Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mkuu, kwanini wamwambia mwenzako hivyo?huna akili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, kwanini wamwambia mwenzako hivyo?huna akili
suirini kesi iishe. pia, mimi sipo mahakamani, hivi ni kwamba zile meseji alikuwa anasoma Urio, zipo kwenye print out ya mtandao wa simu? kumbwe ni kweli mbowe alikuwa anawasiliana na hao watu....basi mbowe ana cha kujibu kwa watanzania. na ndiye anayewatesa hao vijana.Jana nilikuwepo Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuendelea kufuatilia kesi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu. Leo sikuweza kwenda kwakuwa ninatarajia kusafiri hivi punde. Nimemsikia na kumuona Luteni Denis Urio akitoa ushahidi wake. Nimemsikiliza kwa makini na kwa kutaka kumuelewa. Ameeleza mengi kumhusu Mbowe na wenzake watatu walio mahakamani na mmoja ambaye hayuko mahakamani: Komando Lijenje.
Luteni Denis Urio, akitajwa na ACP Kingai na wengine, ndiye kiini cha kesi ya Mbowe. Ndiye mtoa-taarifa wa kwanza kuhusu njama za kutenda makosa ya jina: ugaidi na kudhuru viongozi wa kiserikali. Luteni Urio ndiye anayedai kupeleka taarifa za uhalifu wa kijinai kwa DCI na hata mengine kufuata baada ya hapo. Leo anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani. Mimi siusubiri ushahidi wa leo. Wa jana unanitosha na kunitisha.
Luteni Urio amepasua jipu namna alivyowatafuta na kuwapata makomandoo wanne:Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Lijenje. Kila mmoja alikuwa kwenye harakati zake za kimaisha. Harakati halali zisizo na dalali. Alikuwa kipambana kivyake ili kujikimu na kutunza familia yake. Huyu huku, huyu kule. Hii ni baada ya kuwakuta kilichowakuta jeshini (ukweli wanaujua wao wenyewe na Mungu wao).
Wakatafutwa. Wakataarifiwa kuwa kuna kazi ya ulinzi. Wakashawishiwa kuikubali. Wakakubali. Wakapewa na pesa ya kusafiria na kujikimu. Wakaenda mahali pa kupata kazi. Waliambiwa waseme kinachoendelea huko na wakawa wanasema ( mmoja alikuwepo Dar na akasema kinachoendelea). Kama vijana wenye nguvu na maarifa, waliambiwa kuhusu kazi. Wakaitamani na kuikubali kwakuwa kwao ulinzi ni jambo la kawaida. Wakaenda.
Walipokuwa huko walipoambiwa waende, wakavamiwa na kukamatwa kwa kutaka kutenda ugaidi na kudhuru viongozi. La haula! Hayo yalitokea wapi tena? Je, Luteni Denis Urio aliwatengenezea wenzake kesi labda kwa visasi vyao binafsi wakiwa jeshini? Je, iweje waliotafutwa na kuambiwa waende walikokwenda kwa kazi ya ulinzi waende halafu wakakamatwe hukohuko walikoambiwa waende? Hawa makomandoo watatu waliopo mahakamani na ambaye anatafutwa 'hawana kosa lolote'.
Nani angeacha kuifuata ajira ikiwa ana nguvu, maarifa, ujuzi na shida ya ajira husika? Wasibagazwe kwa harakati zao za kimaisha.
Wasiojulikana sasa wamejulikana!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
Unaweza kukuta Urio na Mbowe wana jambo lao.
Ogopa sana Machame.....Ole imekula kwake!
mtu mbaya kabisa hapa ni mbowe ndiyo amewasababishia shida makomandoo unafikiri bila hao makomandoo kuja kwenda kwa mbowe dhamira ovu ya mbowe isingejulikana na walikamatwa mapema ili mbowe asije akatenda uovu wake
hata hao makomandoo wenyewe pia wana matatizo, wanajua kabisa kwamba hiyo kazi waliyopewa si halali kwanini walikubali kuifanya wakati walishaonywa na Urio kwamba wale walishakua na kiapo kwaiyo kama kazi itakuwa ni ya uhalifu waachane nayo?
