Hatuingilii mwenendo wa Mahakama lakini kuna mambo yapo dhahiri ambayo, laiti kama Jaji angekuwa makini, Mawakili wa Serikali wasingekuwa wanaichezea Mahakama kama wanavyofanya.
Mathalani, leo mawakili wa Serikali wanasema eti shahidi hawezi kuendelea na kuhojiwa kwa sababu ameshauriwa na daktari kupumzika kwa siku mbili. Tuamini kuwa habari hii ya kutengenezwa ni ya kweli.
Halafu wanasema, hata kesho hawawezi kuleta shahidi mwingine kwa sababu wanaweza wasimpate. Mambo ya kujiuliza:
1) Kama shahidi asingeugua jana, huenda Kibatala angemaliza cross examination jana, na leo serikali ingetakiwa kuwa na shahidi mwingine. Kwa maelezo ya hawa mawakili wa serikali kuwa hawana shahidi ambaye yupo tayari kuja kesho kutoa ushahidi wake, ina maana hata kama Kibatala angemaliza cross examination jana, leo wasingeleta shahidi mwingine? Au walifahamu toka mwanzo kuwa shahidi angeugua jana?
2) Baada ya shahidi kuugua jana, na kisha kwenda hospitali, ilitegemewa leo angekuja mahakamani. Na kama angekuja mahakamani, basi Kibatala huenda angemaliza cross examination yake leo, na kesho serikali ingehitajika kuleta shahidi mwingine. Hawa mawakili wa serikali wanaosema hawana shahidi wa kumleta kesho ili kesi iendelee, ina maana hata kama Kibatala angemaliza cross examination leo, kesho wasingeweza kumleta shahidi mwingine?
Au walijua toka jana au juzi kuwa shahidi angeugua jana, leo angeambiwa na daktari apumzike kwa siku 2, na hivyo cross examination isingemalizika leo, na hivyo kutokuwepo umuhimu wa kuandaa shahidi mwingine?
Polisi na Mawakili wa Serikali wasiichezee mahakama na wasiwafanye watanzania wote ni wajinga. Wafahamu kuwa huku nje ya polisi na nje ya Serikali, kuna watu wana akili na weledi hata wa kuwazidi wao maradufu.