najipa tena dakika chache kabla sijaamua.. kwa hiyo nita' break na kuamua..

Jaji ananyanyuka anatoka mahakamani..

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kibatala ni balaa lingine, uzuri ni kwamba watetezi wapo imara ... Swali la kuongezea kwanini bastola aliyokamatwa nayo isipelekwe mahakamani itambulike ilikua ya nani kuna shida sana, pia wakali wa serikali kufanya objection kwa kibatala kuingizwa kwa mambo mapya amwpotoka maana mallya alivyomuingiza Goodluck hawakuhoji huku mbeleni kibatala anachimbua habikishi wakaona sasa ushahidi unakuja kujitisheleza safi sana hii battle nimeipenda
 
Haya maelezo ya shahidi ni ya maumivu sana Mungu tu ndiyo alizidi kumpa pumzi, kwa kweli kuna watu ni watesaji na dhuluma ya haki, ila Mungu mwisho wa hii kesi ataweka watu wazi na uchafu wao
Mkuu hivi komandoo anaweza kushikwa kijinga namna hii kweli
 
Huyu ni miongoni mwa Mabalozi ambao Mahudhurio yake kwenye Kesi ya UGAIDI wa laki 6 inayomkabili Mbowe na wenzake watatu haijawahi kutetereka , Ni huyo mwenye gauni zuri la bluu

Huyu_Mwanamama_huyu_Mwenye_nguo_ya_Blue_Ndiye_yule_alimempeleka_Tundu_Lissu__Airport_kwa_kutum...jpg


Ndiye anayetajwa kunusuru Uhai wa Tundu Lissu kwa kumpatia Kinga ya Ubalozi na kumsindikiza hadi Airport na kuhakikisha anapanda ndege kurudi Belgium , baada ya Spana za Kampeni za Ulioitwa uchaguzi Mkuu wa 2020 kuwachanganya akili watawala .

JamiiForums1604145819.jpg
 
Huyu ni miongoni mwa Mabalozi ambao Mahudhurio yake kwenye Kesi ya UGAIDI wa laki 6 inayomkabili Mbowe na wenzake watatu haijawahi kutetereka , Ni huyo mwenye gauni zuri la bluu

View attachment 1950858

Ndiye anayetajwa kunusuru Uhai wa Tundu Lissu kwa kumpatia Kinga ya Ubalozi na kumsindikiza hadi Airport na kuhakikisha anapanda ndege kurudi Belgium , baada ya Spana za Kampeni za Ulioitwa uchaguzi Mkuu wa 2020 kuwachanganya akili watawala .

View attachment 1950867
Kwani hujui nini kuhusu sistership ya Chadema na Chama cha CDU cha Ujerumani? Ni sawa na kutuletea habari kuwa ndugu yake Mbowe anakuja mahakamani kila siku!
 
Back
Top Bottom