βοΈ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA
SEHEMU YA 3 β TAREHE 8.9.2026
Lissu: Naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno βtunaenda kupiga watu wanaoenda kupiga kura au kuwakata vidole.β
Brenda: Waheshimiwa Majaji, hayo maneno hayapo.
Lissu: Kuna maneno yamesemwa kuwa kuna askari 17 wameuawa siku ya Uchaguzi Mkuu, tarehe 29 Oktoba. Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo kuna maneno kuwa βtutaua askari wa Polisi.β
Brenda: Hayo maneno hayapo.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno βmkachome vituo vya daladala au mabasi yenyewe.β
Brenda: Hayapo kabisa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno βtutachoma moto vituo vya kupigia kura na tutawapiga wasimamizi wa vituo hivyo.β
Brenda: Hayo maneno hayapo.
Lissu: Kwa ufahamu wako, Shahidi, mtu akisema βmsimamo huu unaashiria uasi,β anakuwa ametenda kosa gani?
Brenda: Mtu akisema βmsimamo huu unaashiria uasiβ siyo kosa, kwa sababu uasi ni pamoja na kupinga au kukataa jambo.
Lissu: Asante.
Na mtu akisema βtutazuia uchaguzi,β kwa ufahamu wako anakuwa ametenda kosa gani?
Brenda: Siyo kosa kusema βtutazuia uchaguzi.β
Lissu: Shahidi, mtu akisema βtutavuruga uchaguzi,β anakuwa ametenda kosa gani?
Brenda: Mimi siyo mtaalamu wa sheria na sijui sana, ila kwa maoni yangu siyo kosa.
Lissu: Siyo kwa maoni yako, kwa ufahamu wako je?
Brenda: Kwa ufahamu wangu, siyo kosa.
Lissu: Mtu akisema βtutahamasisha uasi,β anakuwa ametenda kosa gani?
Brenda: Anakuwa hajatenda kosa.
Lissu: Mtu akisema βtutakinukisha,β kwa ufahamu wako, hilo neno lina maana gani?
Brenda: Tutakifanya kinukie.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kukifanya kinukie ni kosa gani kwa sheria za nchi hii?
Brenda: Siyo kosa kwa sheria za nchi hii.
Lissu: Hata βkukifanya kinukeβ ni kosa kwa sheria za nchi hii?
Brenda: Siyo kosa.βοΈ TUNDU LISSU AENDELEA KUMHOJI SHAHIDI BRENDA RUPIA

Brenda: Siyo kosa.