SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Najaribu kuwaza nikifuatilia kisa hiki cha mirathi ya Mengi na najiuliza maswali mengi kuhusu haya maisha.
Mengi amepigana akajenga familia yake na biashara zilizomfanya mmoja wa matajiri wakubwa nchini. Akiwa katika uzee wake, akaachana na mkewe na karibu kila kitu kinavurugika.
Ugomvi ndani ya familia, mali alizozipambania zinatapanywa na amri za kisheria.
Kuna maandiko ya Kiyahudi yanayosema duniani hakuna haki. Nawaza hivi, hawa watoto wa Mengi aliozaa na mke wake wa kwanza wametendewa haki au kwa kuwa wameshakuwa watu wazima, wamepewa elimu bora na experiences za biashara waachwe tu wakapambane kivyao.
Vipi kuhusu Jacqueline? Mwanamke aliyempa penzi jipya na kumfanya Mengi ajione ni kijana mpya je anastahili mali zote anazopata kisa tu amemzalia mapacha katika uzee wake na kumpa upendo huo?
Kuna visa vingi hata huko Marekani kwa matajiri kuachana na wake zao, najua sababu zinaweza kutofautiana, je wake za matajiri huwa wanabadilika wakijua hata wakiachana ana chake au ni kile kiburi tu cha kutambua mchango wake katika mafanikio hayo? Je wanaume wajifunze kujiombea uvumilivu na hekima hasa kwa wake zao?
Najua hatujui mengi yaliyokuwa yanatokea nyuma ya pazia, ila tujadili tu mafunzo ya maisha kutokana na kisa hiki bila kumnyooshea mtu kidole.