Kesi ya Mdee na wenzake 18 yaitia aibu CHADEMA

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Sisi wanachama wa CHADEMA tunataka kuona, kusikia na kufanya mambo yanayosaidia kujenga, kukuza na hatimaye CHADEMA kuingia ikulu.

Kwa mara nyingine CHADEMA imenasa kwenye mtego wa ulimbo wa CCM. CHADEMA Inahangaika na kuwaondoa wanawake wao bungeni kwenye uchaguzi ambao cHADEMA walikataa kuutambua matokeo yake mpaka Leo.

Kesi hii ya kutaka akina Mdee watoke bungeni ilipaswa kutanguliwa na CHADEMA kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020 kwanza. CHADEMA walipaswa kuishia kwenye kuwafukuza uanachama akina Mdee TU basi na sio kukaza shingo lazima watoke kwenye bunge ambalo wao hawalikubali.

Kesi Yao ingekuwa na mashiko kama chadema wangepinga wabunge wote wa bunge kuweko bungeni maana hawakuchaguliwa kihalali kwa kutumia tume wasioikubali kuwa sio huru.

Maadam hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi basi bunge pia sio halali kwao. Kumlazimisha Mdee TU kuwa ndiye wakutoka bungeni badala ya bunge zima ni kukosa dira na mwelekeo.

Kwangu Mimi akina Mdee hawapaswi kuwa bungeni sawa na wabunge wengine wote kutokana na namna uchaguzi mzima ulivyoendeshwa. Njaa Kali, undugu na ukabila ndiyo sababu ya kuwashupalia akina Mdee.
 
Yaani Ccm mkiitwa mbulula mna stahili.
Yaani ulianza kudanganya wewe ni Chadema baadae umejikoroga na kuonyesha jinsia yako.
Waache Chadema wafanye yao. Hamta weza kuibomoa.
 
VICHAA tupo wengi humu Jf Kwa hiyo Chadema iruhusu UHUNI na Ujinga uendelee Kufanywa na Wanachama wake Ikae kimya Eti inajenga Chama basi Chadema itakuwa Chama cha Wahuni. Acha UTOTO
 
Akina Halima Mdee na wenzake wanajitambulisha kama wabunge wa Chadema

Hilo ndio tatizo

Kuzaa na Changu haimaanishi Wewe kavulata ni mumewe, natoa mfano tu!
Mtoto anapofukuzwa na wazazi nyumbani ataondoka na majina yake yote. Hata watoto wa mitaani wanayo majina ya wazazi wao. Akina Mdee wamefika pale bungeni wakitokea chadema, walikuwa wanachama na viongozi halali kabisa wa chadema. Kama wao wamewafikuza nyumbani kwao bado watabaki na jina lao.

Wao wamesusia matokeo, kuwatoa bungeni akina Halima pekee hakuna faida kwa chadema. Labda kama watautambua uchaguzi ule na bunge na kupeleka wanachadema wengine bungeni. Lakini kwa namna ilivyo Sasa wanayo mamlaka ya kuwafukuza uwanachama lakini sio ubunge, maana tume ya uchaguzi ndiyo inayofahamu wabunge wote walioko bungeni walipatikaje.

Jiulizeni akina Halima walifanikiwa vipi kuingia bungeni?
 
Kumbe wamefukuzwa Chadema?!!

Ahsante kwa ufafanuzi
 
Wewe sukuma gang ebu kaa pembeni tuwachie chadema yetu
 
Mfano wa "kavulana" huo.Mtoto akihama kwa shari, aondoke na makopo yake ya kuchezea. Na ikibidi abadili na jina kabisa achukue la mumewe aliyemtorosha nyumbani. Aape mahakamani kubadilisha ubini.
 
Kumbe wamefukuzwa Chadema?!!

Ahsante kwa ufafanuzi
Wametangaza hadharani kuwa wamewafukuza, kwao wanapaswa kuishia hapo. Maana bunge hili la Sasa liketokana na uchaguzi ambao chadema hawautambui na matokeo yake. Sasa shida Yao nini kutaka lazima akina Mdee watoke kwenye bunge wasilolitambua?

Kama chadema wangeyakubali matokeo tangu mwanzo shauri kama hili lisingekuwepo kama lilivyo Sasa. Wake kimya TU kwakweli. Mimi nilidhani wanakwenda mahakamani kusimamisha bunge Zima kuwa halikupatikana kihalali, kumbe ni akina Mdee TU.
 
Mfano unaotoa hauna mashiko, ukiachana na uchama tambua kwanza kuwa chadema pia Ni wananchi, na Wana haki ya kuhoji kitu chenye hakiendi sawa, na pia usisahau hao wabunge waliovikwa/ jivika kivuli Cha chadema wanakula jasho la watanzania
Binafsi naona chadema wako sawa ktk hili
 
Halima Mdee na wenzake hawakuapishwa mbele ya Siwa

Hivyo wale Siyo wabunge hata kama Chadema isingewafukuza
 
Jamaa kajichanganya
Jambo ambalo viongozi wa chadema hawapendi kuliweka wazi kujibu maswali yafuatayo:

1. Je, mwafaka (kama upo) umesabababisha chadema kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 2020?

2. Chadema inanufaikaje na akina Mdee kutoka bungeni Sasa?

3. Je, wabunge wa CCM ni halali?

4. Je, akina Mdee wakitoka bungeni watapeleka watu wengine kuchukua nafasi zao?

5. Chadema inapata hasara gani kwa akina Mdee kuwepo bungeni?

6. Je, ni lini chadema watatangaza kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa 2020?
 
Unapelekaje barua ya kufukuza Wanachama wa Chadena kwa Spika wa Bunge usilolitambua ?

Akina Halima Mdee na wenzake wanajitambulisha kama wabunge wa Chadema

Hilo ndio tatizo

Kuzaa na Changu haimaanishi Wewe kavulata ni mumewe, natoa mfano tu!
 
Uchaguzi wa 2020 ulikuwa mbovu kuliko chaguzi zote nilizowahi kushuhudia, yule jamaa alaaniwe Sana kwa kuua Uhuru na demokrasia hapa nchini kwani ndiye chanzo Cha haya

Japo Ccm km chama inapaswa kumshukuru Sana magu kwani aliisaidia Sana kuimarisha kwa kuua upinzani japo kimabavu Ila alifanikiwa
 
Wanaume wa chadema wanapelekewa moto na wanawake waliowatengeneza wenyewe
Binafsi wananikera sana, badala ya kuangalia na kuhangaika na chanzo (katiba na tume) wanahangaika na consequences za katiba na tume. Nani ameuroga upinzani wetu. Hata akina Mdee wakitoka, so what!!! Yaani mnawafukuza wanawake wwnu 19 bungeni na kuwaacha 400 ambao pia hamna uhakika walichaguliwaje wakifanya maamuzi kwaajili yenu wote. Mimi kwangu sioni kinachotafutwa hapa. Ndio maana nasema ni chuki iliyojisokotea kwenye ubinafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…