Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kesi inayomkabili Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kitunzi Kaijage, imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, huku mshtakiwa akiendelea kusota rumande akisubiri shauri lake kuendelea.
Wakili anayesimama upande wa mshtakiwa, Meshack Ngamando, amesema kesi hiyo iliyopangwa kuendelea, Agosti 27, 2026, haikuweza kusikilizwa baada ya Hakimu aliyepangwa kusikiliza shauri hilo kutokuwepo Mahakamani. Kwa sababu hiyo, kesi imeahirishwa hadi Septemba 10, 2026, ambapo inatarajiwa kuendelea katika Mahakama hiyo.
Soma: Wakili Wasonga: Mhadhiri wa UDOM anatuhumiwa kuchoma majengo ya umma pamoja na makazi ya askari Polisi yote nchini
Kaijage anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye namba 16278, inayohusisha tuhuma za makosa chini ya sheria ya kuzuia ugaidi.
Kaijage anatuhumiwa kuwa Julai 3, 2026 akiwa katika maeneo ya UDOM alikuwa na nia ya kuchoma majengo ya umma pamoja na makazi ya askari Polisi katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Zanzibar.
Awali, kesi hiyo ilipangwa kuendelea Agosti 19, 2026, lakini haikuendelea baada ya Hakimu Mkazi anayesikiliza shauri hilo, Zabibu Mpangule, kutokuwepo Mahakamani.
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Kombe na kuahirishwa hadi leo, Agosti 27, ambapo sasa imeahirishwa tena hadi Septemba 10.
Kwa sasa, Kaijage anaendelea kuwa rumande wakati akisubiri hatua inayofuata ya kesi hiyo, inahusisha uchunguzi wa awali (Preliminary Inquiry) kabla ya shauri hilo kupelekwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa.
Chanzo: Jambo TV