Kesi ya uhaini na kifo cha Komando Tamimu

Hapana familia ya kanal mahfoudhi iko Zanzibar ..japo mahfoudhi alifia na kuzikwa msumbiji ...inasemekana mahfoudhi ndo comandoo mkali kuwahi kutokea tz..cjui wanaosema hvyo wako sasa au lah
Huyo kanali Mahfoudh kuna mzee huwa anamtaja Mavuzi kumbe ni huyo Leo ndo nimejua nini yule mzee huwa anamaanisha.
 
Kingentengenezwa kitabu kwa ajili ya kumbukumbu ya kizazi cha sasa na badae
 
Imebidi nichangie japo kidogo kuhusu Kifo cha Tamimu.

Wengi wenu mnapotosha watu kuhusu kifo cha komando Tamimu. Komando Tamimu hakuuliwa wala kupigwa risasi na Mabere Marando.

Mabere Marando ni kweli alikuwa Tiss lakini wakati wa Jaribio la Mapinduzi ya mwaka 1982, alikuwa ashatoka Tiss ambapo alijiondoa mwaka 1980. Hivyo hakumpiga risasi Komando Tamimu.
 
Humu kwenye hii Thread kuna utani mwingi saaaaaaaaa kuliko uhalisia wa issue nzima ya matukio ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi ya mwaka 1982 ila mwenye nia ya kujuwa ukweli atafute kitabu cha Kesi ya Uhaini chapisho la kwanza (c) 1985 Kilichoandikwa na Marehemu Mnenge S. Suluja. Nacheka kuona kuna mchangiaji akintolea Mbavuni eti Zacharia Hans Pope ndie alipangwa kuwa Rais!!!! Wakati Waratibu wa mpango huo Walitaka Thomas Lukangira au Uncle Tom Hata Hatib Gandhi au Hatty MCghee hakuandaliwa kuwa Rais Sembuse Hans Pope???
 
ii
Mimi napenda kujua kwa mwenye habari zinazohusu kesi ya uhain ktk miaka ya tisini na kifo cha komando tamimu kilitoke vp mwenye kujua aniabarishe hapa jamvin

Kesi ya uhaini ilifanyika mwaka 1983 na baadae watuhumiwa wakafungwa maisha.

Watuhumiwa wote idadi yao walikuwa 19 na miongozi mwao walikuwa ni Cpt Hatibu Hassan Ghandi au Hatty MacGhee, Cpt Metusela Suleiman Kamando, Zakaria Hans Pope, Cpt Vitalis Mapunda, Cpt Damas Mbogolo, Lt Badru Rwechungura Kajaja, Cpt Eugene Maganga na Lt. Christopher Kadego.

Wengine ni Christopher Ngaiza, Cpt Rodrick Rosham Robert na raia wengine wa kawaida.

Kesi ilifanyika katika mahakama kuu Kivukoni chini ya jaji Nasoro Mnzavas ambae baadae alikuja kuwa jaji Kiongozi.

Serikali iliwakilishwa na mawakili William Sekule na Johnson Mwanyika.

Mawakili wa utetezi waliongozwa na mawakili wawili matata Hussein Mukadam, Murtaza Lakha.

Inasemekana mzee Mabere Marando alikuwa ndie shahidi wa upande wa mashtaka akijulikana kama Mr X.

Mohamed Tamimu ambae ndie alikuwa anachukua notes katika mikutano pale Kijitonyama nyumbani kwa akina George Banyikwa na mkewe Zera Banyikwa, aliuwawa tarehe 6 January mwaka 1982.

Komando Tamimu alikuwa ni mzaliwa wa Tanga na kabila lake Mdigo na alikuwa ni mtoto wa Tanga mjini maana alikulia pale. Pia alikuwa anapanga nyumba pale Kinondoni Mkwajuni alipokutwa na mauti na kuuwawa na maofisa usalama na askari polisi.

Uncle Tamimu alikua ni mmoja wa watu wasioeleweka kwa kuwa kati ya marafiki zake, hakuna aliefahamu makazi yake na wapi aliishi khasa isipokuwa yeye aliwafahamu watu wote na mitaa yote waliyoishi hasa kule mitaa ya Nairobi.

Ila wazee Apson Mwang'onda na Hassy Kitine na timu yao walifahamu kwa sababu alikuwa ni jirani yao na kwa kuwa Komando Tamimu alipanga hapo kama "strategic point"(kuna wengine wataelewa namaanisha nini), ilikuwa rahisi kwa kikosi kazi kumfanyia pre-emptive strike.

Hatibu Hassan Ghandi au Hatty MacGhee nae alikuwa ni Mbondei mzaliwa wa Muheza Tanga kijiji cha Mafere na alikuwa ni rubani wa ndege ndogondogo.

Bosi wa mpango mzima ndio alikuwa Pius Rugangira au Uncle Tom (mzee wa noti) ambae alitorokea Nairobi na baadae London Uingereza.

Kesi ilihitimishwa kwa baadhi yao wakiwemo Hatty MacGhee na Maganga kufungwa maisha na Banyikwa na Mkewe waliachiwa huru.

Wengine walifungwa miaka michache na hawa wote walifungwa katika magereza tofauti nchi nzima.
 
..turushieni iyo link ya hii habari kama ilishawahi kujadiliwa huko nyuma
 
Nimejifunza kitu ambacho Hata sikuwahi kukiskia. Ahsante mtoa Mada. Kumbe Marando enzi hizo nae alikua nux...
 
hapa unamzungumzia Mhafoudh
 
Tamimu nilipata kumsoma katka masimulizi ya mjomba wa aliyekuwa rafik yangu capten Maganga na hata nilipofahamiana na capten kadego nilijifunza mengi kuhusu mpango wa mapinduz ya1982.muhusika mwingine ni huyu zakaria hanspope wa simba.
Ukiwasikiliza watu hawa ni watu makini na walikuwa na moyo wa kizalendo kwa nchi yao,bahati mbaya ni kwamba hawajaandikwa popote na wengi wao sasa ni marehem.Capten Kadegho sijui yuko wapi siku hiz,mzee Bagyemu Rweyongeza yeye yuko Bukoba
 
Huyu wa Simba naye alikuwa mhainj pamoja na komando mhamedi siku ya tukio?
 
Walifanya ujinga sana kukaa Kenya tu hapo! Halfu McGhee ndio mpuuzi kuliko wote! Nimejifunza kitu
 
GENTAMYCINE Haya mambo huyajui, wewe field yako ndombolo ya solo
 
Damn im so happy hivi tunawwza fanya movie ya hii kitu
THE FAILED COUP ATTEMPT

Anza na plan, kisha wanavyotekwa, kisha wanavyochomoka gerezani, wanavyohustle Nairobi, na wanavyorudishwa Dodoma, na kifungo chao cha Maisha, kisha wanaachiwa binge LA muvi ila akili na mtaji mzito
 
Alimpima vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…