GE2025 Kesi ya wachokonozi kusikilizwa mfululizo kuanzia Septemba 15

GE2025 Kesi ya wachokonozi kusikilizwa mfululizo kuanzia Septemba 15

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kesi ya jinai inayowakabili wamiliki wa jukwaa la mtandaoni la Wachokonozi, Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko, Agosti 19, 2025, imeendelea katika Mahakama ya Wilaya ya Meru mbele ya Hakimu Sodeyeka, kwa kusomwa hoja za awali(ph)

Washitakiwa wote wawili walikanusha mashitaka mawili yanayowakabili, ambayo ni kuchapisha taarifa za uongo na kutoa maudhui mtandaoni bila kuwa na leseni

Wakili wa utetezi, Ally Mhyellah, amesema katika hoja za awali, zipo ambazo washitakiwa wamekubali na nyingine wamezikataa. Amezitaja hoja zilizokubaliwa kuwa ni majina na anwani zao sahihi.

Aidha, mshitakiwa wa kwanza, Jackson Kabalo, alikiri kupakia video yenye maneno yaliyosababisha kufunguliwa kwa shauri hilo. Video hiyo ilihusisha kauli: "Mimi ninachokiona, Wachina wataendelea kuja, na sasa hivi tena nasikia tumewapa reli ya TAZARA miaka 27. Tumebakiza kuwapa Ikulu waiendeshe, kwa sababu bandari tumetoa, reli tumetoa, mwendokasi tutawapa; kilichobaki ni kuwapa TANESCO na Ikulu”.

Hata hivyo, mshitakiwa wa pili, Joseph Mrindoko, alikana kuhusika na upakiaji wa video hiyo.

Shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa kwa mfululizo kuanzia Septemba 15 na16, 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya Meru.
 
Back
Top Bottom