Kesi ya Sabaya: Video kutoka Benki zikionesha maboksi yenye fedha alizoomba Sabaya zawasilishwa Mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imepokea video sita zilizokuwa kwenye ‘flash disk’ iliyowasilishwa kama ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Wiki iliyopita, upande wa utetezi ulipinga kupokelewa kwa video hizo kama ushahidi katika kesi hiyo lakini baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote, imekubali kuzipokea.

Katika video hizo, watu wawili wanaonekana wakiingia katika benki ya CRDB tawi la kwa Morombo mkoani Arusha na kuchukua maburungutu ya fedha ambazo ziliwekwa kwenye maboksi.

Afisa wa benki alionekana akiwa ameshika maboksi mkononi kabla ya kuanza kuhakiki fedha hizo na kuzipanga kwenye maboksi, kisha aliziweka juu ya kiziti chenye matairi na kwenda kuwakabidhi watu hao wawili.

Watu hao ambao mmoja anaonekana ni mtu wa makamo aliyevaa koti kubwa na mwingine ni kijana, walichukua maboksi hayo yenye fedha na kwenda kuingia nayo kwenye gari la bluu.

Video hizo zilitolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kupitia shahidi wake wa nne, Jonson Kisaka.
Ina maana John Pombe Magufuli alikosa watu wa kuwateua kuwa ma Dc hadi akaamua kumteua Jambazi Ole Sabaya ?
 
Hapa hutasikia watu wamesusia huduma za CRDB, Subiri sasa ushahidi kama huu utolewe kwenye ile kesi pendwa utaskia kelele za watu tufunge akaunti CRDB.
Kwa kweli Miongoni mwa Mitandao ya Simu ina huduma nzuri sana ni Tigo! Wanafanya vizuri aisee
 
MTOTO ALIKUWA JAMBAZI KWELI, ALITUMIA SERIKALI KIVULI CHA WIZI, DAH
Ndio maana mungu alituondolea kikwazo. Hata Kodi zilizokuwa zinaishia bgadolite kutengeneza miundombinu ambayo haikuwamo kwenye mipango.

Mungu mwema anazidi kutuponya tu
 
Hivi hatuez pata video Kama hizi za Bashite nae akamsaidie mwenzake kule. Hebu wadau wenye ushahidi tuukusanye tupate mawakili wa kutusaidia tujenge Tanzania yenye nidhamu
Zipo. Tuanzie zile za clouds
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imepokea video sita zilizokuwa kwenye ‘flash disk’ iliyowasilishwa kama ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Wiki iliyopita, upande wa utetezi ulipinga kupokelewa kwa video hizo kama ushahidi katika kesi hiyo lakini baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote, imekubali kuzipokea.

Katika video hizo, watu wawili wanaonekana wakiingia katika benki ya CRDB tawi la kwa Morombo mkoani Arusha na kuchukua maburungutu ya fedha ambazo ziliwekwa kwenye maboksi.

Afisa wa benki alionekana akiwa ameshika maboksi mkononi kabla ya kuanza kuhakiki fedha hizo na kuzipanga kwenye maboksi, kisha aliziweka juu ya kiziti chenye matairi na kwenda kuwakabidhi watu hao wawili.

Watu hao ambao mmoja anaonekana ni mtu wa makamo aliyevaa koti kubwa na mwingine ni kijana, walichukua maboksi hayo yenye fedha na kwenda kuingia nayo kwenye gari la bluu.

Video hizo zilitolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kupitia shahidi wake wa nne, Jonson Kisaka.
Jiwe aliwaponza hawa watoto wa Watu kibwege sana , huyu alifanya uhalifu bila kuogopa chochote , hata alipojua anarekodiwa hakuogopa chochote
 
Hapa hutasikia watu wamesusia huduma za CRDB, Subiri sasa ushahidi kama huu utolewe kwenye ile kesi pendwa utaskia kelele za watu tufunge akaunti CRDB.

Uwezo wako wa ku analyze mambo ni mdogo sana, hutakiwi hata kujibiwa maana Huna uwezo wa kuelewa utakachojibiwa
 
Huwezi kutenga wizi wa sabaya na utawala wa magufuli. Kwa kifupi huo wizi alitumwa na magufuli..
Katika kesi yeke ya kwanza iliyompatia kifungo cha miaka 30, Sabaya alisema kuwa Makamu wa rais Mpango na Gavana wa benki kuu walikuwa wanajua operation alizokuwa anaendesha!! Cha kusahangaza hakuwaita kama mashahidi wake wakati wa kujitetea na hao ndio wangemsaidia kudhihirisha kama kweli alikuwa anatumwa na mwendazakae!!
 
Uwezo wako wa ku analyze mambo ni mdogo sana, hutakiwi hata kujibiwa maana Huna uwezo wa kuelewa utakachojibiwa
we mwenye uwezo mkubwa umefika wapi? Ungekuwa na uwezo kunizidi ungekuwa kwenye CEOrt au unashindana na aki MO na Bakhresa mida hii. Bangladesh...
 
Hapa hutasikia watu wamesusia huduma za CRDB, Subiri sasa ushahidi kama huu utolewe kwenye ile kesi pendwa utaskia kelele za watu tufunge akaunti CRDB.

Ha ha ha,yani ukitolewa ushahidi upande huu Mahakama inasifiwa kwa kila kitu,lakini kule kwa kesi ile pendwa,Mahakama inatupiwa kejeli zote hata kama kinachofanyika kule ni sawa na kinachofanyika huku.
 
Hivi hatuez pata video Kama hizi za Bashite nae akamsaidie mwenzake kule. Hebu wadau wenye ushahidi tuukusanye tupate mawakili wa kutusaidia tujenge Tanzania yenye nidhamu
Bashite amepora hata physical properties!! Shahidi zipo nyingi sana, ni Muda tu
 
Back
Top Bottom