GE2025 Kesi ya Mpina: Mahakama yaomba muda zaidi mpaka Oktoba 15 kutoa uamuzi wa mwisho na usio wa mashaka

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mahakama kuu masjala kuu Dodoma imesema inahitaji muda zaidi wa kutoa uamuzi wa mwisho na usio wa mashaka katika shauri la Kikatiba lililofunguliwa na Mgombea Urais wa chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.

Mpina.png

Shauri hilo ni la kupinga kuondolewa kwake kuendelea na kampeni za kuwania urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwisho mwa mwezi huu.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa hii leo oktoba 10 na kuweka mustakabali wa iwapo Luhaga Mpina ataendelea na mchakato wa Kampeni au la.

Shauri hilo la Kikatiba la ACT WAZALENDO inayosikikizwa na Majaji watatu dhidi ya Tume ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali sasa itaamuliwa Oktoba 15 mwaka huu kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo, hoja zote za shauri hilo la kikatiba zilishasikilizwa kwa hiyo kipengele kilichobaki ni uamuzi wa mwisho.

Upande wa waleta maombi ukiongozwa na Wakili, John Seka unasema pande zote zilikuwa tayari kupokea uamuzi wa Mahakama Kuu.
 
Sasa muda upo wapi hapo wakati zimebaki chache uchaguzi ufanyike. It means ACT haina mgombea urais, imetoka hiyo!
 
Hivi huyo Mpina hana washauri ?[maana naona ameshindwa kujishauri]

Hadi hapo haoni alishapigwa chenga ya mwili na dalali mkuu na bado haamini kuwa ilikuwa staged karatasi za kura za uchafuzi zilishadurufiwa muda mrefu na ACT haina mgombea???

Tukiacha hilo tu dalali waziwazi alisema ubunge apatiwe yeye urais ni bi Mwenda?

Huyu Mpina wa sasa ni yule yule au ni copy , zile akili za kupambana na mafisadi ya sukari kwenye ile mikataba hapo kwenye kitu kidogo kashindwa kuzitumia na kuamua kuwaacha madalali na chama chao shikizi?
 
Mahakama kuu masjala kuu Dodoma imesema inahitaji muda zaidi wa kutoa uamuzi wa mwisho na usio wa mashaka katika shauri la Kikatiba lililofunguliwa na Mgombea Urais wa chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina na Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.

Shauri hilo ni la kupinga kuondolewa kwake kuendelea na kampeni za kuwania urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwisho mwa mwezi huu.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa hii leo oktoba 10 na kuweka mustakabali wa iwapo Luhaga Mpina ataendelea na mchakato wa Kampeni au la.

Shauri hilo la Kikatiba la ACT WAZALENDO inayosikikizwa na Majaji watatu dhidi ya Tume ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali sasa itaamuliwa Oktoba 15 mwaka huu kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo, hoja zote za shauri hilo la kikatiba zilishasikilizwa kwa hiyo kipengele kilichobaki ni uamuzi wa mwisho.

Upande wa waleta maombi ukiongozwa na Wakili, John Seka unasema pande zote zilikuwa tayari kupokea uamuzi wa Mahakama Kuu.
Hatuna mahakama. Kwenye nchi zenye mahakama zinazojitambua kesi zenye urgency ya aina hii zinachakatwa usiku na mchana, almost 24/7. Hii ingekuwa imeshakuwa decided na wahusika wana-proceed accordingly!
 
Tunaposema mifumo ya hii nch imejifia huu ndo ushahidi wenyewe.

Tunaposisitiza Jeshi na Nchi walikomboe hili Taifa tunaelewa kwa namna gani hii nchi imejifia.

Kwa haya maamuzi ya Mahakama kuna mtu mwenye akili timamu ataamini hii nchi ina Mahakama?
 
Back
Top Bottom