Kesi ya Mbowe: Tathmini na Mwenendo

Kesi ya Mbowe: Tathmini na Mwenendo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Clip inawaonesha washitakiwa mahakamani buheri wa afya na nyuso za bashasha:

Haiyumkiniki faulo zote ni dhahiri zaidi kwao kama watendwa. Yawezekana psychologically wako set wanajua nini watesi wao wamepanga.

Mashahidi Kingai, Anita, Mahita na sasa Jumanne wote wanaongelea ukamataji tu. Hakuna jipya zaidi ya kuwa kila mmoja ana sarakasi zake tofauti na za mwenzake.

Zaidi sana inaonekana ukamataji huu ilikuwa ni operation iliyo ratibiwa na Kingai kuwakamata ambao wangalikuja kuwa walinzi wa Mh. Mbowe.

Hii yumkini ndiyo sababu Kingai alikuwa na taarifa kamili kuwahusu washitakiwa walivyokuwa kwa wajihi wao, mavazi yao, saa ngapi na wapi pa kuwapata.

Mbaya zaidi haupo muunganiko wa kuonyesha Moses Lijenje alitoweka vipi kwani hakujawahi kutolewa tangazo lolote hadharani lenye kuitisha hata usaidizi wa raia wema kwenye juhudi za kumpata.

Wasiri wa bwana Kingai wanaendelea kuwa wasiri hata leo.

Makosa ya msingi kwenye kesi nzito hii yanapewa majina mapya - curable mistakes.

Kuhudhuria kesi imekuwa "in one's own risks":

Mara watu wakamatwe, wazuiwe kuingia mahakamani, wasukwe sukwe, wafungiwe ndani ya mahakama, wazuiwe kuingia na simu nk. Imekuwa ni vurugu mechi.

Sintofahamu yoyote ya msingi bila kujali facts, inaamuliwa in favor ya upande wa mashtaka.

Miito inayoitishwa kumtaka Mh. Mbowe kuwaondosha mawakili wake haiji kutokea kusiko kuwapo.

Kwa kweli mhimili huu uko majaribuni na kama hautaamka sasa na kuirekebisha hali hii kuna hatari ya kupoteza kuaminiwa kwake.

Ieleweke hayupo anayepinga kwa Mheshimiwa Mbowe kuadhibiwa kama ushahidi wa wazi na haki upo kuthibitisha hilo.

Vivyo hivyo ieleweke haikubaliki kumwadhibu Mh. Mbowe au washitakiwa wenziwe kwa ghiliba, hadaa au uonevu.
 
Andiko lako nimesoma mstari wa kwanza to nikaachana nalo. Huwezi kufanya tathmini ya kitu chochote kwa kubase upande mmoja. Hiyo siyo tathmni bali ni mtazamo wako.
 
Andiko lako nimesoma mstari wa kwanza to nikaachana nalo. Huwezi kufanya tathmini ya kitu chochote kwa kubase upande mmoja. Hiyo siyo tathmni bali ni mtazamo wako.

Mstari wa kwanza ni huu:

"Clip inawaonesha washitakiwa mahakamani buheri wa afya na nyuso za bashasha."

Haiyumkiniki umesoma uzi mwingine siyo huu.
 
mi mwenyewe comment yako nimesoma nusu mstari nimebaini wewe hujasoma mstari wa kwanza kama unavyodai

Huyo mburumundu ni huyu hapa:

IMG_20211108_230214_612.jpg

Kutokea kwenye uzi huu:

Kumbe Freeman Mbowe hakuwahi hata kumiliki namba ya simu ya Tigo

Ana hasira kali. Yumkini ni Kingai au binamu zake. Yaani wale wachawi wenyewe!

Cc: kipande Erythrocyte
 
Huyo mburumundu ni huyu hapa:

View attachment 2003662

Kutokea kwenye uzi huu:

Kumbe Freeman Mbowe hakuwahi hata kumiliki namba ya simu ya Tigo

Ana hasira kali. Yumkini ni Kingai au binamu zake. Yaani wale wachawi wenyewe!

