Kesi za kisiasa zinaharakishwa kuliko za kawaida

Kesi za kisiasa zinaharakishwa kuliko za kawaida

Kimali

Member
Joined
Oct 25, 2011
Posts
26
Reaction score
8
Wanasheria na serikali nisaidieni kujibu hii hoja.
1. Ni kwa nini kesi zinazohusu mambo ya siasa zinaharakishwa kusikilizwa na kutolewa hukumu ndani ya kipindi kifupi. Mfano wa kesi za uchaguzi zimesikilizwa kwa muda mfupi na sasa ni karibu zote zimeisha. Pia kesi zinazohusu uchochezi wa mambo ya kisiasa nazo pia hufanyiwa upelelezi haraka na kusikilizwa haraka na hukumu kutolewa ndani muda mfupi. Ila inasikitisha kuona kuwa kesi ambazo za jinai ambazo sio za kisiasa, upelelezi wake unachukua muda mrefu sana na hata upelelezi ukishakamilika usikilizwaji wake unachukua muda mrefu sana. Hata kama mashahidi wote wapo lakini waendesha mashtaka wanaleta shaidi mmoja kila mwezi na wakati mwingine hawafiki mahakamani kwa sababu zisizo za msingi.
2. Kesi nyingi za watumishi wanapokuwa wameshtakiwa na serikali au mwajiri mahakamani zinachukua muda mrefu sana kufanyiwa upepelezi. Na pia pale ambapo upelelezi wa kesi umeshakamilika waendesha mashtaka wa serikali hawafanyi haraka kukamilisha usikilizwaji wa kesi husika jambo ambalo linawagharimu sana watumishi husika na pia serikali yenyewe.
 
Ni kwa sababu kesi za Siasa zina manufaa kwa "Uwepo" wa Serikali madarakani ktk kuwatokomeza Wapinzani wao ili waendelee kutawala bila karaha
 
Na kweli kuna watumishi wamesimamishwa kazi mda wanaendelea tu kula mishahara bila kufanya kazi hili nalo ni tatizo
 
Back
Top Bottom