DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kesi ya jinai iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya waliokuwa wamiliki wa jengo la ghorofa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam lililoporomoka Novemba 16.2024 imeendelea leo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mhini leo, Alhamisi Septemba 18.2025 imekuja Mahakamani hapo kwaajili ya kufanya mwenendo wa shauri la ukabidhi (commital proceedings), hata hivyo jambo hilo sasa limepangiwa tarehe nyingine baada ya kesi kuahirishwa leo
Wakili wa Serikali Mwandamizi Clemence Kato ameieleza Mahakama kuwa Jamhuri ina mashahidi zaidi ya 100 wa kesi hiyo, na kwamba upelelezi wa kesi husika umekamilika, hata hivyo Jamhuri imeomba kesi hiyo isogezwe mbele kutokana na kile kilichoelezwa kuwa haiwezi kuendelea na kesi hiyo siku ya leo kwasababu uchapaji wa maelezo ya mashahidi wa Jamhuri hayajakamilika ingawa zaidi ya nusu ya mashahidi maelezo yao yameshachapwa
Ikimbukwe kuwa watu sita (6) wanashtakiwa kwa kosa la kuuwa bila kukusudia katika kesi hiyo ambao ni Ashur Awadhi, Zainab Ashur, Leondera Mdete, Sostel Mziku na Steven Mziku
Mawakili wa utetezi katika kesi hiyo ni Denio Msemwa, Francis Makota, Obedi Mwandambo na Idd Kasi, huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Clemence Kato.
Kesi hiyo, ina maslahi mapana na kesi ya madai iliyofunguliwa na wafanyabiashara zaidi ya 100 waliokuwa wamepanga kwenye jengo hilo, ambao wamefungua kesi kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi wakidai fidia ya zaidi bilioni 40 kutoka kwa waliokuwa wamiliki wa jengo hilo pia
Kwenye kesi ya madai, wafanyabiashara hao wanasema kuanguka kwa ghorofa hilo kumewasabishia hasara ya mali, wenzao kupoteza maisha nk
Leo wafanyabiashara hao waliofungua kesi ya madai Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi wakiongozwa na Wakili wao Peter Madeleka, wamejitokeza kwa wingi pia kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya kuua bila kukusudia inayowakabili wadai wao, huku ikidaiwa kuwa wengi wa wafanyabiashara hao ni mashahidi wa Jamhuri kwenye kesi ya jinai iliyoko Kisutu.
Soma Pia: Wafanyabiashara Kariakoo wadai fidia TSh. bilioni 40 jengo kuporomoka