Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Glory Mwakihaba anayesikiliza kesi hiyo aliaihirisha hadi Agosti 17, 2026.
Katika kesi hiyo iliyotajwa kwa mara ya kwanza Julai 24, 2026, watuhumiwa watatu wanakabiliwa na shtaka la kupanga kufanya kosa la ugaidi, huku wengine 14 wakishtakiwa kwa kosa la kula njama za kufanikisha kosa hilo.
Upande wa Jamhuri umewakilishwa na jopo la mawakili watatu wakiongozwa na Leonard Kiwango, huku upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili wane ambao ni Peter Kibatala, Gaston Garubindi, Alex Masaba, na Gloria Ulomy.
Soma zaidi: Heche: Ndani ya siku 2, Viongozi 51 wa CHADEMA wamekamatwa na kubambikiziwa Kesi za Ugaidi