Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kesi inayowakabili viongozi wa Uamsho imeendelea leo katika mahakama ya Vuga huku Zanzibar ambapo imeelezwa mahakamani hapo kuwa upelelezi bado unaendelea. Kesi imeahirishwa hadi Rat 29 mwezi huu,
Mahakamani hapo Shelkh Farid amepata wasaa mfupi wa kutoa neno kwa watu na kuwahoji kama wanautaka muungano au lah ambapo watu walijibu kwa nguvu kuwa hawautaki. Pia akawataka waandishi wa habari wafike kwenye vyuo vya mafunzo (jela) wakajionee namna wafungwa wanafoteseka wakiwao wao.
Wamedai kuwa uongozi wa jela unawanyima ndugu zao haki ya kuwapelekea huduma kama maji ya kunywa na vyakula ambavyo huwa inaruhusiwa, lakini kwao wamepigwa marufuku kupelekewa huduma hizo.
Mkuu Mwana Mpotevu, hii imekaaje kisheria kama mtu amekatwa kwa kosa la uchochezi; na bado anafanya uchochezi katika viwanja vya mahakama, si anaendelea kutenda kosa. Aidha, hii inaonyesha kuwa huko Chuo cha mafunzo (jela) hawateswi, wangekuwa wanateswa asingepata nguvu za kuendelea kuwahoji wafuasi wake kuhusu hatma ya Muungano. Yaani mtu aliyeonja mateso ya huko, akikuona tu analia machozi !!!!
Mahabusu sio Serena hotel. Walitakaje? waletewe mademu?