Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imeshindwa kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili msanii Joyce Mbaga, maarufu kama Nicole, kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika. Mbali na Nicole (32), mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Rehema Mahanhu. Wote wawili walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Machi 10, 2025, na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemalira.
Katika kesi hiyo iliyotajwa leo, upande wa Jamhuri umeieleza mahakama kuwa bado haujakamilisha upelelezi, hivyo wameomba muda zaidi. Kutokana na ombi hilo, mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Aprili 14, 2025. Hadi sasa, washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana wakisubiri hatua zaidi za kisheria.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo kuongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia faida kwa njia isiyo halali. Pia, wanadaiwa kupokea amana au kufanya miamala ya fedha bila kuwa na leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kinyume cha sheria za kifedha nchini.
Katika shtaka la pili, wanadaiwa kuwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025, walipokea Sh 185,515,000 kutoka kwa wananchi bila kibali. Aidha, shtaka la tatu linawataja kuendesha mfumo wa malipo bila kuwa na leseni inayotolewa na BoT. Kesi hii inasubiri hatua zaidi baada ya kukamilika kwa upelelezi.