PostGE2025 Mgongano wa Kikatiba Wazuka Mahakama Kuu Zanzibar Katika Kesi za Wagombea Ubunge ACT

PostGE2025 Mgongano wa Kikatiba Wazuka Mahakama Kuu Zanzibar Katika Kesi za Wagombea Ubunge ACT

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mgongano wa kikatiba umejitokeza katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kufuatia kesi zilizofunguliwa na waliokuwa wagombea wa Ubunge kupitia Chama cha ACT-WAZALENDO kwa majimbo 19 ya Unguja

Mgongano huo umeibuka leo mbele ya Jaji Hajji Suleiman Khamis katika Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Tunguu, wakati Mwanasheria mwanandamizi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipodai kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar haina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya wabunge yanayohusiana na mambo ya Uchaguzi.

b6bb73a2-fef8-4c75-87b9-13ef0a95160e.jpeg
469c6a19-a229-4e9d-946a-5df0e4d39604.jpeg
Mwanasheria wa Serikali, Bi. Nalindwa Sekimanga, akiwa miongoni mwa jopo la wanasheria kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano, alitaja vifungu mbalimbali vya kisheria, ikiwemo Ibara ya 83 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kinachobainisha kuwa mashauri yote ya uchaguzi yanayohusu Wabunge yatasikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kutokana na hoja hiyo, Sekimanga aliomba Mahakama ikubali pingamizi lililowasilishwa na upande wa Serikali, akisisitiza kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar haina uwezo wa kikatiba kusikiliza mashauri yanayohusu mambo ya Uchaguzi wa Wabunge wa Jamuhuri.

629d37ff-4150-41c2-9559-2c2d6b8e5344.jpeg
Kwa upande wao, mawakili wasomi wanaowawakilisha waliokuwa wagombea Ubunge wa ACT-WAZALENDO, wakiongozwa na Wakili Msomi Omar Said Shaaban, alipinga hoja hiyo akieleza kuwa Mahakama Kuu ya Zanzibar ina mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusiana na Muungano.

Shaaban alikinukuu kifungu cha 93(1) cha Katiba ya Zanzibar na kifungu cha 3(1)(a) cha sheria Na.2 ya 1985 kuwa ndio kinachoianzisha, na kuipa mamlaka Mahakama Kuu ya Zanzibar na kwamba mamlaka iliyopewa ni bila ya Kikomo (unlimited) kwa mambo yote na sheria zote zinazotumika Zanzibar ikiwemo za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotungwa na Bunge kama ilivyo sheria ya Uchaguzi. Hivyo Mamlaka ya Mahakama Kuu Zanzibar hayaondolewi wala hayapimiwi na Ibara ya 83 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano katika ngazi ya Mahakama Kuu.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama imeahirisha kesi hizo hadi tarehe 27 Januari 2026, kwa ajili ya kutoa uamuzi juu ya pingamizi la kikatiba lililowasilishwa na wanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

IMETOLEWA NA IDARA HABARI NA UENEZI ACT WAZALENDO
 
Haya matatizo aliyatengeneza J.Kikwete na Aman Karume 2010
Mawakili wa ACT Wazalendo wapo sahihi kwa kesi kusikilizwa Zanzibar kwa shauri la Wabunge wa Muungano

Katiba ya Zanzibar (1984) ina ukuu wa kimamlaka dhidi ya ile ya JMT(1977). Sheria zinazotungwa na Bunge la JMT lazima ziidhinishwe na Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zbar. Maana yake ni kwamba Katiba ya SMZ ina ukuu dhidi ya ile ya JMT.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar 2010 ndiyo iliyonyang'anya Mahakama kuu ya JMT baadhi ya mamlaka. Kuna mashauri hayawezi kuletwa JMT. Ni yale yale ya Amir Jeshi Mkuu wa JMT na Amir Jeshi Mkuu wa SMZ. Yaani tuna Maamir Jeshi wakuu 2 katika Nchi moja

Mkanganyiko ni pale shauri hilo litamalizwa iwe Mahakama kuu au Mahakama kuu Zanzibar.
Wabunge wa Zanzibar wanapovuka Bahari, gharama zao ni za JMT a.k.a Tanganyika hata kama shauri lao limemalizwa Kizanzibar. SMZ haihusiki na mzigo wa gharama

Ni vurugu tupu! Tanganyika , halafu kama Wazanzibar wakitaka kuwe na serikali ya Muungano! ndogo.
Ni kama watataka kwasababu Watanganyika hawana cha kupoteza

JokaKuu
 
Upuuzi mtupu. ACT si mlipewa mpaka magari ya kupigia misele kuhalalisha ushetani? Ya nini kuwasumbua waliokuwa wamewaajiri?
Ikiw a ni hivyo nanyi si mlipewa nafasi kushiriki kwenye uchaguzi mukasusia halafu mukaandamana? Yanini kuwasumbua ACT Wazalendo? Oh Mdanganyika!!
 
Haya matatizo aliyatengeneza J.Kikwete na Aman Karume 2010
Mawakili wa ACT Wazalendo wapo sahihi kwa kesi kusikilizwa Zanzibar kwa shauri la Wabunge wa Muungano

Katiba ya Zanzibar (1984) ina ukuu wa kimamlaka dhidi ya ile ya JMT(1977). Sheria zinazotungwa na Bunge la JMT lazima ziidhinishwe na Baraza la Wawakilishi kabla ya kutumika Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zbar. Maana yake ni kwamba Katiba ya SMZ ina ukuu dhidi ya ile ya JMT.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar 2010 ndiyo iliyonyang'anya Mahakama kuu ya JMT baadhi ya mamlaka. Kuna mashauri hayawezi kuletwa JMT. Ni yale yale ya Amir Jeshi Mkuu wa JMT na Amir Jeshi Mkuu wa SMZ. Yaani tuna Maamir Jeshi wakuu 2 katika Nchi moja

Mkanganyiko ni pale shauri hilo litamalizwa iwe Mahakama kuu au Mahakama kuu Zanzibar.
Wabunge wa Zanzibar wanapovuka Bahari, gharama zao ni za JMT a.k.a Tanganyika hata kama shauri lao limemalizwa Kizanzibar. SMZ haihusiki na mzigo wa gharama

Ni vurugu tupu! Tanganyika , halafu kama Wazanzibar wakitaka kuwe na serikali ya Muungano! ndogo.
Ni kama watataka kwasababu Watanganyika hawana cha kupoteza

JokaKuu
Tatizo hapa wanasheria bara ni wanaccm tupu hawana uelewa wa mambo
 
Back
Top Bottom