Pre GE2025 Kesi ya mwanachama wa CCM na CHADEMA ni vitu viwili tofauti, huyo mwingine lazima tuhangaike naye!

Pre GE2025 Kesi ya mwanachama wa CCM na CHADEMA ni vitu viwili tofauti, huyo mwingine lazima tuhangaike naye!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Haya ni maneno yanayosemwa na mwana CCM, kwamba wao wakifanya kosa, watashughulikiwa tofauti na CHADEMA, hata ikiwa polisi ataonywa tu asirudie basi, ila kwa wengine kama CHADEMA ni tofauti, lazima ahenyeshwe sawa sawa!

Na hili ni kweli kabisa, si tunaona yanayotokea? Mwenyekiti UVCCM Kagera alifanywa nini baada ya kusema wakiwapoteza watu polisi wasiingilie? Si alionywa tu, kwamba huyu ni kijana, ulimi unateleza bla...blaaa....blaaa... angekuwa CHADEMA au mwananchi anakosoa serikali angeonywa hivyo tu kiupole na kuachwa salama?

Kama hukumbuki uzi huo soma hapa upate hasira kidogo: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Na hiki ndicho Nchimbi alichojibu: Nchimbi apinga kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera aliyeahidi "kuwapoteza" wakosoaji wa serikali

Ila nini kinatokea kwa watu wanaokosoa serikali, kwa wananchi wa kawaida na upinzani:

- Serikali, kutoa taarifa kutetea wanyonge ni kosa Kisheria? Malisa kafanya kosa gani kupaza sauti ili walimu walipwe stahiki zao?

- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana

Huu ni uonevu wa waziwazi kabisa, kwahiyo usipokuwa CCM wewe mhalifu moja kwa moja? Ndio tumefikia huku?

Narudisha mpira kwenu Wakuu.

#KataaMachawa
#KataaUozo2025
#KataaWasiyojulikana2025

===

"…lakini utaitamani tu pindi ukipata tatizo kwasababu kesi ya mwana CCM na kesi ya mwana CHADEMA hata iwe polisi au kwa mwenye kiti wa Kijiji ni vitu viwili tofauti. Huyu anaweza akaambiwa tu bwana hebu pisha usirudie moja mbili tatu akini tunakujua wewe ni wa hivi tutahangaika na wewe, si ndiyo maana yake? Uongo kweli?"

 
"…lakini utaitamani tu pindi ukipata tatizo kwasababu kesi ya mwana CCM na kesi ya mwana CHADEMA hata iwe polisi au kwa mwenye kiti wa Kijiji ni vitu viwili tofauti. Huyu anaweza akaambiwa tu bwana hebu pisha usirudie moja mbili tatu akini tunakujua wewe ni wa hivi tutahangaika na wewe, si ndiyo maana yake? Uongo kweli?"

View attachment 3038980
Huyu mshenzi atakufa kwa presha na unene huu. Apartheid kabisa anaitangaza wazi. Erythrocyte take note of this. Mbowe should adress this publically dunia ijue, mahakama ijue and all concerned!
 
"…lakini utaitamani tu pindi ukipata tatizo kwasababu kesi ya mwana CCM na kesi ya mwana CHADEMA hata iwe polisi au kwa mwenye kiti wa Kijiji ni vitu viwili tofauti. Huyu anaweza akaambiwa tu bwana hebu pisha usirudie moja mbili tatu akini tunakujua wewe ni wa hivi tutahangaika na wewe, si ndiyo maana yake? Uongo kweli?"

View attachment 3038980
Kuna jamaa alisema hii nnchi ngumu sana .hivi alikua nnani vile???
 
Kuna watu ni manguruwe katika umbo la binadamu. Kwa jinsi lilivyonenepeana kama furushi haishangazi kwa hayo anayoongea japo ni kweli
 
Katika Qur'an, mafundisho ya hukumu na haki yanajitokeza kwa njia mbalimbali, kutoa mwongozo kuhusu jinsi ya kuendesha mahakama na kutatua mizozo kwa njia ambayo ni ya haki na yenye uadilifu. Hapa kuna baadhi ya mafundisho muhimu kuhusu hukumu na haki katika Qur'an:

  1. Uadilifu na Usawa:Qur'an inasisitiza umuhimu wa uadilifu na usawa katika hukumu. Mfano wa haya unapatikana katika Surat An-Nisa (4:58) ambapo Allah anawaamuru walezi na majaji kutoa hukumu kwa uadilifu bila ya kubaguliwa kwa watu au kuathiriwa na hisia za kibinafsi.
  2. Kusikiliza Pande Zote:Qur'an inawahimiza majaji na watu wenye mamlaka kusikiliza pande zote mbili kabla ya kutoa hukumu. Hii inapatikana katika Surat Al-Hujurat (49:6) ambapo watu wanahimizwa kuchunguza kwa uangalifu madai na hoja kabla ya kufanya maamuzi.
  3. Kuzuia Uonevu:Qur'an inakataza vikali uonevu na ubaguzi katika hukumu. Kwa mfano, Surat Al-Ma'idah (5:8) inawakumbusha waamuzi kutoa hukumu kwa uadilifu hata kama hilo linahusisha kujipigania mwenyewe.
 
Kwa sababu nchi haina uwajibikaji jamaa ataendelea na nafasi yake kama hakuna ambacho kimetokea. Kauli kama hizi kutoka kwa viongozi ujue katu CCM haiwezi kuondolewa kwa sanduku la kura maana hata wao wanakwambia polisi wanashughulikia tofauti watu kwa misingi ya vyama.
Ni kama vile anawatisha watu wajiunge na CCM hata wakitenda uhalifu wanaweza wasishughulikiwe.
 
Ni sahihi kabisa, kwa sababu shetwani akimkosea mwanadamu, na kesi hiyo ikapelekwa kwa jaji shetwani, matokeo yake wajaua yatakuwaje?
Kwetu sisi Wa Matumbi huwa tuna usemi wetu wa kesi ya nyani ukampelekea shitaka tumbili/ngedere unategemea hukumu itakuwaje?
Lakini, wengine huwa tuna imani kuwa shetwani hajawahi kumshina Mungu, tusimame na MWENYE ENZI MUNGU!
 
Back
Top Bottom