Kesi ya ZZK ina makosa mengi

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Mchezaji wa simba sports club akihisi coacher hatampanga kwenye mechi anaweza kwenda mahakamani kuzuia mechi isichezwe kwasababu ya hisia kuwa hatapangwa na atapata loss kwa washabiki wake, na fedha ya mechi ya siku.

Jaji atasaidia wengi sana kwenye vyama vya siasa wana hisi vikao vikikaa hawawezi kutendewa haki. Itakuwaje kwenye kura za maoni ambapo kuna wengi huwa wanakatwa majina na vyama vyao, Je hukumu hii si italeta kasheshe kwenye utendaji wa kila siku wa vyama vya siasa, makampuni, na taasisi mbalimbali?

Kesi hii ni kesi ya kipuuzi kabisa kuwahi kufunguliwa kwenye uwanja wa sheria? Sioni ni jinsi gani Jaji wa mahakama kuu atatoa hukumu kwa hisia. Sheria ni pamoja na material evidence, huwezi kuwa na hisia ukashinda kesi.

Kesi hii hata kama ina mkono wa Ikulu labda jaji awe mwehu kabisa. Kweli unazuia kikao cha chama kisikae eti unahisi utafukuzwa chama? Unazuia usijadiliwa kwa hisia utanyang'anywa kadi? Ni vipi mahakama inazuia chama kisisimamie maadili na sheria, kanuni na kanuni zake. Je Ni lazima kuwa mwanachama wa chama fulani is it enforceable by law kuwepo kwenye siasa? Kweli hii ni sababu ya kwenda mahakamani? Kwanini usisubiri ufukuzwe ndio uende mahakamni.

Posho, mshahara, ajira ndio vinapiganiwa sasa. Wasiwasi wangu ni kuwa wakili wa ZZK amemwingiza ZZK choo cha kike bila ya zito kujijua. Ajira Hapa TZ ngumu, Zito katangaza dau kubwa wakili kasema twende mzigo. Ushauri wa kisheria haujazingatiwa zaidi ya panic na kukurupuka.

Naamini kesi hii itatupwa.
 
Nachoona ni ndoto ya huyu kijana kufifia ghafla kama ya ile ya Mrema Lyatonga, namshauri Zito ni heri angeondoka mwenyewe kuliko kusubiri Ubunge wa mahakama angejijengea sifa, Kama alipokelewa na wafuasi wake kwa wingi iweje leo anaogopa kuondoka akanzishe chama chake au aende, NCCR kwa wenziye, Hafu nadhani wanasiasa vijana wanalo la kujifunza hapa.
 
Siasa imeingiliwa na tamaa ya utajiri sio kutumikia watu. Uwezo wa kizazi cha sasa kuwa wavumilivu unapungua na kuondoa umakini. Hakuna kiongozi malaika na huwezi kukubaliana na kila mtu, ZZK, Msando, kinachowasumbua ni tamaa tu ya madaraka fedha, na utukufu.
 
Kwa Tanzania hizi ndo kesi zinazopewa kipaumbele.siajabu kuna msukumo wa watu wazito nje ya CDM na kumtumia ZZK kuyumbisha chama.katika hili usitegemee kuwa kesi hii itatupwa kirahisi.
 
lazima ukweli liwekwe wazi kwa maslai ya taifa na siyo kutishia watu kwa maslai ya watu waovu zito ajiondoe mwenyewe kwani imethibitika wazi anatiuwa na serekali ya ccm kuivuruga chadema na democrasia nchini kwani hata kesi inayoendelea mahakama aliyeidrafti ni jaji alitambulika kwa jina la makaranga na kuituma kwa wakili msando kupitia e-mail adress ili yeye akafungua kesi mahakamani kama alivyofanya na nyaraka hiyo ilishakatwa kwenye mawasiliano ya wakili msando na jaji makaranga je ni halali kwa jaji kumsaidia wakili kuandaa kesi wakati wao ndiyo waamuzi wa kesi zinazofunguliwa mahakamani na hii inaweza kuaribu maamuzi ya mahakama, kama baadhi ya majaji wanashriki kuleta vurungu ndani ya vyama ni makosa makubwa sana na aipaswi kuvumiliwa na wananchi wapenda democrasia aifai hata kidogo
 

kamanda unaushahidi wa hii tuhuma ...... it is serious accusation. Leta email na mawasiliano tuanzie hapo.
 
Jamani kweli common sense is not common! najaribu kufikiria linearly kwamba vigogo wa ccm na selikali wamfacilitate zito mpaka akarudi kwenye nafasi yake kichama kama anavo taka! hivi ataongoza na akina nani? (viongozi wenzake) nashawishika kuamini kuwa anakomalia nafasi hizo ili apate nafasi nzuri ya kudumaza, chama!
 
Zitto analazimisha uanachama baada ya kuvurunda!anapaswa aadhibiwe kwa kuvuliwa uanachama na wapenzi wake.ahamie huko wanakomuunga mkono,aone kama umaarufu wake utaendelea.
Huo ndio mwisho wa umaarufu wake kisiasa na kijamii.
 

Tatizo hujui sheria ndo maana unakimbilia kufungua thread mpya na kutumia maneno ya Mh. Tundu Lissu!!

Wewe mwenyewe umeandika kwa hisia bila kuwa na facts, halafu una washangaa waliofungua kesi!! Kweli Nyani haoni kundule.
 
Khaa!! Kweli hii kesi ni mauzauza tangu kuanza kwake hasa pale ZZK alipotaka kugombea nafasi ya Mkiti
 
Tatizo hujui sheria ndo maana unakimbilia kufungua thread mpya na kutumia maneno ya Mh. Tundu Lissu!!

Wewe mwenyewe umeandika kwa hisia bila kuwa na facts, halafu una washangaa waliofungua kesi!! Kweli Nyani haoni kundule.

Ni kweli mimi sio mwanasheria, naomba wewe unieleweshe nini alichokisema Msando mteja wake anachokiomba. Nitashukuru sana kwa elimu yako.
 
Khaa!! Kweli hii kesi ni mauzauza tangu kuanza kwake hasa pale ZZK alipotaka kugombea nafasi ya Mkiti

Eti chama kinahubiri Demokrasia,wanamuita Zitto na kumzuia kugombea ueneyekiti.Kwa nini hawakusubiri wajumbe waamue?Sasa CHEDEMA ina tofauti gani na CCM?bora hata nyerere aliacha kura ziamue kati ya JK na Mkapa,Pamoja na kwamba yeye alimpenda Mkapa
 

zitto zuberi kabwe anatumia anatumia akili ya MADRASA badala ya akili yake kama mchumi mwenye MASTERS YA UCHUMI!

CC: Ritz, FaizaFoxy
 
Channel ten wamemuonyesha Msando kwa kweli amesawajika yaani utamuonea huruma Zitto macho kma alikua aalia kwa kweli wanasikitisha kwa maamuzi yao ya kukurupuka
 
Eti chama kinahubiri Demokrasia,wanamuita Zitto na kumzuia kugombea ueneyekiti.Kwa nini hawakusubiri wajumbe waamue?Sasa CHEDEMA ina tofauti gani na CCM?bora hata nyerere aliacha kura ziamue kati ya JK na Mkapa,Pamoja na kwamba yeye alimpenda Mkapa
Usijitoe akili dada mdogo hivi nafasi ya mwenyekiti wa CCM,hata iliyokuwa Tanu wenyeviti waligombea na nani leo hii Mangula yupo channel ten analalamika sana kuhusu waasi wa CCM wanaotaka kupora madaraka sasa demokrasia gani ya CCM unayoiota
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…