Kesi ya Rais Kenyata ICC mashahidi 2 wajiondoa, yaahirishwa kukusanya ushahidi zaidi

Kesi ya Rais Kenyata ICC mashahidi 2 wajiondoa, yaahirishwa kukusanya ushahidi zaidi

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
68797894_68797893_a4173.jpg

Kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta huenda ikachelewa kuanza baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC) Kukiri kuwa hana ushahidi wa kutosha wa kuendeleza kesi hiyo.
Rais wa Kenya amekanusha mashtaka ya dhulma dhidi ya ubinadamu zinazohusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Zaidi ya watu elfu moja waliuawawa katika mapiganao hayo na maelfu yaw engine kupoteza makazi yao.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bi. Fatou Bensouda amesema kuwa uamuzi huo unatokana na mashahidi wawili wakuu katika kesi hiyo kukataa kutoa ushahidi dhidi ya Rais Kenyatta. Mmoja wao amesema kuwa hayuko radhi kusema anayojua kuhusu kesi hiyo ilhali wa pili amesema kuwa alidanganya katika ushahidi wake wa awali katika kesi hiyo.
Kujiondoa kwa mashahidi hao imemfanya kiongozi wa mashtaka kusema kuwa kesi dhidi ya Bwana Kenyatta haifikii kiwango cha ushahidi kinachohitajika jambo lililomchochea kuomba kesi hyo isimamishwe kwa muda ili aweze kusawazisha na kukusanya ushahidi zaidi.

Kesi ya Bwana Kenyatta ilipaswa kuanza huko The Hague tarehe 5 Februari mwaka ujao . Bwana Kenyatta alishtakiwa pamoja na naibu wake William Ruto na mtangazaji Joshua Arap Sang kwa makosa ya mauji, kusababisha watu kuhamishwa kwa nguvu katika makazi yao, kusababisha mateso kwa umma na ubakaji kufuatia ghasia zilizotokana na matokeo ya urais katika uchaguzi huo.

Kesi ya Kenyatta na naibu wake imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na jamii ya kimataifa haswa baada ya Umoja wa Afrika kutishia kuyaondoa mataifa ya Afrika katika uanachama wa mahakama hiyo iliyobuniwa chini ya mkataba wa Roma. Umoja wa Afrika umekuwa ukidai mahakama hiyo imekuwa ikiwalenga viongozi wa bara Afrika.(P.T)

Hisani ya Mjengwa Blog
 
mashaidi wanajitoa kwa sababu ya rusha na vitisho kutoka katika serekali dhalimu na icc imeshandwa kuwapa ulinzi mashaidi hivyo hakuna haliopo tiyari kupoteza maisha yake kwa sababu ya kutoa ushaidi dhidi kiongozi wa mongiki
 
Hivi odinga aliachwa kwa sababu zipi.?odinga ni mtuhumiwa namba moja kwenye hii kesi
 
wala si vitisho mkuu. ICC wanalipana mishahara minono kisha wanawafungia mashahidi ktk safe house kwa kuwapa posho ya kujikimu with lots of restrictions....huku UK wanatoa mkwanja wa nguvu ili wajitoe katika kesi. Hiyo inasababisha wengi wajitoe.
 
kuna kitu hawezekani mashahidi wagome kutoa ushahidi lazma watakuwa wamepewa rushwa
 
Looks like these cases will falter, no credible evidence was gathered by the ICC. This is the folly of relying on other people's work.
 
I said it..Raila ndo key suspect kwa hii kesi nashangaa kwa nini aliachwa
 
Kuwa rais raha, no wonder watu wanatoa kila kitu waupate urais muda ukienda hivyo mheshimiwa rais atakuwa hana kesi ya kujibu..😀😀🙄
 
ni heri kesi ingefanyika sasa kuliko amalize kipindi chake cha urais, atajuta.
 
mashaidi wanajitoa kwa sababu ya rusha na vitisho kutoka katika serekali dhalimu na icc imeshandwa kuwapa ulinzi mashaidi hivyo hakuna haliopo tiyari kupoteza maisha yake kwa sababu ya kutoa ushaidi dhidi kiongozi wa mongiki

Kenyata ni mtu hatari sana
Na ndiye aliyelipua westgate ili kupata sababu ya ziada ya kutoburuzwa kortini.
 
wala si vitisho mkuu. ICC wanalipana mishahara minono kisha wanawafungia mashahidi ktk safe house kwa kuwapa posho ya kujikimu with lots of restrictions....huku UK wanatoa mkwanja wa nguvu ili wajitoe katika kesi. Hiyo inasababisha wengi wajitoe.
Mkuu ni kweli UK anatoa mkwanja wa kufa mtu, lakini hiyo pekee haiwezi kuzuia watu wenye misimamo kutoa ushihidi dhidi ya UK - mimi nafikiri vile vile wanatoa vitisho kwa mashahidi na familia zao pia, nimewahi kusikia some potential witness walikuwa wanapotea kiaina. All in all huyu mama prosecutor siwa kuchezea, atakuwa anatafuta mbinu za kumunasa UK eventually.
 
Hivi odinga aliachwa kwa sababu zipi.?odinga ni mtuhumiwa namba moja kwenye hii kesi

Hata mwai kibaki sioni kwanini aliachwa ilihali yeye ndie aliyelazimisha matokeo ya kihuni kutangazwa!!!
 
Mkuu ni kweli UK anatoa mkwanja wa kufa mtu, lakini hiyo pekee haiwezi kuzuia watu wenye misimamo kutoa ushihidi dhidi ya UK - mimi nafikiri vile vile wanatoa vitisho kwa mashahidi na familia zao pia, nimewahi kusikia some potential witness walikuwa wanapotea kiaina. All in all huyu mama prosecutor siwa kuchezea, atakuwa anatafuta mbinu za kumunasa UK eventually.

AU/IGAD/EAC inamsupport uhuru kwa hili jambo la kujiondoa ICC na kwa sasa wanachezea mbali UK maana wanajua ana mamlaka ya kukusanya mataifa yote africa kujitoa iCC, anaweza vuta trigger, kwa kutia saini kwenye mswada. chances sio hata 50-50 kati yake, na lazima ICC kukimya kuongelea uhuru, ndio huyu mama mwongo bensuda kafukuza mashaidi mwenyewe.................
 
Mkuu Kabaridi - well said jamaa huyu mjanja sana, nafikiri anawatumia vile vile baadhi ya Waingereza kumpigia debe. Kinacho nishangaza naona Ruto wala hajashtuka kwamba actually Uhuru atamuacha kwenye mataaa afungwe yeye! 4 some reason Ruto hilo hajaliona!!!
 
Ashaliona lakini nd'o basi tena...hana jinsi.
 
Back
Top Bottom