Cc: kipande Erythrocyte
Daah aisee, sema kwasababu sizingatiagi ID huwenda huyu ndo yule aliyekua ananiambia ile namba ni ya mbowe kwasababu imesajiliwa kwa majina yake

Ni mtu ambayr vitu vingi hajui, kwasababu kaisha jiaminisha kua kile kinacho-operate kwa mfumo rasmi mbao umeruhusiwa kwa umma ndio hivyo hivyo katika department zote
 
Nchi ina watu wa ajabu na hasa lile genge la wasiojulikana.

Wana hasira kali. Wakisikia katiba mpya, Mbowe au hata Chadema huhamanika mno, karibu ya roho zao kuwatoka:

Kama CCM siyo adui, mchawi wetu ni nani?

Hao ndiyo wachawi wenyewe.

Wako kama paka wenye kengele shingoni.
 
Ngoja tuone baadae jaji ataamua nini kwenye ule objection ya jana, hakuna kurudi nyuma.

Ushauri wa bure kwake - ni kheri akaacha sheria ikafuata mkondo wake.
 
Ilikuwa Jaji Luvanda akaja Jaji Siyani yupo Jaji Tingatinga. Nani mwingine ajaye?

Kama vipi mwingine tena itapendeza zaidi 😁😁.
 
Andiko lako nimesoma mstari wa kwanza to nikaachana nalo. Huwezi kufanya tathmini ya kitu chochote kwa kubase upande mmoja. Hiyo siyo tathmni bali ni mtazamo wako.
Kwani ni dhambi mtu kutoa mtazamo wake?Mataga wote motoni tu
 
Mstari wa kwanza ni huu:

"Clip inawaonesha washitakiwa mahakamani buheri wa afya na nyuso za bashasha."

Haiyumkiniki umesoma uzi mwingine siyo huu.
Mkuu achana na viumbe hawa waliojaa ushetani mioyoni mwao.
 
Kwani ni dhambi mtu kutoa mtazamo wake?Mataga wote motoni tu
Siyo dhambi kabisa. But asiseme tathmini, huwezi kuongelea tathmini halafu ukaegemea upande mmoja, lazima uangalie factors zote. Labda mleta mada awe haelewi maana ya tathmini.
 
Mstari wa kwanza ni huu:

"Clip inawaonesha washitakiwa mahakamani buheri wa afya na nyuso za bashasha."

Haiyumkiniki umesoma uzi mwingine siyo huu.
Nilichoandika ndicho nilichomaanisha. Hiyo nyingine ni tafsiri yako. Hakuna mtu anaeweza kushtakiwa kwa kesi nzito vile halafu akawa na uso wa bashasha mahakamani tusidanganyane, najua nia yako ni kuwatengeneza kisaikolojia nyumbu wenzio kwamba mwenyekiti wenu yupo salama.
 
Nyumbu ni mama yako
 
Ulivyojibu tu, umejionesha wazi, uwezo wako unaishia wapi.

Mtu mjinga anachoweza kufanya ni kukejeli au kutukana maana hiyo hata vichaa na wendawazimu huweza kufanya. Lakini jambo pekee ambalo vichaa na wendawazimu wanashindwa, ni kujenga hoja.
 
Nilichoandika ndicho nilichomaanisha. Hiyo nyingine ni tafsiri yako. Hakuna mtu anaeweza kushtakiwa kwa kesi nzito vile halafu akawa na uso wa bashasha mahakamani tusidanganyane, najua nia yako ni kuwatengeneza kisaikolojia nyumbu wenzio kwamba mwenyekiti wenu yupo salama.

Clip inajieleza unaweza kuchagua kujidanganya kama ilivyo haki yako kikatiba
 
Back
Top Bottom