Kama tunavyojua Sheikh Ilunga alikamatwa Tabora na si kama ilivyo kawaida anapokamatwa kiongozi wa kiislam. safari hii imetumika staili ya kizenzi, kakamatwa tabora na kaambiwa anahitajika mwanza aende mwenyewe. Na baada ya kufika mwanza kafunguliwa mashtaka ya uchochezi.
Naam, Yupo kitaa na kesi imeahirishwa hadi januari 6 kutokana na ushahidi haujakamilika
Ushahidi haujakamilika au hana kesi ya kujibu kwa uchochezi. Kwa mujibu wa kauli yake alikuwa anatamani sana afunguliwe kesi hiyo ya uchochezi ili jamii ipate maana halisi ya uchochezi. na jamii ijue iwapo kusema ukweli ni uchochezi? au kuwa na fikra mbadala nje ya siasa au tofauti na watawala ni kosa? Na kwanini watu wamuhukumu kwa kumuelewa vibaya alisisitiza.
Mwisho anaamini hana kesi ya kujibu zaidi polisi kufunika kombe na kuwaridhisha jamii kuwa serikali inafata misingi ya utawala bora na kufumbia mambo uhuru wa kuongea uliopo.