mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Tanzania yenye neema.waliahidiwa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ngoja nimpigie Donald Trump atume wale jamaa wanaotaka kupima akili zake wàanze na wewe wakati yale madawa yakiwa bado hayajaghushiwa. Utakuwa na ma tatizo makubwa kwenye ubongo wako. Tena ninadhani ni fungusKESI ZA KUMTUKANA RAIS ZINAONGEZEKA,
KUNA NJIA RAHISI YA KUMALIZA TATIZO :
Jana nimesoma tena kwamba kuna mwanamke Mbeya amefikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana - kosa ni kumtukana Rais kwenye mtandao wa Facebook.
Kesi za kumtukana au kumkashifu Rais zipo nyingi tu kwa sasa,
zikihusisha wanasiasa na wananchi wa kawaida.
Kwa nini zaidi katika awamu hii ya uongozi?
Tukiri kuna tatizo mahali.
Mficha maradhi,
Basi kifo humuumbua.
Wala suluhisho SIO kutumia kila njia kutafuta wanaomtukana na kumkashifu ili kuwafungwa jela!
Falsafa zinasema,
ili kumaliza tatizo rekebisha chanzo,
sio ishara au matokeo yake.
Ni vema basi,
Rais wetu na washauri wake,
kujiuliza kwa nini hili jambo linazidi kuwa kubwa.
Inawezekana kabisa ikawa kwamba wananchi wa Tanzania wana hasira na Rais wao kwa kuwa hawamwelewi.
Badala ya kuagiza kamata kamata,
wafikirie namna ya kuboresha mawasiliano na wananchi.
Wakati wa Nyerere,
baada ya vita vya Kagera,
Tanzania ilipitia kipindi kigumu ambacho sidhani kama kitakuja kutokea tena.
Mwalimu Nyerere alikuwa hodari wa kuelewesha wananchi wake,
na hatukuona matukio ya kutukana sio kwa sababu tu hakukuwa na Facebook na WhatsApp
Groups wakati huo.
Watu waliendelea kumpenda Nyerere na hata kuitikia wito wake wa
"tujifunge mikanda miezi 18",
ambayo iliendelea sana tu.
Watu walikosa sukari hadi chumvi,
lakini hukusikia watu wakitukana hovyo kila kona.
Kwa nini kipindi hiki watu watukane kila kukicha?
Ni suala la kujiuliza sana.
Hakuna rais anayetukanwa kwa maoni yangu. Watu wanatoa opinion zao; kitu ambacho ni haki, watu wanaikosoa serikali na rais wao; ila yeye anajiona ni Mungu. Hataki kusikia na kukubali kuwa yeye ni binadamu. Anakosea halafu hataki kuambiwa. Lazima watu wapate hasira wapaze sauti. Na the best rais angefanya, ni kuifuta rasmi katiba na kusema mfumo utakaotumika ni ule atakaoamua yeye mwenyewe kila siku asubuhi.
Una uhakika na unachokinena? Really?Nyerere ndie Rais aliekuwa anachukiwa zaid na Watanzania.
Kakoswa koswa kupinduliwa Mara nane
Hakuna Mwaka wa Uchaguzi ambao alipata kura nyingi kuliko Kura za Miaka mitano iliyopita japo Hapakuwa na uhuru wala Demokrasia
Mgombea wake 1985 Mzee Rashed Kawawa alipigwa chini na Wajumbe WA NEC na kumchagua Ally Hassan Mwinyi
Of course kutukana mtu yeyote Siyo tu ni kosa bali pia ni dhambi. Nilidhani mleta mada angesema kumkosoa lakini kutukana siyoHili jambo unalichukulia kirahisirahisi kulitolea majibu.
Wote wanaomtukana rais ni watu waliokaririshwa chuki na wanasiasa pamoja na mafisadi. Pia elimu zao zinamushkeri.
Ukichunguza watukanaji wote wanaotupwa jela, wanatukana kishabiki kwa kukaririshwa. Mtukanaji yeyote ukimchukua aeleze kwa hoja za msingi, sababu iliyopelekea kutukana watawala, atakuwa na majibu ya kiujumla ama chuki.
Yote tunayoyaona hivi sasa yana nafuu kuliko baadhi ya tawala zilizopita huko nyuma, hasa awamu ya kwanza.
Mambo ya njaa, ukame, ukosefu wa ajira, ugumu wa upatikanaji wa fedha nk. Yote yalikuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyo hivi sasa na kila utawala ulikuwa na mbinu zake namna ya kutatua changamoto zake.
Hii kitu inayoitwa haki za binadamu, baadhi ya raia wenzetu inawapotosha na kujiona wana haki ya kufanya lolote, hata kama jambo hilo linaenda kinyume cha maadili.
Una uhakika na unachokinena? Really?
Mbona yeye aliita watu vilaza??Hili jambo unalichukulia kirahisirahisi kulitolea majibu.
Wote wanaomtukana rais ni watu waliokaririshwa chuki na wanasiasa pamoja na mafisadi. Pia elimu zao zinamushkeri.
Ukichunguza watukanaji wote wanaotupwa jela, wanatukana kishabiki kwa kukaririshwa. Mtukanaji yeyote ukimchukua aeleze kwa hoja za msingi, sababu iliyopelekea kutukana watawala, atakuwa na majibu ya kiujumla ama chuki.
Yote tunayoyaona hivi sasa yana nafuu kuliko baadhi ya tawala zilizopita huko nyuma, hasa awamu ya kwanza.
Mambo ya njaa, ukame, ukosefu wa ajira, ugumu wa upatikanaji wa fedha nk. Yote yalikuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyo hivi sasa na kila utawala ulikuwa na mbinu zake namna ya kutatua changamoto zake.
Hii kitu inayoitwa haki za binadamu, baadhi ya raia wenzetu inawapotosha na kujiona wana haki ya kufanya lolote, hata kama jambo hilo linaenda kinyume cha maadili.
Soln
KUACHA KUTUKANA