Kwa akili za aina hii, wacha tu ccm iendelee kutawala.Baada ya kuona amekuwa mwenyekiti wa kudumu Mboe aliamua kukigeuza chama kama kampuni yake binafsi na kuanza kukitumia chama kama kichaka cha kupanga mipango ya kihalifu dhidi ya Serikli/nchi.
tulimshauri mara kadhaa ang'atuke lkn aliye diriki kugombea nafasi hiyo aligeuka kuwa adui wake!! kumbe alikuwa na agenda za kimafia dhidi ya serikali.
sasa yamemkuta.
Shida ni kwamba huo ubaya wa Mbowe bado mpaka sasa haujajulikana ni mbaya wapi na kwa lipi. Mimi ninataka nijiridhishe na mbele ya Mungu niweze kusema "ni kweli Mbowe ana hatia au hana hatia" na nitafanya hivi baada ya kupitia ushahidi unaotolewa dhidi yake. Mpaka sasa sijaona.mtu mbaya kabisa hapa ni mbowe ndiyo amewasababishia shida makomandoo unafikiri bila hao makomandoo kuja kwenda kwa mbowe dhamira ovu ya mbowe isingejulikana na walikamatwa mapema ili mbowe asije akatenda uovu wake
subirini hadi kesi iishe ndio mkoment. mashahidi bado wanaletwa. its too premature for us to comment kwenye hii kesi.Shida ni kwamba huo ubaya wa Mbowe bado mpaka sasa haujajulikana ni mbaya wapi na kwa lipi. Mimi ninataka nijiridhishe na mbele ya Mungu niweze kusema "ni kweli Mbowe ana hatia au hana hatia" na nitafanya hivi baada ya kupitia ushahidi unaotolewa dhidi yake. Mpaka sasa sijaona.
Mpumbavu mkubwa mmoja eti naye ametoa mawazo.mtu mbaya kabisa hapa ni mbowe ndiyo amewasababishia shida makomandoo unafikiri bila hao makomandoo kuja kwenda kwa mbowe dhamira ovu ya mbowe isingejulikana na walikamatwa mapema ili mbowe asije akatenda uovu wake
Na ndicho nilichosema. Soma nilichoandika: "Shida ni kwamba huo ubaya wa Mbowe bado mpaka sasa haujajulikana ni mbaya wapi na kwa lipi. Mimi ninataka nijiridhishe na mbele ya Mungu niweze kusema 'ni kweli Mbowe ana hatia au hana hatia' na nitafanya hivi baada ya kupitia ushahidi unaotolewa dhidi yake. Mpaka sasa sijaona."subirini hadi kesi iishe ndio mkoment. mashahidi bado wanaletwa. its too premature for us to comment kwenye hii kesi.
urio tokea mwanzo kwa maelezo yake alijua ni kazi ya uhalifu kwa nini aliwaingiza wenzake kwenye mkenge huo?hata hao makomandoo wenyewe pia wana matatizo, wanajua kabisa kwamba hiyo kazi waliyopewa si halali kwanini walikubali kuifanya wakati walishaonywa na Urio kwamba wale walishakua na kiapo kwaiyo kama kazi itakuwa ni ya uhalifu waachane nayo?
Swali mujarabu sanaurio tokea mwanzo kwa maelezo yake alijua ni kazi ya uhalifu kwa nini aliwaingiza wenzake kwenye mkenge huo?
Waliambiwa watafanya kazi ya ulinzi.. Kazi ya ulinzi siyo halali?hata hao makomandoo wenyewe pia wana matatizo, wanajua kabisa kwamba hiyo kazi waliyopewa si halali kwanini walikubali kuifanya wakati walishaonywa na Urio kwamba wale walishakua na kiapo kwaiyo kama kazi itakuwa ni ya uhalifu waachane nayo?