JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kesi inayomkabili Diana Bundala maarufu kama mfalme Zumaridi na wafuasi wake imeshindwa kuendelea leo Oktoba 17, 2022 baada ya mtuhumiwa huyo kudai kuwa ana maumivu makali ya mguu na kuomba kesi hiyo ihairishwe ili apate matibabu.
Mfalme Zumaridi alitarajiwa kuanza kujitetea leo katika kesi inayomkabili yeye na wafuasi wake ya kuwazuia maafisa wa serikali kutekeleza majukumu yao pamoja na kuwajeruhi Askari Polisi.
Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo, Februari 23 mwaka huu nyumbani kwa Zumaridi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa jijini Mwanza kinyume na kifungu namba 241, 243 (b) na 114 (a) na (b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Hakimu Ndyekobora amesema mahakama imewakuta washtakiwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa mashahidi 12 na vielelezo 11.