Kesi ya Mtumishi wa TRA aliyetishia Bastola na kujeruhi mtu Club 1245 yapigwa Kalenda hadi Januari 21, 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Kesi inayomkabili mshtakiwa Derick Derick Junior, ambaye alionekana katika kipande cha picha jongefu (video) kilichosambazwa katika mitandao ya kijamii, akimshambulia mtu mwingine kwa mateke na kitako cha bastola, imepangwa kuanza kusikilizwa ushahidi Januari 21, 2025, katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Pia Soma
  1. DOKEZO - √ - Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi
  2. Derick Derick Junior aliyemjeruhi mtu kwa Bastola (Club 1245) aachiwa kwa Dhamana
Tarehe hiyo ilipangwa jana Jumatano, Novemba 20, 2024 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Is-haq Kupa, wakati ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali huku upande wa mashtaka ukieleza unatarajiwa kuwa na mashahidi 12 na kuwasilisha vielelezo kadhaa.

Derick (36), ambaye ni Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkazi wa Salasala jijini Dar es Salaam anakabiliwa na mashtaka mawili, kujeruhi na kutembea na silaha hadharani kwa namna ya kuleta utisho, akidaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 27, saa 12.30 asubuhi, eneo la Maaki katika Club ya 1,245, iliyopo wilayani Kinondoni.

Katika shtaka la kwanza, Anadaiwa katika shtaka la kwanza alimjeruhi usoni sehemu ya jicho na puani Julian Bujuru kwa kumpiga kwa kitako cha bastola.

MWANANCHI
 
Mtu akishalewa unategemea kweli atende kosa akishirikisha ubongo wake!!??
Mazingira ya tukio ni kwenye club ya pombe.....
Ombaneni msamaha mka-settle hii kesi nje ya mahakama
 
Huo sio utetezi. Kwanini alienda na silaha mazingira ya pombe?
 
Utetezi mzuri kabisa huo. Kuna watu waliniambia hiyo silaha ilihifadhiwa gorofani wakati wa kuondoka alikwenda kuichukua ndio dhahama ikatokea. Watu wakiwa katika ulevi mwingi. Alafu ogopa ulevi wa pombe na k unaharibu akili kabisa
 
Kesi inayomkabili mshtakiwa Derick Derick Junior, ambaye alionekana katika kipande cha picha jongefu (video) kilichosambazwa katika mitandao ya kijamii, akimshambulia mtu mwingine kwa mateke na kitako cha bastola, imepangwa kuanza kusikilizwa ushahidi Januari 21, 2025, katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Pia Soma
  1. DOKEZO - √ - Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi
  2. Derick Derick Junior aliyemjeruhi mtu kwa Bastola (Club 1245) aachiwa kwa Dhamana
Tarehe hiyo ilipangwa jana Jumatano, Novemba 20, 2024 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Is-haq Kupa, wakati ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali huku upande wa mashtaka ukieleza unatarajiwa kuwa na mashahidi 12 na kuwasilisha vielelezo kadhaa.

Derick (36), ambaye ni Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), mkazi wa Salasala jijini Dar es Salaam anakabiliwa na mashtaka mawili, kujeruhi na kutembea na silaha hadharani kwa namna ya kuleta utisho, akidaiwa kutenda makosa hayo Oktoba 27, saa 12.30 asubuhi, eneo la Maaki katika Club ya 1,245, iliyopo wilayani Kinondoni.

Katika shtaka la kwanza, Anadaiwa katika shtaka la kwanza alimjeruhi usoni sehemu ya jicho na puani Julian Bujuru kwa kumpiga kwa kitako cha bastola.

MWANANCHI
Umezingatia mwaka?
 
Hii mbona sio mbinu mpya hapo wanaipiga kalenda na sababu watu ni wasahaulifu itaisha tu kama ilivyokuwa kesi ya afande Fatma Kigondo na Pauline Gekul.
 
Na kwa nchi zisizofuata sheria ndio kuna hao watoto wa kishua ila kwa wenzetu huku sheria ni msumeno na itakufikia tu.
Hii itamalizwa kihumi tu, ila ukiangalia ile video jamaa alikuwa anaenda aisee. Mtu ameshika gun kihasala vile, dakika sifuri tu unaweza zingua
 
Back
Top Bottom