Kesi ya urithi wa Marehemu Dkt. Mengi: Yaliyojiri Mahakamani

Kesi ya urithi wa Marehemu Dkt. Mengi: Yaliyojiri Mahakamani

Kwanini Jack asione hukumu hii ina mkono wa MUNGU hivyo akatubu na kuungana na familia yote kuliko laana ya baadae kwake na watoto malaika wadogo alioachiwa na mzee Mengi?
 
Humu nilishawahi kuuliza je dini ya Mengi inasemaje kuhusu mirathi ya watu wake?? Upo uzi hapa nashindwa kuupandisha
 
Humu nilishawahi kuuliza je dini ya Mengi inasemaje kuhusu mirathi ya watu wake?? Upo uzi hapa nashindwa kuupandisha
Dini gani Tena?
Inatambulika katika dini ya kikristo ambayo Mengi alikuwa muumini ndoa Ni moja mpaka kifo kitapapowatenganisha, lakini bwana Mengi kabla mke wa kwanza kufa alifunga ndoa nyingine sijui kwa dini ipi, hapo Kuna utata.

Kikristo watoto wote wanayo haki ya kurithi Mali za baba vinginevyo kuna sababu ambazo huwekwa wazi kiutaratibu, lakini pia kikabila la kichagga Kuna utaratibu wake pia Kama ilivyo kwa mujibu wa sheria ya nchi ya mirathi.

Marehemu sijui kwanini aliamua kuwatenga wanae dah, Tena watoto ambao wako dedicated katika kufanya shughuli za makampuni ya kifamilia, mama mdogo nae busara Hana na aibu Hana hata hajajali haki za watoto wanaomzidi hata umri dah!

Sijui ndio visasi na kuwakomesha kwamba kwakuwa hamkufurahianiolewe na baba yenu Sasa hamuambulii kitu.
 
Mimi nadhani ifike mahala mtu yeyote akimaliza kusoma kozi anayotaka basi asome hata kozi ya sheria kama nyongeza.
Hii itamsaidia kupunguza ujinga kwenye mambo yasiyohitaji kutumia nguvu bali akili.

Sheria zetu hapa tz hasa katiba na nyingine nyingine zina chenga chenga ila waliotunga sheria ya ndoa, mirathi...walitulia sana sheria hizi zimenyooka.

Wewe dada ulie na ndoto za kuolewa na tajili kwa tamaa zako nenda kwanza tuliza akili kazipitie ujue haki zako ni zipi.

Ndio sheria imempata mtoa wosia uhuru wa kugawa mali zake kwa watu anaowataka ila msisahau kuwa kila general rule ina exception.

Hata kama marehemu alitoa wosia huo, sisi tutaona wakati akitoa wosia huo alikuwa katika hali gani na je alifata utaratibu?

Mengi alikuwa mtu msomi haiwezekani hata kama hakusoma sheria atengeneze wosia ambao utaleta shida hapo baadae.

May be aliandika wosia huo wakiwa kwenye migogoro ya familiya.lakini mkumbuke wale watoto ameishi nao miaka mingi sana kuliko jack aloishi nae 5yrs.
Wewe dada Mambo ya kumuweka mzee kifuani ukaanza kumshawishi baba andika hivi, baba ongeza hiki hiyo hapana.

Jifunzeni kula na vipofu.

Na nyinyi marehemu huko mlipo mkishindwa kufata sheria nkaandika wosia utakaozua utata sisi tulioko duniani tutawasaidia kugawa mali mliozitafuta wenyewe.

Who knows? Dalili ya nvua ni mawingu. Wenda siku moja ntakuja angukia kwa mtu tiyari ana mali na watoto wake.ntamwambia baba mali hizi sio zangu nitengee unachoona kinafaa pembeni ila usiguse haki za watoto niliyowakuta hapa.mm sipendagi kelele.
 
Awe pisi kali tu akili tutatumia zangu.

Unaweza kuoa mcharuko na mali zikabaki mikono salama, hapa tatizo ni moja tu mzee Mengi alichelewa kuandaa mirathi na inaonekana aliandaa kienyeji too many loopholes, natilia mashaka uwezo wa wanasheria wake kwa mtu wa hadhi yake....
Kuna watu wana IQ kubwa!

Yaweza kuwa mzee huyo aliandika wosia wenye mapungufu kwa makusudi ili kumridhisha mshawishi, aone kwamba mzee anampenda na kumjali huku akilinda haiba yake na haki ya familia pana.

Haiwezekani tajiri aliyekuwa na wanasheria kuweza kuandaa document zenye mapungufu bila hao wanasheria kung'amua kuingilia na kushauri.
 
Sidhani angefanya ujinga huo ambao anajua ungepelekea kuleta mafarakano ya kifamilia
 
Sidhani angefanya ujinga huo ambao anajua ungepelekea kuleta mafarakano ya kifamilia
Hapa tunayageuza geuza maneno kama kutafiti ni nini kilisababisha wosia uwe na mapungufu hayo yote wakati marehemu alikuwa na wanasheria washauri nguli.

Je, wosia huo ni wa kughushi?

Je, waliokuja kutoa ushahidi walipangwa? Nk nk.
 
Mimi nadhani ifike mahala mtu yeyote akimaliza kusoma kozi anayotaka basi asome hata kozi ya sheria kama nyongeza.
Mind you ikitokea leo hii watu wote wakaamua kuwa wanaongea ukweli tu bila hata chembe ndogo ya uongo, basi tutakuwa hatuna tena haja ya kujua sheria wala kuwa na sheria
 
Sidhani angefanya ujinga huo ambao anajua ungepelekea kuleta mafarakano ya kifamilia
Kwa hiyo wewe unaamini kabisa kwamba Dk Mengi aliyekuwa anaingia mikataba na makampuni makubwa ya kimataifa anaweza kuwa na mawakili dhaifu kiasi washindwe kujua kwamba ili wosia uwe halali kisheria lazima unapoandikwa awepo ndugu wa mwandikaji?

Wasijue umuhimu wa wosia kuwa sealed,wasijue kwamba wosia haupaswi kukaa kwa mmoja wa wanufaika wake?
 
Back
Top Bottom