Kesi ya Sabaya: Video kutoka Benki zikionesha maboksi yenye fedha alizoomba Sabaya zawasilishwa Mahakamani

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imepokea video sita zilizokuwa kwenye ‘flash disk’ iliyowasilishwa kama ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Wiki iliyopita, upande wa utetezi ulipinga kupokelewa kwa video hizo kama ushahidi katika kesi hiyo lakini baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote, imekubali kuzipokea.

Katika video hizo, watu wawili wanaonekana wakiingia katika benki ya CRDB tawi la kwa Morombo mkoani Arusha na kuchukua maburungutu ya fedha ambazo ziliwekwa kwenye maboksi.

Afisa wa benki alionekana akiwa ameshika maboksi mkononi kabla ya kuanza kuhakiki fedha hizo na kuzipanga kwenye maboksi, kisha aliziweka juu ya kiziti chenye matairi na kwenda kuwakabidhi watu hao wawili.

Watu hao ambao mmoja anaonekana ni mtu wa makamo aliyevaa koti kubwa na mwingine ni kijana, walichukua maboksi hayo yenye fedha na kwenda kuingia nayo kwenye gari la bluu.

Video hizo zilitolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kupitia shahidi wake wa nne, Jonson Kisaka.
 
Hivi hatuez pata video Kama hizi za Bashite nae akamsaidie mwenzake kule. Hebu wadau wenye ushahidi tuukusanye tupate mawakili wa kutusaidia tujenge Tanzania yenye nidhamu
Wakati utafika tu
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imepokea video sita zilizokuwa kwenye ‘flash disk’ iliyowasilishwa kama ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Wiki iliyopita, upande wa utetezi ulipinga kupokelewa kwa video hizo kama ushahidi katika kesi hiyo lakini baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote, imekubali kuzipokea.

Katika video hizo, watu wawili wanaonekana wakiingia katika benki ya CRDB tawi la kwa Morombo mkoani Arusha na kuchukua maburungutu ya fedha ambazo ziliwekwa kwenye maboksi.

Afisa wa benki alionekana akiwa ameshika maboksi mkononi kabla ya kuanza kuhakiki fedha hizo na kuzipanga kwenye maboksi, kisha aliziweka juu ya kiziti chenye matairi na kwenda kuwakabidhi watu hao wawili.

Watu hao ambao mmoja anaonekana ni mtu wa makamo aliyevaa koti kubwa na mwingine ni kijana, walichukua maboksi hayo yenye fedha na kwenda kuingia nayo kwenye gari la bluu.

Video hizo zilitolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kupitia shahidi wake wa nne, Jonson Kisaka.
Halafu unaambiwa mhalifu huyo ndiye alikuwa anataka kuwawa na Mbowe?
 
Back
Top Bottom