R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, leo inaanza kusikiliza kwa siku tatu mfululizo kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Lema anadaiwa kutoa kauli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alikwenda kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha kama anakwenda kwenye sherehe za kuaga mtoto wa kike ‘sendoff'. Shauri hilo linalovuta hisia za wengi linasikilizwa na Hakimu Mkazi, Devotha Msofe, ambapo Juni 10, mwaka huu Wakili wa Serikali, Elianenyi Njiro, wakati akisoma maelezo ya awali alidai kuwa wanatarajia kuleta mashahidi tisa akiwamo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), John Nanyaro na Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Arusha (OCD), Gillis Mroto.
Mashahidi wengine ni maofisa wa Jeshi la Polisi akiwamo Mkaguzi Bernard Nyambanya na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane, PC Godfrey, Joachim Mahanyu na wengine kutoka Chuo cha Uhasibu, Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu Hamidu.
Katika kesi hiyo, Lema akiwa eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu, anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi yaliyosababisha uvunjifu wa amani.
Maneno hayo yanayodaiwa kutamkwa na Lema ni kinyume cha kifungu cha 390 sura ya 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu marejeo ya mwaka 2002. "RC anakuja (Chuo cha Uhasibu), kama anaenda kwenye sendoff, hajui chuo kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho … (RC), ameshindwa hata kuwapa (wanafunzi) pole kwa kufiwa na amesema hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu," alinukuu baadhi ya maneno yanayodaiwa kutamkwa na Lema siku ya tukio.
Wakili Njiro alidai mahakamani hapo kuwa kauli hizo zilipandisha hasira za wanafunzi ambao walianza kumrushia mawe na chupa Mkuu wa Mkoa, Mulongo alipokuwa akiwahutubia kuhusiana na tukio la kifo cha mwanafunzi, Henry Koga, kilichotokea Aprili 23,