KUNA tetesi kuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameshindwa kushiriki ziara ya Rais Samia nchini China kutokana na kukabiliwa na Kesi ya Rushwa na Uhujumu uchumi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuhusu kashfa ya utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi.
Pamoja na kwamba kwenye ziara hiyo kuna mikataba mbalimbali inayokwenda kusainiwa kuhusu sekta ya Kilimo kati ya China na Tanzania lakini kutokana na hiyo Kesi imelazimika kuzuiliwa kuambatana na Mama ili aendelee kushughulikia kesi inayomkabili.
Baadhi ya watu wake wa karibu ndani ya Wizara ya Kilimo wanadai kuwa Bashe amshtakiwa kama Waziri hivyo kwa sehemu kubwa atatakiwa kukutana mara kwa mara na Mawakili wa Serikali ili kujua kwa kina aina ya makosa aliyostakiwa nayo kwani kwa sehemu kubwa makosa aliyofanya Bashe ameyafanya yeye kama yeye binafsi na sio kupitia mfumo wa Wizara. Hata kesi ya Wakulima wa Miwa wa Kilombero wameshtaki Waziri wa Kilimo na hawakuishtaki Serikali wala Wizara ya Kilimo.
Pia soma:Mpina kuwapeleka Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria