Kesi ya ugaidi wa Mbowe na wenzake: Nini maana ya "submission?". Je, ni kweli kuwa DPP ana mamlaka ya kuingilia majukumu ya mahakama?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Jana tarehe 29/10/2021 mashahidi wa pande mbili wamemaliza kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili m/kiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu...

Kesi hii ndogo imezaliwa baada ya upande wa utetezi kupinga kupokelewa kwa maelezo ya mshitakiwa wa pili Adamoo aliyoyatoa polisi baada ya kukamatwa kama kielelezo ikidaiwa kuwa alilazimishwa kwa mateso kusaini maelezo yasiyo yake...

Pande zote mbili zimemaliza kujitetea. Jamhuri ikijitetea kivyake ili kuishawishi mahakama ipokee kielelezo hicho na upande wa utetezi kupinga kuwa kielelezo hicho kilipatikana kinyume cha sheria ya makosa ya jinai...

Jaji Siyani ametangaza kuwa atatoa uamuzi wake tarehe 19/10/2021 na tarehe 4/10/2021 ameangiza kila upande ulete "submission" yake kwa maandishi fupi isiyozidi kurasa 5....

Nini maana ya "submission" kwa mujibu wa sheria ktk kesi ya jinai? Wakili Peter Madeleka anaeleza...

Kwa upande mwingine, wote tunajua kuwa aliyekuwa DC wa wilaya ya Hair, Ole Lengai Sabaya naye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi...

Kwa mujibu wa sheria na katiba, mahakama kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuamua mashauri yote ya kesi za uhujumu uchumi...

Lakini cha ajabu, kesi ya Ole Lengai Sabaya inasikilizwa na mahakama ya hakimu mkazi Arusha kwa maelezo kuwa DPP ametoa kibali mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo...

Je, DPP ana mamlaka hayo? Wakili Peter Madeleka analitolea ufafanuzi hilo pia katika video hiyo hapo juu...

Elimu haina mwisho. Tuendelee kujifunza
 
Ndio maana sisi wananchi tunaomba kila siku Lugha ya Kiswahili itumike ktk kutoa Haki za Watanzania.
Sheria imepitishwa na Bunge lkn hatujui Utekelezaji umekwamia wapi, hata mimi sijui maana ya hilo neno "submachine" ndio nini? ni silaha ya kivita au ?
 
Court submission
A document intended for the court which summarizes the relevant facts, the law and a proposed analysis to bring to the two, on behalf of a litigant. Related Terms: Factum.

Jana tarehe 29/10/2021 mashahidi wa pande mbili wamemaliza kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili m/kiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu...

Kesi hii ndogo imezaliwa baada ya upande wa utetezi kupinga kupokelewa kwa maelezo ya mshitakiwa wa pili Adamoo aliyoyatoa polisi baada ya kukamatwa kama kielelezo ikidaiwa kuwa alilazimishwa kwa mateso kusaini maelezo yasiyo yake...

Pande zote mbili zimemaliza kujitetea. Jamhuri ikijitetea kivyake ili kuishawishi mahakama ipokee kielelezo hicho na upande wa utetezi kupinga kuwa kielelezo hicho kilipatikana kinyume cha sheria ya makosa ya jinai...
 
Jana tarehe 29/10/2021 mashahidi wa pande mbili wamemaliza kutoa ushahidi wao katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili m/kiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu...

Kesi hii ndogo imezaliwa baada ya upande wa utetezi kupinga kupokelewa kwa maelezo ya mshitakiwa wa pili Adamoo aliyoyatoa polisi baada ya kukamatwa kama kielelezo ikidaiwa kuwa alilazimishwa kwa mateso kusaini maelezo yasiyo yake...

Pande zote mbili zimemaliza kujitetea. Jamhuri ikijitetea kivyake ili kuishawishi mahakama ipokee kielelezo hicho na upande wa utetezi kupinga kuwa kielelezo hicho kilipatikana kinyume cha sheria ya makosa ya jinai...
Sema 29/9/2021
 
ndio maana sisi wananchi tunaomba kila siku Lugha ya Kiswahili itumike ktk kutoa Haki za Watanzania.
Sheria imepitishwa na Bunge lkn hatujui Utekelezaji umekwamia wapi, hata mimi sijui maana ya hilo neno "submachine" ndio nini? ni silaha ya kivita ?
Hilo neno ni gobore la kivita,hata hujakosea,umepatia Kweri kweri. 😂
 
Video ya dakika 12 angalia wewe mwenyewe mleta uzi.Unafikiri kuwa bando ni sawa na maji ya bomba?
AUfr_W.jpg
 
ndio maana sisi wananchi tunaomba kila siku Lugha ya Kiswahili itumike ktk kutoa Haki za Watanzania.
Sheria imepitishwa na Bunge lkn hatujui Utekelezaji umekwamia wapi, hata mimi sijui maana ya hilo neno "submachine" ndio nini? ni silaha ya kivita au ?
Imesemwa submission na sio submachine
 
Back
Top Bottom