PreGE2025 Kesi ya waliojaribu kumteka Tarimo kuendelea June 9 na 10, 2025. Kwanini imekuwa ngumu kupata taarifa za kesi hii?

PreGE2025 Kesi ya waliojaribu kumteka Tarimo kuendelea June 9 na 10, 2025. Kwanini imekuwa ngumu kupata taarifa za kesi hii?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
284
Reaction score
870
images (83).jpeg

Kwa taarifa zilizopo kwa kumulika kwelikweli na tochi ni kuwa kesi ya wale jamaa waliojaribu kumteka Tarimo A.K.A Bonge itaendelea June 9 na 10, 2025. Kwanini itakuwa siku mbili, hata mimi mwenyewe sijui, labda wanasheria watueleze vizuri kuhusu hili.

Tukija kwenye sehemu ya pili, toka wakati tulipopata taarifa kuwa watekaji walitaka kumlawiti Tarimo ndio ukawa mwisho wa kupata updates. Yaani imekuwa ziiiii, jambo linaloshangaza hasa ukizingatia ni kesi yenye maslahi kwa umma.

Kuna watu wanazuia waandishi wa habari kufuatilia kesi hii? Kuna vitisho vinapita katikati watu kujitoa kufuatilia kesi hii?

Maana inashangaza kwa mara ya kwanza waliojaribu kufanya utekaji walidakwa, wanatambulika mtaani mpaka sehemu walipokuwa wanafanyia kazi. Kwanini iwe changamoto kupata mwenendo wa kesi hii inavyoendelea?

Kuna mdau amekuwa anatuma update hapa lakini tunaona jinsi taarifa zinavyokuja kwa uchache, hatupati kwa undani juu ya kinachoendelea, yaani tupo gizani.

Je, kuna juhudi za makusudi zinafanywa ili wananchi tuache kufuatilia na jamaa waendelee na mambo yao ya utekaji kama hakuna kilichotokea? Kuna mkono wa mtu mkubwa anazuia hili lisifike mwisho?

 
Naona unajiuliza majibu kwenye paragraph yako ya mwisho mkuu wa watekaji tumeshamjua
 
Aisee! Hawa jamaa tukiwaona sehemu yoyote wanafanya huu ujinga tuwe tunawapiga mawe..
 
Naona unajiuliza majibu kwenye paragraph yako ya mwisho mkuu wa watekaji tumeshamjua
Haitoshi tu kumjua, tunataka wachukuliwe hatua, watarudi mtaani safari hii watakuwa wamejipanga zaidi wasiweze kuonekana
 
Ukweli wa hii kesi anaujuwa mwenyewe tarimo!

Ova
 
Back
Top Bottom